Tuesday, December 23, 2008

Tunawataka vigogo

Vita dhidi ya mafisadi ndo inaanza kukolea. Baada ya shinikizo la wananchi, vigogo kadhaa sasa wanaanza kuadhirika kwa kufikishwa mahakamani. Huu ni ushindi wa wananchi, si wa serikali; kwa kuwa tangu awali ilikuwa haikubali kuwa kuna ufisadi, na kwamba walioufanya wamo au walikuwa serikalini. Wachunguzi wa mambo wanajua kuwa kinachofanyika sasa ni mchezo wa kisiasa unaolenga kulegeza hisia za wananchi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2009 na uchaguzi mkuu mwaka 2010 kwa ajili ya CCM. Zaidi ya hayo, baadhi yetu tunasema, waliokamatwa hadi sasa ni DAGAA tu. Tunawataka vigogo wenyewe!

Sunday, December 21, 2008

Hata Bush kapigwa kiatu

Rais Jakaya Kikwete alirushiwa mawe akiwa ziarani Mbeya watu wakashangaa; na sasa Rais George W. Bush wa Marekani karushiwa kiatu katika mkutano na waandishi wa habari akiwa ziarani Iraq.

Wednesday, November 26, 2008

The Power Of Your Smile

SENT TO ME BY A FRIEND: This is a good story and is true, please read it all the way through until the end! (After the story, there are some very interesting facts!)

I am a mother of three (ages 14, 12, 3) and have recently completed my college degree. The last class I had to take was Sociology. The teacher was absolutely inspiring with the qualities that I wish every human being had been graced with. Her last project of the term was called, 'Smile.' The class was asked to go out and smile at three people and document their reactions. I am a very friendly person and always smile at everyone and say hello anyway.

So, I thought this would be a piece of cake, literally. Soon after we were assigned the project, my husband, youngest son, and I went out to McDonald's one crisp March morning. It was just our way of sharing special playtime with our son. We were standing in line, waiting to be served, when all of a sudden everyone around us began to back away, and then even my husband did. I did not move an inch... an overwhelming feeling of panic welled up inside of me as I turned to see why they had moved.

As I turned around I smelled a horrible 'dirty body' smell, and there standing behind me were two poor homeless men. As I looked down at the short gentleman, close to me, he was 'smiling'. His beautiful sky blue eyes were full of God's Light as he searched for acceptance. He said, 'Good day' as he counted the few coins he had been clutching. The second man fumbled with his hands as he stood behind his friend. I realized the second man was mentally challenged and the blue-eyed gentleman was his salvation.

I held my tears as I stood there with them. The young lady at the counter asked him what they wanted. He said, 'Coffee is all Miss' because that was all they could afford. (If they wanted to sit in the restaurant and warm up, they had to buy something. He just wanted to be warm). Then I really felt it - the compulsion was so great I almost reached out and embraced the little man with the blue eyes. That is when I noticed all eyes in the restaurant were set on me, judging my every action. I smiled and asked the young lady behind the counter to give me two more breakfast meals on a separate tray.

I then walked around the corner to the table that the men had chosen as a resting spot. I put the tray on the table and laid my hand on the blue-eyed gentleman's cold hand. He looked up at me, with tears in his eyes, and said, 'Thank you.' I leaned over, began to pat his hand and said, 'I did not do this for you. God is here working through me to give you hope.'

I started to cry as I walked away to join my husband and son. When I sat down my husband smiled at me and said, 'That is why God gave you to me, Honey, to give me hope..' We held hands for a moment and at that time, we knew that only because of the Grace that we had been given were we able to give. We are not church goers, but we are believers. That day showed me the pure Light of God's sweet love. I returned to college, on the last evening of class, with this story in hand. I turned in 'my project' and the instructor read it.

Then she looked up at me and said, 'Can I share this?' I slowly nodded as she got the attention of the class. She began to read and that is when I knew that we as human beings and being part of God share this need to heal people and to be healed. In my own way I had touched the people at McDonald's, my son,the instructor, and every soul that shared the classroom on the last night I spent as a college student.. I graduated with one of the biggest lessons I would ever learn: UNCONDITIONAL ACCEPTANCE.

Monday, November 17, 2008

Tusilainishwe na Tabasamu

Tabasamu gani hilo? Tumelainikaje? Soma HAPA. Mwendelezo wake huu hapa: 0002 na 0003

Wednesday, November 12, 2008

Tuesday, November 11, 2008

Obama na Bush Ikulu


Rais Mteule wa Marekani Obama ameingia katika ofisi ya rais kwa mara ya kwanza kukutana na mwenyeji wake, rais anayestaafu George W. Bush, kama sehemu ya mchakato wa makabidhiano ya madaraka yanayoendelea hadi Januari 20, 2009.

