Monday, July 28, 2008

Chacha Wangwe afariki dunia


Taarifa nilizopata sasa hivi (28.07.2008 saa 3:15 usiku) kwa simu kutoka kwa Mhariri wa RAI, Deodatus Balile, Tanzania, ni kwamba mpambanaji, Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, (pichani kushoto) amefariki dunia katika ajali ya gari maeneo ya Panda Mbili akitokea Bungeni Dodoma njiani kuelekea Dar es Salaam. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amin! Kwa habari zaidi za kifo chake SOMA hapa.

Thursday, July 24, 2008

Moto wa Obama Ulaya

Katika hotuba inayosisitiza umoja na mshikamano wa kimataifa Seneta Barack Obama amesisitiza umuhimu wa kila binadamu kukiri kuwa raia wa dunia. Kama ilivyo nchini mwake, Marekani, Obama ameonyesha mvuto mkali kwa Wajerumani waliokusanyika jijini Berlin kwa wingi kumsikiliza, katika hotuba kuu inayojadili mwelekeo wa ushirikiano wa kimataifa unaolenga kuvunja kuta za migawanyiko na utengano wa binadamu katika makundi mbalimbali. Msikilize akihutubia makumi ya maelfu jijini Berlin.

Isome hotuba ya Obama katika maandishi; na baadaye isikilize katika video. Wakati Obama amejitahidi kufafanua umuhimu na maana ya ziara yake hii, wachambuzi nao hawakubaki nyuma katika kutafakari hotuba yake na athari zake katika kinyang'anyiro cha urais wa Marekani. Wasikilize: 0001. 0002. 0003. 0004. 0005. 0006. 0007. 0008.

Wazungu wa Ulaya wanawaonaje Obama na mshindani wake JohnMcCain? Pata mtazamo wao hapa. Obama na McCain nao "wapashana." Hapa msikilize Obama mwenyewe akijifagilia na kumponda McCain

Sunday, July 20, 2008

Serikali, vibaka wa MwanaHALISI


Kwanini serikali na "vibaka" wamekuwa wanavamia ofisi za gazeti la MwanaHALISI? Kuna mradi gani unaowaunganisha serikali na vibaka katika ofisi hizi?
Katika picha ni Mhariri Mtendaji wa Hali Halisi newspaper, Saed Kubenea (kushoto) akizungumzia tukio la polisi waliovamia ofisi yake kwa upekuzi hivi karibuni. Kulia ni mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Sakina Datoo, katika mazungumzo na waandishi wa habari Dar es Salaam. Picha na Tryphone Mweji wa IPP MEDIA.

Wednesday, July 16, 2008

Mpayukaji na unabii mpya

Viwango vya unabii wa ndugu yetu Mpayukaji naona vinaendelea kupanda. Msome hapa.

Tuesday, July 15, 2008

Siasa na teknolojia; tunaweza kuongopa?

Usicheze na zama hizi za teknolojia. Tazama na sikiliza wanamuziki wanavyoimba kipande cha hotuba ya Barack Obama, na kusisitiza kauli mbiu yake ya Yes We Can. Na hapa John McCain akijikanyaga kanyaga kwa kukana na kupinga kauli zake mwenyewe. Na hapa Hillary Clinton na Obama katika igizo la Tunaweza-Hatuwezi. Ndivyo wanasiasa walivyo vigeugeu wa kauli zao.

Katika video hii hapa, Obama na Clinton wanatwangana ulingoni, lakini hatimaye mshindi anapatikana. Mnamjua! Ifurahie na hii hapa ya Obama Girl.

Monday, July 14, 2008

Ole wenu CHADEMA

Mgogoro wa uongozi katika CHADEMA unaleta kumbukumbu na hisia mbaya. Lazima viongozi wajifunze kutokana migogoro iliyotangulia, na wachukue hatua sasa. Maoni yangu ya kwanza kwao, ni haya hapa.

Sunday, July 06, 2008

Tufanye nini?

Hili ndilo swali kuu ambalo Watanzania wengi wanajiuliza. Hebu tujadiliane na tuanze kulijibu hatua kwa hatua. 1.xxx

Wednesday, July 02, 2008

McCain ampiku Mbowe

Wale waliokuwa wanashangaa Chopa ya Mbowe, sasa wamepata nyongeza. Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican, John McCain, wa Marekani, ameingiza mashine ya kampeni isiyo ya kawaida. Hatulinganishi nchi wala vyama, bali mbinu na vifaa.

Tuesday, July 01, 2008

Kikwete na wenzake wamshindwa Mugabe

Mkusanyiko wa marais wa Afrika uliotarajiwa kumdhibiti Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kuhusu uchaguzi wake wenye utata umeshindwa kumdhibiti wala kumkemea. Wakati jumuiya ya kimataifa inafanya kila liwezekanalo kumwekea Mugabe vigezo kwa kuongoza nchi yake kidikteta, viongozi wetu wa Umoja wa Afrika (AU) wamemuita shujaa. Hii ni aibu kwa Bara la Afrika.
My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'