Tuesday, August 26, 2008

Obama awa mgombea urais


Fuatilia au jikumbushe kuhusu Mkutano Mkuu wa Chama cha Democratic, Marekani, wa kumteua rasmi Barack Obama kuwa mgombea urais. Ni mkutano wa siku nne, uliopambwa na wazunguzaji wakali wa chama hicho. Hapa nakuletea wazungumzaji wakuu wa siku.

Siku ya Kwanza
: 1. Edward Kennedy. 2. Michelle Obama.

Siku ya Pili:
1. Hillary Clinton na HAPA pia.

Siku ya Tatu
: 3. Bill Clinton - MSOME kwa kifupi - na 4. Joe Biden.

Siku ya Nne: 1. Al Gore. 2. HOTUBA ya Obama.

Na huu ni uchambuzi wa vyombo vya habari vya Marekani kuhusu hotuba yake.

Mgombea mwenza wa Obama

Huyu hapa ndiye, Joe Biden, mgombea mwenza wa Barack Obama. Mzungumzaji mzuri kama Obama. Msikilize hapa.

Saturday, August 16, 2008

Changamoto ya Kosa Kuu

Siku chache zilizopita nilijadili kwa kifupi Kosa Kuu la Jakaya Kikwete, Rostam Azizi na Edward Lowassa; bahati mbaya nikatumia mfano 'ulioteleza,' lakini ujumbe wa msingi ulifika, na kosa kuu liliainishwa, na wapo wanaolirudia sasa. Katika makala iliyofuata, nilidokeza kwamba kinachowafanya mafisadi wafurukute sasa, na hata kurudia kosa hilo, ni kwa sababu liliwasaidia kupata walichotaka mwaka 2005, na sasa wanajipanga kwa ngwe ijayo, 2010; mada ambayo iliendelezwa na Absalom Kibanda katika safu yake ya Tuendako, akisema "Tumeanza kwa Mguu Mbaya."

Baadhi ya wasomaji wameifuatilia hoja hii kwa umakini zaidi. Wengine wamejitokeza kutusahihisha, kutushauri na kutupa changamoto; na kututaka tujitakase kwa kushiriki kosa hilo kuu la wanamtandao. Hii ni changamoto halali. Swali linalokuja ni je, tuko tayari kujikosoa na kuomba radhi kwa umma? Nadhani hili nalo ni swali gumu.
My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'