Monday, November 10, 2008

Mtobwa, Nyaulawa wafariki


WADAU wawili wakongwe wa habari nchini wametutoka. Richard Nyaulawa (pichani kushoto), Mbunge wa Mbeya Vijijini na mmiliki wa kampuni ya Business Times inayochapisha magazeti ya Majira, Business Times, Dar Leo na mengine, amefariki dunia. Kwa mujibu wa habari za Majira, Nyaulawa amefia nyumbani kwake Kawe Beach, Dar es Salaam, Jumapili 09.11.2008. Siku hiyo hiyo, mwandishi mkongwe na mmiliki wa gazeti la HEKO, Ben Mtobwa, amefariki dunia kwa ugonjwa wa moyo 09.11.2008 katika hospitali ya Tanzania Hearts Institute, Dar es Salaam. Amewahi kuandika vitabu kadhaa, kikiwamo ZAWADI YA USHINDI kinachotumika katika mitaala ya sekondari. Baadhi ya wanafunzi waliosoma vitabu vyake walipata fursa ya kumtembelea na kumuhoji zaidi katika kujifunza juu ya fikra na mtazamo wake. Mwandishi mkongwe mwenzake, Ndimara Tegambwage anasema: "Mtobwa alikuwa mwalimu nje ya darsasa." Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa ndugu na rafiki zake, marehemu anatarajiwa kuzikwa Jumanne Novemba 11. Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi! Amina!

Wednesday, November 05, 2008

Obama aibuka kidedea urais Marekani



Barack Obama ASHINDA.

Mtazame hapa akishuhudia matokeo.

John McCain akubali kushindwa.

Hotuba ya Obama, shukrani kwa ushindi.

Jisomee na kusikiliza hotuba yake.

Obama na John McCain baada ya mshindi kujulikana.

Spika wa Bunge, Nancy Pelosi, azungumzia ushindi Obama.

Umma wajadili ushindi wa Obama.

Pongezi za Condoliza Rice kwa Obama.

Safari ya Obama kuelekea Ikulu.

Rais George Bush ampongeza Obama.

Neno la Jesse Jackson.

Swali gumu juu ya ushindi wa Obama.

Wakenya na Obama.

Obama na Intaneti.

Monday, November 03, 2008

Uchaguzi Mkuu Marekani

Fuatilitia uchaguzi wa Marekani 2008 kati ya Barack Obama na John McCain.

001.Kampeni na tathmini siku ya mwisho. 00.2 Walikotoka. 002.

Sunday, November 02, 2008

Tumsamehe Rais Kikwete

Rais Jakaya Kikwete amewasamehe rasmi wezi wa EPA. SWALI LANGU: Na sisi tumsamehe yeye, yaishe?

Sunday, October 19, 2008

Wananchi wamechoka

'Fujo' za wananchi dhidi ya viongozi wao na watawala zina chanzo na maelezo. HII HAPA ni sababu mojawapo. Soma pia makala ya Maggid Mjengwa akinikosoa na kuniambia Rais hapigwi mawe. Usikose pia majibu yangu kwake, mwendelezo wa mjadala katika makala isemayo: Hatuvunji nyumba, tunabomoa mlango. Na wewe toa maoni yako.

Sunday, October 12, 2008

Mtawa na Obama


VIKONGWE wawili Wamarekani wenye miaka 106 ni miongoni mwa wapiga kura wa (Rais) Barack Obama. Wa kwanza ni Ann Nixon Cooper ambaye Obama alimtaja katika hotuba yake ya ushindi; na wa pili sista huyu (pichani kushoto) ambaye hajapiga kura tangu mwaka 1952, lakini sasa amesema amepiga kura, na amempigia Obama. SOMA HAPA.

Thursday, October 09, 2008

Obama na McCain wanatuhusu nini?

Urais wa Barack Obama au John McCain kwa Marekani unatuhusuje sisi tusio Wamarekani? SOMA HAPA ujue mambo yanayotuhusu wanayotaka kufanya.

Soma hapa uone mgombea mwenza wa McCain, Sarah Palin alivyoingizwa mjini na wasanii kwenye simu.

Wakati huo huo, kampeni zimepamba moto, na McCain amemfagilia Obama bila kutaka; akazomewa na mashabiki wake. Sikiliza hapa.

