Sunday, November 11, 2012

Wafuasi wa Romney wamwaga chozi

Hivi ndivyo wafuasi wa Mitt Romney walivyomwaga chozi baada ya kuona matokeo ya kura yanampa ushindi Rais Barack Obama, ambaye wafuasi wake wanashangilia kwa kunyosha vidole viwili kama vya Chadema!

Saturday, October 27, 2012

UVCCM wapongezana kwa kipigo Dar



Hivi ndivyo UVCCM walivyowapokea viongozi wao wapya - kwa mabango na kichapo - katika ofisi za Makao Makuu ya Umoja huo leo.

Tujadili masuala haya

Magonjwa ya CCM na imani kwa JK au Dk. Ulimboka.

Thursday, October 11, 2012

Naibu Waziri Wa Sheria Na Katiba Akiwa Ghana

Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angela Kairuki akiteta na Naibu Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Dk. Arthur Mutambara katika kongamano la mwaka la wajasiriamali na viongozi wanaochipukia Barani Afrika, linalofanyika kwa siku tatu Accra, Ghana, kuanzia jana. (Picha na Ansbert Ngurumo)

Ngurumo Ahudhuria Mafunzo Accra Ghana


Mkurugenzi Mtendaji wa Vox Media, ambaye pia ni Naibu Mhariri Mtendaji wa Free Media, Ansbert Ngurumo, akiwa miongoni mwa washiriki wa kongamano la mwaka la wajasiriamali na viongozi wanaochipukia Barani Afrika, linalofanyika Jijini Accra, Ghana, kwa siku tatu kuanzia Jana.

Friday, September 28, 2012

Magamba Yapukutika Nyakatanga

Baadhi ya makumi ya wana CCM wameamua kuvua magamba na kujiunga na M4C mbele ya Ansbert Ngurumo aliye Muleba pamoja na John Heche kwenye M4C

Heche Aendeleza M4C Kamachumu

Leo John Heche Mwenyekiti wa CHADEMA viana taifa,akiwa Kamachumu,Muleba, kagera

Sunday, September 23, 2012

John Heche Apenya Vijiji Muleba




 Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, John Heche, akihutubia Mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nsisha, Kagoma, Wilayani Muleba, Mkoa wa Kagera.
 Wananchi
 Katibu wa CHADEMA Muleba kaskazini


John Heche na viongozi wa jimbo la Muleba kaskazini

Monday, September 17, 2012

Hotuba ya Mbowe Washington DC

Mheshimiwa Freeman Mbowe akihutubia Watanzania waishio Marekani kuhusu azima ya mabadiliko Tanzania. Anasema mabadiliko yanayotokea sasa ni mpango wa Mungu! Msikilize sasa.

Wednesday, September 05, 2012

Tuesday, September 04, 2012

Tanzia mwanana ya Daudi Mwangosi

Katika yote yaliyoandikwa kuhusu mateso na kifo cha Daudi Mwangosi (pichani) aliyeuawa na polisi kijijini Nyololo, Iringa, andiko hili linastahili enzi ya pekee, na linastahili kuwa tanzia mwanana ya Hayati Mwangosi. Requiem In Pacem!

Thursday, July 19, 2012

Nukuu ya Leo kutoka UN

“Neither peace, development nor human rights can flourish in an atmosphere of corruption.”(Amani, maendeleo au haki za binadamu haviwezi kushamiri mahali penye ufisadi) - Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

M4C yavuna mamia Chato kwa Magufuli

Mmoja wa mavuno mapya ya M4C ni Dk. Benedict Lukanima, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe. Ndiye aliyenipokea na kunionyesha mazingira katika Chuo Kikuu cha Hull, Uingereza; wakati huo akiwa katika mwaka wa pili wa Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Uchumi.

Wednesday, July 18, 2012

Nukuu ya Sugu Bungeni

"Natuma salamu kwa Kova kwamba ile filamu yake ya Dk Ulimboka, Mchungaji, na Mkenya, wananchi hawajaielewa; hivyo ni vema arudi Studio ili afanye remix!" Joseph Mbilinyi, Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema)


Sunday, July 08, 2012

Nukuu ya Leo

"Katika mapambano ya ukombozi ni lazima wengine wawe mbegu, sisi tupo tayari kufanywa mbegu.” Dk. Willibrod Slaa Julai 8, 2012: Dar es Salaam

Saturday, July 07, 2012

Libya wachagua rais mpya

Wananchi wa  Libya leo wamejitokeza kwa wingi kupiga kura kuchagua rais, katika uchaguzi huru baada ya miaka 60 ya udikteta. Habari zaidi soma hapa.

