Thursday, November 18, 2010

Chadema wamkataa Kikwete hadharani

Chadema wamesisitiza hoja yao ya kukataa matokeo ya urais kwa sababu za uchakachuaji. Mdau mmoja, Bartholomew Mkinga, ameamua kufafanua uamuzi wa Chadema kumkataa rais, na kuendelea na shughuli za Bunge. Anasema:

"CHADEMA haijatamka kuwa haimtambui Kikwete kama Rais wa Tanzania, bali hawayatambui matokeo ya uchaguzi yaliyompa Kikwete mamlaka ya kuwa rais. Kwa tafsiri rahisi, ni Kikwete hana tofauti na marais wan chi nyingine wanaotumia mbinu mbalimbali kuupata urais bila ridhaa ya wananchi wanaowaongoza; amewekwa madarakani na tume ya uchaguzi, si wapiga kura.

CHADEMA haiongelei matokeo ya kura za ubunge kwa vile sheria inaruhusu kuhoji matokeo ya ubunge kwenye vyombo vya kisheria. Kwa hiyo, CHADEMA inategemea kuhoji matokeo ya kura za ubunge katika majimbo kadhaa. Kwa upande wa urais ni tofauti kwa vile sheria hairuhusu kuhoji matokeo ya urais mara tume ya uchaguzi ikishayatangaza. Kwa hiyo, jitihada pekee inayoweza kutumika ni ya kisiasa.

CHADEMA hawatahudhuria matukio yote mawili kama njia mojawapo ya kuonesha kutokuridhika na kile kilichofanywa na tume ya uchaguzi ya kuhujumu demokrasia."

Katika tukio la hivi karibuni, Alhamisi wiki hii, wabunge wa Chadema wamesusa hotuba ya Kikwete Bungeni. Mara tu alipoinuka na kuanza kuhutubia, wabunge wote, wakiongozwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, wameondoka, wakimwacha Kikwete mdomo wazi. Kikwete amelazimika kuhutubia wabunge wa CCM, CUF, TLP na NCCR-Mageuzi.

Wednesday, November 03, 2010Dk Slaa amesema kuwa matokeo ya kura za urais na ubunge yanayoendelea kutangazwana Tume ya Taifa ya Uchaguzi yamepikwa na Idara ya Usalama wa Taifa. Aliwaambia waandishi wa habari, makao makuu ya chama chake, kuwa Chadema kimefuatilia na kugundua kuwa takwimu za matokeo zinazotangazwa na Tume hazifanani na zile zilizo majimboni na kwenye kata, kutokana na idadi ya kura kutoka vituo vya kupigia kura. Alitoa mifano kadhaa, ukiwamo wa Geita ambako Chadema kilipata kura zaidi ya 22,000 za urais, lakini Tume ilitangaza kwamba kilipata kura 3,000.

Kwa sababu hiyo, Dk Slaa aliitaka Tume kusitisha mara moja utangazaji wa matokeo ya urais na kuandaa upya uchaguzi wa rais. Alimtaka pia Mkurugenzi wa Idara ya Usalama ajiuzulu kwa sababu amekipendelea chama kimoja badala ya kujali maslahi ya taifa.

Monday, November 01, 2010

Majimbo ya upinzani

Hadi sasa inasemekana upinzani umechukua majimbo haya. Matokeo yameshajulikana katika majimbo mengi. Lakini Tume haitangazi, hasa katika maeneo ambako CCM wameshindwa. Wanataka walale nazo, waingize masanduku mapya, waombe zihesabiwe upya, ili watangaze mtu wao kesho. Katika baadhi ya maeneo, vijana wameshaanza kudai matangazo ya matokeo yao kwa nguvu: Matangazo rasmi kwa majimbo yote yanaendelea kutolewa:

Wapinzani walioshinda hawa hapa

1. Halima James Mdee .... Kawe (Chadema)
2. Tundu Lissu .... Singida Mashariki (Chadema)
3. Mustapha Quorro Akonaay ... Mbulu (Chadema)
4. Israel Yohana ..... Karatu (Chadema)
5. John Mnyika ..... Ubungo (Chadema)
6. Silinde David ...... Mbozi Magharibi (Chadema)
7. Felix Mkosamali ..... Muhambwe (NCCR-Mageuzi)
8. Salvatory Naluyaga Machemuli ...Ukerewe (Chadema)
9. Agripina Z. Buyogela .... Kasulu Vijijini (NCCR-Mageuzi)
10. Ole Sambu ...... Arumeru Magharibi (Chadema)
11. Augustine Lyatonga Mrema ..... Vunjo (TLP)
12. Salum Barwani ...... Lindi (CUF)
13. Joseph Mbilinyi ....... Mbeya Mjini (Chadema)
14. Philemon Ndesamburo Kiwelu ....... Moshi Mjini (Chadema)
15. Dk Antony Mbasa ....... Biharamulo Magharibi (Chadema)
16. Machali Moses John ......Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi)
17. Joseph Selasini ...... Rombo (Chadema)
18. Hezekiah Wenje ....... Nyamagana (Chadema)
19. Peter Msigwa ....... Iringa Mjini (Chadema)
20. Freeman Mbowe ....... Hai (Chadema)
21. Vincent Nyerere ...... Musoma Mjini (Chadema)
22. Godbless Lema ....... Arusha Mjini (Chadema)
23. Zitto Kabwe ....... Kigoma Kaskazini (Chadema)
24. Hayness Samson ...... Ilemela (Chadema)
25. John Shibuda ........ Maswa Magharibi (Chadema)
26. Meshack Opulukwa ....... Meatu (Chadema)
27. Sylvester Kasulimbayi Mhoja ....... Maswa Mashariki (Chadema)
28. John Cheyo ......... Bariadi Mashariki (UDP)
29. Bungaro Said ........ Kilwa Kusini (CUF)
30. David Kafulila ....... Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi)


Mengine baadaye

Uchakachuaji wa kura waanza

Taarifa zilizopo zinasema katika vituo vingi, kura za urais anaongoza Dk Slaa, lakini wanatangaza ya udiwani na ubunge tu. Eti ya urais yanasubiri baadaye. Njama za kuchakachua, kumuongezea JK! TUnasubiri.

Habari zinasema JK na Yusuf Makamba wamekimbilia Mwanza kumnusuru Masha, Nyamagana. Pale Ilemela, Anthony Diallo, amekubali kushindwa, akasaini fomu ya matokeo. Anataka kumwaga damu?
My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'