Sunday, October 05, 2008

Tunaondoaje ombwe la uongozi?

ZIPO njia nyingi. Napendekeza tuanze kwa kuwadhibiti waviziaji wa uongozi wa nchi. Pata maoni yangu hapa.

Saturday, September 27, 2008

Midahalo ya Obama na McCain


Sikiliza na fuatilia midahalo kati ya wagombea urais wa Marekani, Barack Obama na John McCain. Fanya tathimini na uchambuzi kujua nani zaidi.


1
. Mdahalo wa Kwanza: 27.09.2008.

2. Mdahalo wa Wagombea wenza (Joe Biden na Sarah Palin) 03.10.2008

3. Mdahalo wa Pili: 07.10.2008 au HAPA 4. Mdahalo wa Tatu: 15.10.2008

Wengine wameshatoa tathmini na kugawa alama B+ na B. Wewe unatoa ngapi?

Thursday, September 25, 2008

Tuwajadili Mabilionea wa Kikwete

Mabilionea wa Rais Jakaya Kikwete ni akina nani? Baadhi yao ni HAWA HAPA.

Monday, September 15, 2008

Zimbabwe kama Kenya


Mahasimu wa kisiasa nchini Zimbabwe, Rais Robert Mugabe na Kiongozi wa Upinzani, Morgan Tsvangirai, wamesaini makubaliano ya kugawana madaraka - baada ya usuluhishi uliofanywa na Rais wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki. Mugabe ataendelea kuwa rais na mkuu wa nchi, huku Tsvangirai akiwa Waziri Mkuu na msimamizi wa Baraza la Mawaziri. Hata hivyo, hotuba za viongozi hao mara baadaya kusaini makubaliano hayo, zinaonyesha waziwazi tofauti walizonazo. Msikilize Mugabe hapa; na Tsvangirai hapa.

Sunday, September 14, 2008

Njiani kuelekea nyumbani


Hapa ni Brenda Zulu, Timothy Kasolo (Zambia) na mimi, tukiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, Johannesburg, Afrika Kusini, njiani kuelekea makwetu baada ya mkutano wa Highway Africa. 13.09.2008

Sunday, September 07, 2008

Nipo Highway Africa

Wiki (6.9.2008 - 13.9.2009) hii nitakuwa Afrika Kusini, katika Chuo Kikuu cha Rhodes, kuhudhuria kongamano la kila mwaka la Highway Africa linalojadili matumizi ya teknolojia za kisasa katika kukuza mawasiliano na kuboresha maisha. Mada kuu ya mwaka huu ni Uandishi wa Kiraia: Uandishi kwa Manufaa ya Raia. Wapo Watanzania kadhaa nimekutana nao hapa, wakiwamo Mhariri Mtendaji wa Mwananchi, Theophil Makunga; Mtangazaji wa DTV, Dina Chahali; Mpiga picha na mwanablogu, Philemon Msangi (Bob Sankofa); Mwandishi anayeibukia, Furaha Thonya; Mhariri wa Mtanzania Jumapili, Eric Anthony na Ofisa Uhusiano wa CRDB, David Mbulumi. Habari zaidi za Highway Africa zinapatikana hapa. Sikiliza na matangazo mafupi ya redio kuhusu dhana ya mkutano.

Monday, September 01, 2008

Marafiki walimuonya Kikwete

Alionywa akapuuza. SOMA onyo lao hapa. Wenzake sasa wanamuhoji: Ni kazi ya serikali kubatiza au kusilimisha Watanzania?

Tuesday, August 26, 2008

Obama awa mgombea urais


Fuatilia au jikumbushe kuhusu Mkutano Mkuu wa Chama cha Democratic, Marekani, wa kumteua rasmi Barack Obama kuwa mgombea urais. Ni mkutano wa siku nne, uliopambwa na wazunguzaji wakali wa chama hicho. Hapa nakuletea wazungumzaji wakuu wa siku.

Siku ya Kwanza
: 1. Edward Kennedy. 2. Michelle Obama.

Siku ya Pili:
1. Hillary Clinton na HAPA pia.

Siku ya Tatu
: 3. Bill Clinton - MSOME kwa kifupi - na 4. Joe Biden.

Siku ya Nne: 1. Al Gore. 2. HOTUBA ya Obama.

Na huu ni uchambuzi wa vyombo vya habari vya Marekani kuhusu hotuba yake.

