Saturday, September 29, 2007

Warioba amekuwaje?


Sielewi Jaji Joseph Sinde Warioba amekuwaje. Kiongozi mstaafu, mwanasheria mstaafu na mtu aliyewahi kuongoza tume ya rushwa anaposema 'tuhuma hizi si mpya,' anataka kusema alitarajia kuona mpya zipi? Au alitaka hizi za zamani ziachwe tu? Simwelewi. Namshangaa pia anapoona kwamba kujadili rushwa ya wakubwa si muhimu kwa maendeleo ya nchi. Zaidi nipale anapopata shida kuelewa kwanini rais na rais mstaafu wanatuhumiwa. Nadhani angepaswa kuwashangaa wao na kujiuliza: "kwanini watuhumiwe? Kwanini wao na si wengine?" Badala yake, anawatetea kana kwamba anatoa 'hukumu kuwasafisha.' Bado simwelewi. Hivi hajui kwamba Tanzania itakuwapo bila yeye wala Jakaya Kikwete au Benjamin Mkapa?

Wednesday, September 19, 2007

Wonders of Mathematics

Bofya hapa uone maajabu ya HESABU - The Wonders of Mathematics. Nimetumiwa na rafiki yangu.

Kingunge ang'atuke


Pamoja na mambo mengine, natoa wito. Mheshimiwa Kingunge Ngombale-Mwiru ang'atuke. Badala ya kushauri vijana wake wajiheshimu n akutimiza wajibu wao, anafanya kazi ya mganga wa jadi kwenye masuala mazito! Naona Mpayukaji tayari ameniunga mkono.

Monday, September 17, 2007

Salva Rweyemamu ateuliwa mkurugenzi Ikulu


Salva Rweyemamu (pichani), aliyekuwa mkurugenzi wa Habari Corporation, ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Ikulu. Anaziba nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kallaghe aliyepelekwa Canada. Mwingine anayeonekana pichani kulia ni Dk. Gideon Shoo. Picha: Issa Michuzi

Dansi la Tanzania latesa majuu


The Ngoma Africa Band inayoongozwa na Ebrahima Makunja, a.k.a Ras Ebby Makunja "Bwana Kichwa Ngumu" imepata mashabiki wa kutisha jijini Frankfurt, Ujerumani. Msemakweli kaniandikia na kusema maelfu ya watu wa matabaka na mataifa mbalimbali jana usiku "walijikuta wanapelekwa mchaka mchaka na mlindimbo wa muziki huo Bongo Dance made in Tanzania... Nyimbo zao pia zinatesa katika redio mbalimbali Ulaya, Africa, Marekani na Canada...Unaweza kuwasikilza online hapa www.myspace.com/thengomaafrica"

Sunday, September 16, 2007

Hawa ndio wala nchi?


Hili ndilo linaitwa sasa kundi la wala nchi. Gazeti la Serikali, Habari Leo Jumapili, tarehe 16. Septemba 2007, limemnukuu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willibord Slaa, akiwataja 11 bora wanaodaiwa kushiriki katika ulaji na uuzaji nchi kwa namna moja au nyingine, kutokana na nyadhifa zao za kisiasa, kitaaluma au kwa sababu ya uwakala au ukaribu wao na wenye madaraka. Waliotajwa ni:
1. Rais Jakaya Kikwete

2. Rais Mstaafu Benjamin Mkapa

3. Waziri Mkuu Edward Lowassa

4. Waziri wa Nishati na Madini Nazir Karamagi

5. Waziri wa Miundombinu Andrew Chenge

6. Waziri wa Viwanda na Biashara Basil Mramba

7. Gavana wa Benki Kuu (BoT) Daudi Balali

8. Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Gray Mgonja

9. Katibu Mkuu Wizara ya Maji Patrick Rutabanzibwa

10. Mbunge wa Musoma Vijijini Nimrod Mkono
11. Mbunge wa Igunga Rostam Aziz (pichani juu).
. Tuhuma zao kamili hizi hapa.
Je, unajua kuwa Mwalimu Nyerere alisema CCM sasa inatumia pesa za bangi kupata viongozi?

