Sunday, November 25, 2007

Tusiogope, Mapinduzi Yanawezekana


Nina hoja mbili. Kwanza, tuwe na rais wa kukaa mdarakani miaka mitano badala ya miaka kumi. Pili, tukubali kwamba maendeleo tunayotaka kuyafanya hayawezekani kama hatutakubali kuanza sasa kufanya mapinduzi. Wengine wana shaka, na wengine wanadhani haiwezekani. Lakini kama iliwezekana kwa Warumi, (mtazame Kaizari Julius pichani na utafakari yaliyomkuta) itashindikanaje kwa Watanzania? Na je, kushuka kwa umaarufu wa Kikwete kwaweza kuwa ishara mojawapo ya mwanzo mpya? Au ndiyo wanaanza kujifunza Afrika Kusini na Kenya, kujitambua na kugundua makosa?Tujadiliane.

Wednesday, November 07, 2007

Kuna ukweli gani katika hili?

Ujumbe huu unazunguka katika barua pepe za watu. Ulipofika kwangu nikaamua niuweke hapa tuujadili wazi wazi. Unasema hivi:

"Je tutafika? ...tuhuma zote za ufisadi zinazoikabili BoT, je unawajua walioajiriwa kusimamia uchumi wa nchi yetu na kutuletea mafanikio? Pokea taarifa ya wateule hawa. Ndani ya mtungi wa BoT walioqualify kuajiriwa kwa sifa na vigezo vinavyotambulika na BoT ni pamoja na hawa wafuatao:-

1. Pamella Lowassa,
2. Filbert Frederick Sumaye,
3. Zalia Kawawa,
4. Harieth Lumbanga,
5. Salama Ally Mwinyi,
6. Rachael Muganda,
7. Sylvia Omari Mahita,
8. Justina James Mungai,
9. Kenneth John Nchimbi,
10. Blassia Blassius William Mkapa,
11. Violeth Phillemon Luhanjo,
12. Liku Irene Katte Kamba,
13. Thomas Mongella,
14. Jabir Abdallah Kigoda etc.

Hapa nani atamwajibisha Dalali alas Balali? Je KAPUKU MWENDE(a.k.a KAYUMBA) ATAAJIRIWA KWELI HAPO? Hawa ni wale wenye uhusiano wa moja kwa moja na wazito wa nchi, wapo wengine ambao ni ndugu wa karibu au kabila moja na waheshimiwa. Ni vigumu kuamini kuwa hii ni bahati mbaya (mere coincidence). Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika."

Tuesday, November 06, 2007

Mkaribisheni Peter Nyanje

Mkaribisheni Peter Nyanje, mhariri wa habari wa gazeti la Tanzania Daima katika ulimwengu wa blogu. Ameingia na kuahidi makubwa; na anatualika "tujadili hoja nzito." Tunaamini ataitumia blogu yake kuwaletea wasomaji kile wanachokikosa katika gazeti lake, yaani kile kilicho muhimu kinachobaki na kukosa nafasi katika habari za kawaida za kila siku. Blogu yake hii hapa. Mtembeleeni.

Kikwete mfa maji?


Usimshangae Rais Jakaya Kikwete. Huu ni mkakati wake. Wakati mawaziri wametoka mikoani majuzi kulaani kauli za wapinzani kwamba ni uzushi, yeye amesema wapinzani wasipuuzwe. Na baada ya kuona wananchi wanapuuza hoja za utetezi wa CCM na kukumbatia za wakosoaji kuhusu masuala ya madini, sasa rais anataka kuunda kamati ya madini itakayowashirikisha hata wakosoaji wake hao hao. Je, anataka kuwaziba mdomo wanaoikosoa serikali? Na tayari ameahidi kuwapa hela ya kutosha na ziara nje ya nchi kwa kazi hiyo. Ni hongo? Anataka kumaliza nguvu za upinzani kiujanja ujajanja? Au ndiko kutapatapa kwa mfa maji?
My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'