Mgombea mwenza wa Obama

Huyu hapa ndiye, Joe Biden, mgombea mwenza wa Barack Obama. Mzungumzaji mzuri kama Obama. Msikilize hapa.

Saturday, August 16, 2008

Changamoto ya Kosa Kuu

Siku chache zilizopita nilijadili kwa kifupi Kosa Kuu la Jakaya Kikwete, Rostam Azizi na Edward Lowassa; bahati mbaya nikatumia mfano 'ulioteleza,' lakini ujumbe wa msingi ulifika, na kosa kuu liliainishwa, na wapo wanaolirudia sasa. Katika makala iliyofuata, nilidokeza kwamba kinachowafanya mafisadi wafurukute sasa, na hata kurudia kosa hilo, ni kwa sababu liliwasaidia kupata walichotaka mwaka 2005, na sasa wanajipanga kwa ngwe ijayo, 2010; mada ambayo iliendelezwa na Absalom Kibanda katika safu yake ya Tuendako, akisema "Tumeanza kwa Mguu Mbaya."

Baadhi ya wasomaji wameifuatilia hoja hii kwa umakini zaidi. Wengine wamejitokeza kutusahihisha, kutushauri na kutupa changamoto; na kututaka tujitakase kwa kushiriki kosa hilo kuu la wanamtandao. Hii ni changamoto halali. Swali linalokuja ni je, tuko tayari kujikosoa na kuomba radhi kwa umma? Nadhani hili nalo ni swali gumu.

Monday, July 28, 2008

Chacha Wangwe afariki dunia


Taarifa nilizopata sasa hivi (28.07.2008 saa 3:15 usiku) kwa simu kutoka kwa Mhariri wa RAI, Deodatus Balile, Tanzania, ni kwamba mpambanaji, Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, (pichani kushoto) amefariki dunia katika ajali ya gari maeneo ya Panda Mbili akitokea Bungeni Dodoma njiani kuelekea Dar es Salaam. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amin! Kwa habari zaidi za kifo chake SOMA hapa.

Thursday, July 24, 2008

Moto wa Obama Ulaya

Katika hotuba inayosisitiza umoja na mshikamano wa kimataifa Seneta Barack Obama amesisitiza umuhimu wa kila binadamu kukiri kuwa raia wa dunia. Kama ilivyo nchini mwake, Marekani, Obama ameonyesha mvuto mkali kwa Wajerumani waliokusanyika jijini Berlin kwa wingi kumsikiliza, katika hotuba kuu inayojadili mwelekeo wa ushirikiano wa kimataifa unaolenga kuvunja kuta za migawanyiko na utengano wa binadamu katika makundi mbalimbali. Msikilize akihutubia makumi ya maelfu jijini Berlin.

Isome hotuba ya Obama katika maandishi; na baadaye isikilize katika video. Wakati Obama amejitahidi kufafanua umuhimu na maana ya ziara yake hii, wachambuzi nao hawakubaki nyuma katika kutafakari hotuba yake na athari zake katika kinyang'anyiro cha urais wa Marekani. Wasikilize: 0001. 0002. 0003. 0004. 0005. 0006. 0007. 0008.

Wazungu wa Ulaya wanawaonaje Obama na mshindani wake JohnMcCain? Pata mtazamo wao hapa. Obama na McCain nao "wapashana." Hapa msikilize Obama mwenyewe akijifagilia na kumponda McCain

Sunday, July 20, 2008

Serikali, vibaka wa MwanaHALISI


Kwanini serikali na "vibaka" wamekuwa wanavamia ofisi za gazeti la MwanaHALISI? Kuna mradi gani unaowaunganisha serikali na vibaka katika ofisi hizi?
Katika picha ni Mhariri Mtendaji wa Hali Halisi newspaper, Saed Kubenea (kushoto) akizungumzia tukio la polisi waliovamia ofisi yake kwa upekuzi hivi karibuni. Kulia ni mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Sakina Datoo, katika mazungumzo na waandishi wa habari Dar es Salaam. Picha na Tryphone Mweji wa IPP MEDIA.

Wednesday, July 16, 2008

Mpayukaji na unabii mpya

Viwango vya unabii wa ndugu yetu Mpayukaji naona vinaendelea kupanda. Msome hapa.

Tuesday, July 15, 2008

Siasa na teknolojia; tunaweza kuongopa?