MAISHA: Enjoy the jokes

Someone sent me these 2 jokes, and I thought my readers would enjoy them.


A young man went to his father one day to tell him that he wanted to get married. His father was happy for him. He asked his son who the girl was and he told him that it was Samantha, a girl from the neighborhood. With a sad face, the old man said to his son, "I'm sorry to say this son but I have to, the girl you want to marry is your sister, but please don't tell your mother". The young man again brought 3 more names to his father but ended up frustrated because the response was still the same. So he decided to go to his mother. "Mama I want to get married but I can't marry any of the girls that I love because dad said they are my sisters and I must not tell you". His mother said to him with a smile, "Don't worry my son, you can marry any of those girls. You are not his son anyway, but please don't tell him".

The mathematics behind our life span.

God created the dog and said: "Sit all day by the door of your house and bark at anyone Who comes in or walks past. For this, I will give you a life Span of twenty years." The dog said: "That's a long time to be barking. Howabout only ten years and I'll give you back the otherten?" So God agreed.

God then created the monkey and said: "Entertain people, do tricks, and make them laugh. For this, I'llgive you a twenty-year life span."The monkey said: "Monkey tricks for twenty years?That's a pretty long time to perform. How aboutI give you back ten like the Dog did?" And God agreed.

God then created the cow and said: "You must go intothe field with the farmer all day long and suffer under the sun, have calves and give milk to support the farmer's family. For this, I will give you a lifespan of sixty years." The cow said: "That's kind of a tough life you wantme to live for sixty years. How about twenty and I'llgive back the other forty?" And God agreed again.

God created man and said: "Eat, sleep, play, marry and enjoy your life. For this, I'll give you twenty years." But man said: "Only twenty years? Could you possibly give me my twenty,the forty the cow gave back, the ten the monkey gave back, and the ten the dog gaveback; that makes eighty, okay?" "Okay," said God, "You asked for it."

So that is why for our first twenty years we eat,sleep, play and enjoy ourselves. For the next forty years we slave in the sun to support our family. For the next ten years we do monkey tricks to entertain the grandchildren. And for the last ten years we sit on the front porchand bark at everyone. Life has now been explained to you.

Saturday, September 15, 2007

Pole Mheshimiwa Mudhihir


Mbunge wa Mchinga (CCM), Mudhihir Mohammed Mudhihir akipokewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam, Ijumaa septemba 14. 2007, akitokea Lindi alikopata ajali ya gari. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Saidi Mecky Sadick. Picha kutoka Daily News.

Ajali haina kinga. Yaliyompata Mudhihir yanaweza kumpata mtu yeyote. Zaidi ya hayo yanawapa abiria wengi katika ajali za barabarani na angani kila siku. La msingi, tumshukuru Mungu kwamba Mudhihir yuko hai. Tumpe pole na kumwombea apone haraka.

Hapa ilikuwa zamu yangu


Huyo aliyeketi kwenye kiti ni Profesa Guy Berger, mkuu wa kitivo cha uandishi wa habari katika Chuo Kikuu cha Rhodes. Ndiye alikuwa mwenyekiti wa mdahalo wetu. Ukutani ni picha kutoka kwenye Power Point presentation niliyokuwa natoa mimi. Huyo aliyesimama mbele kulia, ndiye mimi.
NETucation walinihoji kidogo na kutoa stori yao kwa Youtube.
Baadaye, AllAfrica walitoa stori yangu iliyoandikwa na Rebecca Wanjiku wa Kenya. BIZCOMMUNITY.com nao wakaitumia kwa headline tofauti.
David Musoke wa Uganda hakubaki nyuma. Sarah Bel wa APC alipendezwa na hoja yangu kuhusu haja ya kupeleka intaneti vijijini. Hii ndiyo stori yake. Mail&Guardian waliandika stori hii na kukosea jina langu.

