Monday, April 02, 2012

Chadema kidedea Arumeru Mashariki



CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeshinda katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki. Kwa hiyo, Mbunge wa Arumeru Mashariki ni Joshua Nassari (pichani kulia). Kura halali 60,038: Zilizokataliwa 661. Wagombea: Mazengo Adam (AFP) 139; Charles Msuya (UDP) 18; TLP 18; Kirita Shauri Moyo 22; Hamisi Kiemi 35; Mohammed DP 77; Sumari, Sioi 26757; Nassari, Joshua 32,972. Vile vile, kimeshinda udiwani katika kata nyeti zote nchini. Nguvu ya Umma imefanya kazi. Mchakamchaka kuelekea 2015!
My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'