Usicheze na zama hizi za teknolojia. Tazama na sikiliza wanamuziki wanavyoimba kipande cha hotuba ya Barack Obama, na kusisitiza kauli mbiu yake ya Yes We Can. Na hapa John McCain akijikanyaga kanyaga kwa kukana na kupinga kauli zake mwenyewe. Na hapa Hillary Clinton na Obama katika igizo la Tunaweza-Hatuwezi. Ndivyo wanasiasa walivyo vigeugeu wa kauli zao.

Katika video hii hapa, Obama na Clinton wanatwangana ulingoni, lakini hatimaye mshindi anapatikana. Mnamjua! Ifurahie na hii hapa ya Obama Girl.

Monday, July 14, 2008

Ole wenu CHADEMA

Mgogoro wa uongozi katika CHADEMA unaleta kumbukumbu na hisia mbaya. Lazima viongozi wajifunze kutokana migogoro iliyotangulia, na wachukue hatua sasa. Maoni yangu ya kwanza kwao, ni haya hapa.

Sunday, July 06, 2008

Tufanye nini?

Hili ndilo swali kuu ambalo Watanzania wengi wanajiuliza. Hebu tujadiliane na tuanze kulijibu hatua kwa hatua. 1.xxx

Wednesday, July 02, 2008

McCain ampiku Mbowe

Wale waliokuwa wanashangaa Chopa ya Mbowe, sasa wamepata nyongeza. Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican, John McCain, wa Marekani, ameingiza mashine ya kampeni isiyo ya kawaida. Hatulinganishi nchi wala vyama, bali mbinu na vifaa.

Tuesday, July 01, 2008

Kikwete na wenzake wamshindwa Mugabe

Mkusanyiko wa marais wa Afrika uliotarajiwa kumdhibiti Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kuhusu uchaguzi wake wenye utata umeshindwa kumdhibiti wala kumkemea. Wakati jumuiya ya kimataifa inafanya kila liwezekanalo kumwekea Mugabe vigezo kwa kuongoza nchi yake kidikteta, viongozi wetu wa Umoja wa Afrika (AU) wamemuita shujaa. Hii ni aibu kwa Bara la Afrika.

Sunday, June 29, 2008

Wanalinda skendo zao

Wabunge hawa ni hatari kwa taifa, lakini wanaakisi tu msimamo halisi wa wakubwa wao waliowatuma.

Friday, June 27, 2008

Happy Birthday Nelson Mandela!


Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, amesherehekea miaka 90 ya kuzaliwa, na miaka 10 ya ndoa yake na mkewe, Grace Machel. Bonyeza hapa umsikilize Graca akisimulia maisha yake ya kifamilia na Mandela; akizungumzia jambo moja ambao Mandela anasikitikia maishani mwake, na zawadi kuu ambayo yeye (Grace) amempatia Mandela katika miaka 10 ya ndoa yao. Lakini pia, Mandela anatoa rai kwa matajiri wa Afrika Kusini kutumia sehemu ya utajiri wao kusaidia maskini katika nchi hiyo.

Monday, June 23, 2008

Wabongo kwa ubunifu!

Sijui aliyeanzisha hii. Imenifikia, nikasema ngoja niwawekee wasomaji wa blogu hii. Isome mwenyewe hapa chini uone ubunifu wa Wabongo:


* Benjamin Mkapa Institute of Political Entrepreneurship and Openness

* David Balali Schoolof Central Banking and Foreign Debt Management

* AndrewChenge College of Applied Contractual Law

* AliHassan Mwinyi University of Inflation Control

* Karamagi Institute of Mining Licensing and Administration of Mining Contracts

* Zakia Meghji college of Tourism and Protection of Public Funds and Natural Resources

* Ditopile Mzuzuri School of Conveyance and Welfare of Public Drivers

* Mwalimu Nyerere University College of Privatization

* Mkono Institute of Legal Fraud Prevention

* Lowassa School of Prevention of Fake Companies

Fomu za Kujiunga zinapatikana Bank M. Nyote Mnakaribishwa.

Sunday, June 22, 2008

Raila "aongoza" watawala Afrika

Tatizo la Afrika ni kukosa viongozi wenye mitazamo ya kisasa. Waliopo sasa wamefungwa kwenye minyororo ya "ukale" wanaoendelea kuung'ang'ania. Lakini waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, anawataka watawala wa Afrika wachukue visu, wakate minyororo hii. Msikilize katika video hii. Amekuwa wa kwanza kumkaripia Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, na anataka viongozi wa Afrika waamke na kumkabili Mugabe, ili kudhibiti ukatili anaouendeleza dhidi ya watu wake.