Wajumbe wakitoka ukumbini baada ya kutusikiliza tukitoa mada zetu. Alianza Ndesanjo Macha, akafuatia Daudi Were, baadaye mimi. Tazama ratiba.

Wednesday, September 12, 2007

Mwanablogu mpya wa kike Mtanzania


Furaha Thonya, mwandishi wa kike wa kujitegemea wa magazeti ya ThisDay na Kulikoni, amejiunga na jamii ya wanablogu. Msome hapa. Pichani ni Ndesanjo Macha, Ansbert Ngurumo, Furaha Thonya na Philemon Msangi (Bob Sankofa) Jumapili 9. Septemba 2007, nje ya ukumbi wa mikutano.

Tuesday, September 11, 2007

Mtazame Ndesanjo akitoa mhadhara


Hii ilikuwa tarehe 9.9.2007 katika Ukumbi wa Barrat, Chuo Kikuu cha Rhodes, Afrika Kusini. Ndesanjo Macha (pichani kushoto) alikuwa anatoa hotuba ya ufunguzi wa mdahalo kuhusu kublogu katika kongamano lijulikanalo kama Digital Citizen Indaba, lililofanyika kwa siku moja kama sehemu ya kongamano mama la Highway Africa, 10-12, Septemba 2007. Kongamano hili hujadili matumizi ya ubunifu katika vyombo vya kisasa vya habari. Hii ilikuwa mara ya 11 kwa kongamano hilo.

Monday, September 10, 2007

Wameandika hivi juu yetu


Tukiwa Grahamstown, tulitumia vema fursa tuliyopata kuzungumza na Waafrika wenzetu katika midahalo,. mijadala na kongamano. Mara ya kwanza ilikuwa katika Digital Citizen Indaba, Jumapili asubuhi, ambapo mimi, Ndesanjo na mwandishi wa Kenya Daudi Were tulijadili mada ya fractured identities. Mimi nilizama katika kueleza umuhimu wa kublogu wa Kiswahili. Baadaye Mpiga Bob Sankofa alitoa mhadhara kwa nini anablogu kwa kutumia picha. Tumetoa ujumbe. Umefika. Baadhi ya waandishi waliokuwapo wameandika hivi juu yetu. Mwingine huyu hapa. Pia usikose stori hii. Kumbe hata wapiga picha hupendeza wakipigwa picha. Muone BOB SANKOFA akihojiwa na mapaparazi kama yeye. Pichani, kutoka kushoto ni Daudi Were kutoka Kenya, mimi na Ndesanjo Macha wakati wa maswali na majibu. Huyu hapa ni Mwandishi kutoka Zambia, Brenda Zulu, anatutwanga swali. Tazama na picha hii ya Nokia. Hapa Ndesanjo alikamatwa vizuri akisisitiza jambo.

Hii nayo kali

Zamani Shirika letu la Ndege (Air Tanzania Corporation), kwa sababu ya kutokuwa na huduma inayoaminika, liitaniwa na wabongo, likaitwa Any Time Cancellation (ATC). Wanigeria nao sasa wameibuka na mpya kuhusu 'TANESCO' yao. Kwa sababu ya mgawo wa umeme na matatizo yasiyoisha, mamlaka yao ya umeme iitwayo Nigerian Electric Power Authority (NEPA), imekuwa ikitaniwa na kuitwa Never Expect Power Always (NEPA).

Ili kukabiliana na tatizo la umeme, serikali imeifanyia mabadiliko ya kimfumo, kiutawala na kiuendeshaji, ikaundwa kampuni iitwayo
Power Holding Company of Nigeria (PHCN). Matatizo ya mgawo yamebaki pale pale, na sasa wanaiita Problem Has Changed Name (PHCN).