Serena ang'ara tena

Mchezaji maarufu za tenisi Serena Williams ameibuka kidedea kwa kutwaa taji mara ya tano
.

Narejea

Nimekuwa mbali na blogu hii kwa muda sasa. Nimerejea. Tarajia mwendelezo wa harakati.

Monday, April 02, 2012

Chadema kidedea Arumeru Mashariki



CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeshinda katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki. Kwa hiyo, Mbunge wa Arumeru Mashariki ni Joshua Nassari (pichani kulia). Kura halali 60,038: Zilizokataliwa 661. Wagombea: Mazengo Adam (AFP) 139; Charles Msuya (UDP) 18; TLP 18; Kirita Shauri Moyo 22; Hamisi Kiemi 35; Mohammed DP 77; Sumari, Sioi 26757; Nassari, Joshua 32,972. Vile vile, kimeshinda udiwani katika kata nyeti zote nchini. Nguvu ya Umma imefanya kazi. Mchakamchaka kuelekea 2015!

Thursday, March 29, 2012

Mexico wasaka Amani kwa Haki na Utu


Wameksiko jana waliadhimisha mwaka wa kwanza wa Harakati za kulinda Amani kwa Haki na Utu, mjini Cuernavaca. Maandamano, machozi, ngoma na ibada ni baadhi ya mapambo ya maadhimisho hayo. Dada huyu naye alikuwa kikolezo cha maadhimisho. Waweza kujisomea zaidi habari hizo kwa Kiingereza katika tovuti ya narconews. Mama huyu aliimba kwa hisia. Na kasisi huyu alisali kwa hisia pia, ingawa kusema kweli sikuwa naelewa alichosema. Lugha gongana!

Fidel Castro amuuliza Papa swali jepesi


Wote ni wazee. Wanazidiana mwaka mmoja tu. (85-84). Mmoja ni Mkomunisti. Mwingine ni Mkristo Mkatoliki. Mmoja amewahi kuwa rais wa Cuba. Mwingine sasa ni rais wa Vatican City. Baada ya Castro kufuatilia ziara ya Papa Benedict XVI kwenye runinga tangu alipotua nchini humo siku tatu zilizopita, alipopata fursa ya kukutana naye ana kwa ana, akamuuliza: "Hivi kazi ya Papa ni nini?" SOMA HAPA uone majibu ya Papa.

Monday, March 12, 2012

Oa mwanamke mzee, kufa mapema!

SI mimi ninayesema hivyo. Ni utafiti mpya. Soma hapa.

Saturday, March 10, 2012

Friday, March 09, 2012

Ajabu! Upepo mkali unasababisha golikipa 'kujifunga.' Huwezi kumlaumu. Tazama mwenyewe.

Wednesday, March 07, 2012

Unique Letter to President Kikwete


This letter was circulates in one of Tanzania's social media network, wanabidii: It is addressed to President Jakaya Kikwete (pictured) in a unique tone, and with a message that makes it eccentric. Read on:

Dear Jakaya,
Your not-so-Excellency President Kikwete,
It is my obligation to inform you, as a loyal citizen of The United Republic of Tanzania, that you are an awful president. As much as I'd love to praise your abilities to keep Tanzania in good light to most of the world, I cannot; as your cons outweigh your pros. As much as I'd praise you because you are the reason my father has the job he does at this present moment, I cannot; as you still do not fit the requirements required to be President of Tanzania. My reasons can be expressed as follows:
To start with, you do not know how to run the economy of this country. Tanzania is one of the richest countries in Africa in terms of natural resources, however, it seems that your degree in Economics did not teach you much, considering that you are unable to apply these resources to use to raise the economy of this nation. However, what you have been doing so far is giving the resources to 'investors' to raise the money for you, not realizing that these investors are not here to develop Tanzania, they are here to develop themselves! It is your job to create employment, investment opportunities and more capital for the Tanzanians themselves and I must say your failure at doing so is immense.
Even as an 18 year old, studying average high school economics, I can think of way more solutions to our economic problems compared to the ones that you are providing, which so far, are actually not even present, as you are not providing solutions to our problems. I must not get into stereotypes, lest I judge you by your background, however I must ask, who in the world informed you that the only way out of our problems is through foreign aid? Actually, I must also question who you put on your economic affairs advice team, as they are obviously not doing anything but smiling at your face and nodding to whatever you think is right for this economy.
Foreign aid is not helping Tanzania create jobs and social services because in case you have not noticed, the people do not have any incentive to push them to work for themselves, because obviously, our dear president will bring more foreigners to do it for us instead, and lend us some money so we can eat for the rest of the tax year. Mr. President, I do not know of your personal views of this country, but have you no self respect? Tanzania is now the third most aided country in the world, despite our resources. Have you no shame to beg from the Western world every other month, instead of working to run away from the exploitation of our past?
You are running straight back to what we ran away from 50 years ago under the reign of our dear Mwalimu. How do you feel once Rwanda and Kenya boast about having no budget deficit and no financial aiding from foreigners in their next parliamentary budgets, while you will smile and say Denmark is giving you an extra 10 million euros to finish up your budget? Do you seek pride in being the little beggar child that all of the rich people lend money to every now and then because they have been a 'good child' and listen to everything the rich people demand?
You are a prime example of the able bodied man on the street, begging from car to car, not knowing that he has strong limbs to work for himself! I am tired of the days where we run to the West to help us. Why? Because they exploited us, and as wealthy nations it is their obligation to help us out? No. That's how life is. One has to fend for their lives, and we are the ones who need to fend for the life of this country, with you in the lead. However, you are not in the lead at all, and I pity your lack of abilities. As an 18 year old girl, I feel like even I, and many others like me out there can run this country better than you do. And I do not criticize with no willingness to act, trust me, given the opportunity, I would run this country today. As we search for chances to serve our country today, you need to do the same. Do you serve this country, or is this country supposed to serve you?
I must say, you will never be known as the man who changed Tanzania. You will be known as the man who was too much of a coward to face the liars, the corrupt and the exploiters who ruin this country. No one will remember you when you are gone. No one will say, "What if Kikwete was here?" or "I miss the days when Kikwete was president." As you lie in your mansion somewhere in the nation, people will probably be glad you even left. Hope you're happy.
Sincerely,

Inviolata Sia Chami

source: http://webcache.googleusercontent.co...&ct=clnk&gl=us

Tuesday, March 06, 2012

Tajiri Nambari Wani Duniani


Tajiri Nambari Wani Duniani si Bill Gates tena. Ni Carlos Slim, (pichani) raia wa Mexico, mmiliki wa Kampuni ya Simu iitwayo America Movil SAB (AMXL). Kwa mujibu wa utafiti mpya uliofanywa na Bloomberg Billionaires Index, Bill Gates ni wa pili. Mmarekani mwenzake, Warren Buffett, anashika nafasi ya tatu. Endelea kujisomea.

Mfano mzuri wa ujasiriamali


Nimeipata hii kwenye mtandao wa BBC, nikadhani inaweza kusaidia kutufikirisha zaidi kuhusu ujasiriamali. Jamaa katumia magari mabovu kutengeneza mtambo wa kondomu. Jisomee mwenyewe habari yake hapa.

Thursday, February 02, 2012

Jasho letu na vipato vyetu


Picha inazungumza yenyewe. Nimeipata mahali, nikasema ngoja niiweke.

Saturday, January 21, 2012

Dk. Slaa akutana na JK


LEO jioni, Dr. Willibrod Slaa amekutana na Rais Jakaya Kikwete katika Ikulu ya Magogoni, kwa wito wa rais ili kueleza chama hicho hatua alizochukua baada ya mkutano wa na ujumbe wa Chadema mwaka jana. Maelezo zaidi baadaye.

Saturday, January 14, 2012

Regia Mtema afariki dunia

. Habari mbaya zilizoifikia blogu hii ni kwamba Mbunge wa Viti Maalumu kutoka Kilombero (Chadema), Regia Mtema, pichani, amefariki dunia leo muda mfupi uliopita, katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Ruvu. Taarifa zaidi zitafuata baadaye. Mungu amlaze pema peponi!

Goli la kizembe, na la kifundi


1. Huu ni uzembe wa golikipa. 2. Na huu hapa ni umahiri wa mfungaji - HENRY.
My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'