Usafi wa Lowassa, uchafu wa CCM


CCM imesafisha Lowassa. Je, yenyewe imejisafisha? Tujadili.

Sunday, June 15, 2008

Wachache wameshinda

Mwaka mmoja uliopita umedhihirisha ushindi wa wachache dhidi ya wengi. Hoja yangu hii hapa.

Swali refu kuliko yote?

Swali hili limeulizwa Marekani, lakini hata Bongo wapo watu wanaouliza maswali mabaya kama hili hapa, linalodhaniwa kuwa swali refu kiliko yote.

Saturday, June 14, 2008

Dinner with Mugabe


Itazame video inayomjadili Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe katika uchambuzi mfupi wa kitabu DINNER WITH MUGABE cha Heidi Holland.

Wednesday, June 11, 2008

Unabii wa Mpayukaji

Mpayukaji sasa amekuwa nabii. Na anahoji. "Maiti itazikwa au la?"

Monday, June 09, 2008

Mtanzania afariki Italia


Raia mmoja wa Tanzania, Omar Jaffar Ngwaya (pichani), amefariki dunia leo Jumatatu Juni 09, 2008, nchini Italia kwa ajali ya gari. Kwa mujibu wa Katibu wa Jumuiya ya Watanzania waishio nchini Italia, Kaguta NM, mipango ya mazishi ya marehemu Ngwaya inafanyika kwa kushirikiana na Balozi wetu nchini Italia. Taarifa za nyongeza zinapatikana katika tovuti hiyo hapo juu. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi! Amina!

Sunday, June 08, 2008

Kikwete anaweza kuwa mwalimu

Rais Mstaafu Benjamin Mkapa amekuwa mwalimu wa Rais Jakaya Kikwete; naye anaweza kuwafundisha wengine. Katika hili? Soma hapa.

Saturday, June 07, 2008

Clinton ampigia debe Obama


Seneta Hillary Clinton (pichani kushoto) amekubali rasmi kushindwa, amehitimisha kampeni zake na kumuunga mkono mshindi, Seneta Barack Obama, katika kinyang'anyiro cha urais wa Marekani mwaka huu kupitia chama ha Democratic. Sikiliza sehemu ya hotuba ya Hillary ya kumkubali Obama. Hotuba nzima ya Clinton hii hapa. Barack atachuana na Seneta John McCain katika uchaguzi mkuu Novemba 2008. Kundi la wagombea waliopambana na Obama katika chama chao, ambao amewashinda, ni hawa hapa.

Hii ndiyo pensheni ya Mkapa?

Rais Mstaafu Benjamin Mkapa amenukuliwa akisema kuwa yeye anaishi kwa pensheni kama alivyo Mzee Ali Hassan Mwinyi; kwamba hana utajiri wowote, na kwamba wanaomhusisha na biashara akiwa Ikulu na ufisadi mwingine unaozungumzwa wanamwonea kwa sababu eti alikataa kuwapendelea alipokuwa rais. Lakini Mzee Mkapa hajakanusha ujasiriamali wake wa Ikulu unaowakera wananchi. Baadhi ya yanayosemwa juu ya Mkapa, ambayo hajayakanusha kabisa, ni haya hapa. Je, hii ndiyo pensheni anayozungumzia?

Wednesday, June 04, 2008

Barack Obama: This is Our Moment


Msikilize Barack Obama hapa au hapa akihutubia mashabiki wake siku ya mwisho ya kampeni za awali, siku ambapo aliibuka mshindi na mgombea urais wa chama cha Democratic dhidi ya Hillary Rodham Clinton. Obama anasema huu ndio wakati wa Wamarekani kuleta mabadiliko wanayokusudia. Msikie Obama hapa katika mojawapo ya mahojiano aliyofanya kabla ya kukamilisha ushindi wake.

Tuesday, June 03, 2008

Sometimes size matters


Nimepokea picha hii kutoka kwa rafiki yangu, nikadhani inawafaa pia wasomaji wa blogu hii. Inafikirisha na kuburudisha.

Sunday, June 01, 2008

Friday, May 30, 2008

Muuaji wa Ballali anajulikana

Licha ya utata wa kifo cha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Daudi Ballali, vyanzo vya kuaminika vimemtaja mtu aliyetajwa na Ballali kwamba ndiye alimlisha sumu.

Sunday, April 20, 2008

Tuwanyonge viongozi wa umma

Baada ya kukithiri kwa ufisadi serikalini, wananchi wengi wamekuwa wanahoji: "Tufanye nini?" Nadhani huu ni wakati mwafaka, tuanze kujadili majibu ya swali hili. Pendekezo langu la kwanza ni hili hapa. Linaendelezwa hapa.

