Tuesday, March 12, 2013

Jihadhari na tapeli huyu anayetumia simu yangu

Kuna mtu ameibia simu yangu yenye laini mbili - Tigo (0719001001) na Airtel (0782172665) - tangu juzi, na anatumia namba hizo kutapeli pesa kwa watu ambao majina yao yamo kwenye contact list. Anawatumia watu meseji, hapigi wala hapokei simu anapopigiwa. 
Anadai kwamba mimi nina shida naomba msaada, na anapendekeza kiwango cha pesa za kutumiwa. Wapo wachache ambao wameibiwa tayari, na wengine walitaka kuthibitisha kama ni mimi, wakapiga simu hakupokea. 
Wanaojua namba zangu za simu wameniuliza kupitia simu yangu ya Voda, wakagundua ni mtego wa tapeli. Kwa taarifa hii, nawajulisha wote wanaonifahamu na wasionifahamu watakaoombwa pesa na mimi kutoka kwa yeyote, wasitoe kabisa. Anayeomba pesa hizo si mimi, ni tapeli!

Wednesday, March 06, 2013

Kibanda aumizwa kama Dk. Ulimboka

Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari, ambaye hadi Desemba 2012 alikuwa Mhariri Mtendaji wa Free Media, Absalom Kibanda, amevamiwa mbele ya lango la nyumba yake, Mbezi Beach, Dar es Salaam,  wakati anarejea kutoka kazini usiku; akapigwa; akang'olewa baadhi ya meno na kucha; akakatwa kidole na kuchomwa jicho. Kwa msaada wa watu mbalimbali, amesafirishwa kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu. Tunafuatilia maendeleo ya matibabu yake.
My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'