Sunday, September 09, 2007

Kutoka Grahamstown

Jamaa alinikamata vizuri na kamera yake nilipokuwa nawasilisha mada yangu. Leo Septemba 10. 2007 imekuwa siku ya michakariko. mimi, Ndesanjo na Bob Sankofa tumekuwa tunawasilisha mihadhara yetu kwa wasikilizaji waliokuwa katika Digital Citizen Indaba. Tumejumuika na waandishi wengi kutoka sehemu mbalimbali za Afrika. Hotuba ya ufunguzi wa mjadala wa leo katika Indaba imetolewa na Ndesanjo. Pata sehemu ya mhadhara wa Macha hapa. Nitawaletea taarifa nyingine baadaye. Zoopy wameweka hapa sehemu ya kilichotokea.

Saturday, September 08, 2007

Nimekutana na Ndesanjo

Tayari nimefika Grahamsatown, alasiri Jumamosi Septemba 9, 2007. Nimekutana na Ndesanjo Macha kwa mara ya kwanza, ana kwa ana. Muda wote tulikuwa tunafahamiana kupitia blogu na magazeti. Baadaye jioni tutakuwa kwenye hafla ya ufunguzi wa Digital Citizen Indaba kama nilivyoeleza hapo chini.

Friday, September 07, 2007

Naenda Bondeni

Wiki hii nitakuwa Bondeni kushiriki mkutano wa Highway Africa na wanahabari wengine kutoka pande mbali za Afrika na kwingineko duniani. Mojawapo ya majukumu yangu huko ni kuzungumzia uandishi mpya wa kijamii katika mkusanyiko ujulikanao kama Digital Citizen Indaba siku moja kabla ya mkutano wenyewe, ambako pia nitashiriki kujadili mada ya kublogu, nikiwa pia na gwiji wa kublogu, mwanablogu nambari wani wa Kiswahili, Ndesanjo Macha na wadu wengine. Msiwe mbali na blogu.

Sunday, September 02, 2007

Asante Lowassa, heko Nyamongo

HII ndiyo nukuu yangu kuu kutoka kwa Waziri Mkuu Edward Lowassa.

Makamanda wanyeshewa mvua Geita


Mvua haikuwazuia kufanya walichodhamiria. Hii ni sehemu ya umati wa waliohudhuria mkutano wa wapinzani Geita Mjini, Septemba 2).Anayehutubia ni Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe.
(Picha kwa hisani ya Joseph Senga).

Ndimara Tegambwage afungua blogu


Mwandishi mkongwe wa vitabu na magazeti; mchambuzi mahiri na mjenzi makini wa hoja kali; mmoja wa waasisi wa mageuzi ya vyama vingi nchini; mbunge mstaafu wa Muleba Kaskazini; Ndimara Tegambwage, anayeandika safu ya SITAKI (na hii hapa mpya) katika gazeti la Tanzania Daima Jumapili, ameingia katika ulimwengu wa blogu. Jina lenyewe la blogu ni dalili tosha kwamba kishindo chake kitakuwa kikubwa.

Wanablogu wengi ninaowajua ni vijana. Wazee wengi wa rika la Ndimara wamekuwa waoga wa teknolojia. Lakini Ndimara hazeeki. Hata katika dotikomu naye yumo. Na kwa wanaomfahamu, Ndimara ni kijana kuliko vijana wengi tulionao, waliozeeka kabla ya wakati wao. Msome hapa.


Mbowe, Zitto watua Mwanza


Wamo katika helikopta hii inayokaribia kutua katika uwanja wa Mirongo, Mwanza, wakiwa na viongozi wengine wa upinzani wanaoandamana nao. Umati wa wananchi, unaishuhudia inavyotua kabla ya mkutano kuanza. (Picha zote kwa hisani ya Joseph Senga)

Mresha katika Chopa ya Mbowe


Mheshimiwa Mrema ameshuka kwenye Chopa, ilipotua katika uwanja wa Mirongo, Mwanza.

Mrema naye atema tete


Mzee wa Kiraracha naye alikuwapo. Hapa anawapa shule wakazi wa Mwanza walioketi chini kumsikiliza.

People's Power


Mbowe 'akiwachochea' wananchi kutumia nguvu ya umma kuishikiza serikali adabu.
My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'