Friday, April 18, 2008

Obama apanda, Clinton ashuka


Utafiti mpya wa Yahoo! News Unaonyesha kuwa Barrack Obama anapanda, Hillary Clinton anashuka chati. Wote wanawania kupitishwa na chama cha Democratic kugombea urais Marekani, kupambana na mgombea wa Republican, John MacCain.

Spichi 'Tamu' ya Raila Odinga


Nimeisoma hotuba ya Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, baada ya kula kiapo. Ni kauli nzito yenye ujumbe murua kwa Wakenya. Na inamtia katika wakati mgumu iwapo hatatimiza alichoahidi. Nikiitazama kwa kina, ni kama vile ndiyo alikuwa amejiandaa kutoa siku ya kuapishwa kuwa rais, lakini ameibadili kidogo ikawa ya waziri mkuu. Nimeilinganisha na hotuba ya Rais Mwai Kibaki ya siku hiyo hiyo, katika tukio hilo hilo. Tofauti iko wazi. Kila la heri Wakenya! Pichani juu ni vigogo wa Kenya: (Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka, Rais Mwai Kibaki, Waziri Mkuu Raila Odinga na Naibu Waziri Mkuu, Musalia Mudavadi).

Thursday, April 17, 2008

Intelligence Officer In Media Attack Scam In Tanzania

Habari hii imenifikia katika mzunguko wa barua wa pepe. Nimeona vema niianike hapa kwa faida ya wasomaji wa blogu hii. Soma mwenyewe.

By Derrick Msowoya
Back From Dar es Salaam, Tanzania

An officer with the Tanzania Intelligence Service (TIS) in Dar es Salaam is being held in connection with the assault on editors at a weekly tabloid Mwanahalisi on 5th January this year but the police would not reveal his real identity.

Fifteen days of independent investigations in the port city of Dar es Salaam have confirmed Ferdinand Mwenda (alias Ferdinand Msepa alias Fredy), recently joined to a list of six alleged conspirators and attackers on editors at Mwanahalisi weekly tabloid, is a TIS employee.

The police, in a case that comes up for yet another mention today (Monday 14th April 2008), have identified him as a “businessman in Dar es Salaam.” But authoritative sources within the police force have it that the young man in his thirties is a middle cadre officer with TIS.

On 5th January this year, at around 08.30 East African time, three young men stormed the offices of Mwanahalisi newspaper. At work were the publisher of the paper, Mr. Saidi Kubenea and a prominent journalist, Mr. Ndimara Tegambwage who has been providing consulting services to a two-year-old newspaper for at least seven months now.

The TIS officer, first arrested on second day after the incident and released almost immediately, only to be re-arrested weeks later, is an alleged architect of the assault in which Mr. Tegambwage sustained a deep cut by a machete on the nape well close to his right ear while Mr. Kubenea had his eyes spilled with unidentified chemical stuff which inflamed them and immediately impaired his sight.


Police, suspects vs TIS

The arrest of a TIS-officer has been a real issue within the police force. While authority at TIS would not wish to have the man’s identity revealed, other suspects are said to have been complaining about their mentor remaining free as they stayed behind bars at a Dar es Salaam remand prison.

Fear to reveal the identity of the alleged architect of the assault stems from Tanzania President Jakaya Kikwete’s visit to victims at the Muhimbili National Hospital in the port city within hours of the attack. The biggest question intelligence officers have been asking themselves is, “How will the president feel if he knows the men he visited at the hospital were victims of the dirty work of one of his men?” TIS is a coercive institution enjoying big budgets for secretive operations under the president. It has often been accused of misinformation, deliberate distortion, and torture and excessive, unaccounted for expenditures – funds most of it sunk into personal projects of luxurious nature.

And, it is yet to be known, who sent the TIS officer to attack a media outlet and journalists and how much was promised and, or received in advance for the execution of the task.

Unconfirmed reports have it that the planner of the attack was given cash money Tanzania shillings four (4) million as advance for seducing and recruiting would-be perpetrators to whom he introduced himself merely as Fredy – a businessman.

Paramour coveat

Reports have it that “Fredy” told his recruits that he was working at Azania, a food production firm in Dar es Salaam and that he wanted them to help him “do away with Mr. Kubenea” who he alleged was a paramour to his wife. While police investigations have found there was one Fredy at Azania and took his statement, they have remained convinced it was not the one the driver of suspects identified, and therefore did not call for an identification parade. They insisted Fredy in their hands be produced in court which they did almost in defiance of TIS and at least over two months since the arrest of others.

Informants have told this investigator in Dar es Salaam that there were serious efforts to have bail for all suspects so that Fredy could meet “his men” and plan how to argue their case, their earlier statements at police stations notwithstanding. This is meant, so to speak, to clear TIS of the scam by completely dissociating Fredy with TIS and possibly

clear the president of grave embarrassment. This however depends on whether the police and intelligence authorities have clinched an agreement. As of now all the alleged persons have been granted bail.

University student

It is understood that Fredy and his wife have since vacated the structure at which they were putting-up, at Tegeta, off Bagamoyo Road and are now staying with in-laws at Temeke. Further reports say the man has worked as an official of TIS in Temeke administrative district before his transfer to Kinonduni district, all in Dar es Salaam. His wife is said to be a nurse at a TIS dispensary at Kijitunyama in the city.

Other reports have it that the alleged architect of attack on an upcoming weekly is a registered student at the sociology department of the University of Dar es Salaam. However, it has not been possible to establish complicity of three other men whose names are frequently mentioned in interviews. These are Maneno, David and Mwamba whose other names and identity have not been established and the police remain silent on the suspects.

All said and done, and the police having established that there was no “love affair” involved in the attack on the media outlet, one question remains unanswered: Who must have paid Fredy for the assault?

Most observers in Dar es Salaam find the attack to be politically motivated. Mwanahalisi has, in the past 10 months, been known for its fraternity with truth and openness. It has been very hard on corruption, mismanagement and bad governance. It has openly named those caught in the web and has doggedly refused to back down. While it has not been the initiator of many down-to-earth expose, it has dug such stories beyond the ordinary, to the surprise of almost everyone and drugged them to the dead end.

That has earned the paper cumulative unfriendliness and bitter resentment, mostly from politicians whose positions and fame have been subjected to exposure and public scrutiny; and thereby eroded them irreparably. Sources suggest that that group could be central to enmity and consequent mentoring of attacks on media and its personnel.

Caught in “crossfire”

One source in Dar es Salaam wanted me to believe that Mr. Tegambwage was “probably not the target as he does not own the paper but goes there on an on-and-off-basis as consultant as he does with other media outlets.” But he quickly added, “That man is gifted; his style of writing is indeed compelling; his brilliant arguments send out messages that percolates both the bones and brains. Some people may not wish to see him plant ‘seeds of defiance’ as he has contact with many media houses.”

Mr. Tegambwage of Centre for Democratic and Strategic Management (IDEA) is also media consultant at a number of media outlets in the country and member of International Press Institute (IPI), a global forum of executive editors.

Distant sources suggest that the attack on Mwanahalisi was planned in a “kind of network” that went beyond the city of Dar es Salaam. Intimidatory statements made public by Mr. Kubenea at a press conference in Dar es Salaam, according to press reports, have been made by persons from all over the country, possibly orchestrated to make life difficult for the publisher of Mwanahalisi and his staff.

A good number of “big” politicians have so far been linked to the attack. Journalists in the port city say it is too early to make public names of those mentioned behind the curtain until the case starts and lawyers dig deep into statements made by Fredy and other suspects. But sources say Fredy hails from the same area as that of one politician’s wife; and were recruited at a meeting held at a bar owned by brother in law of the politician at a suburban bar in Dar es Salaam.

Unavoidable embarrassment

The recruitment of a TIS officer into a scum of this nature has a lot to tell on how the secret services of the organ under the president can be misused. And lives of the two victims of attack, and any other vocal journalists, remain in peril.

However, it requires pressure – both internal and external – to expose the role of TIS in the attack of a media outlet. However, the embarrassment of the president remains unavoidable. Proceedings in court can now provide the best forum at which exposure could be done without stint. Will the police be bold enough to identify the TIS official? What about the political big gun that recruited him: Will he let his agent be exposed, and at his detriment?

Monday, April 07, 2008

Adui wa Kikwete si Karume


Kama Rais Jakaya Kikwete anataka kumaliza mpasuko wa kisiasa Zanzibar, huku Rais Amani Karume anakataa, na Kikwete anakubali kugomewa kama ilivyotokea Butiama majuzi; ni nani adui wake katika hili?

Tuesday, April 01, 2008

Mugabe kama Kibaki?


UCHAGUZI Mkuu wa Zimbabwe unaelekea kwenye mkondo ule ule wa Kenya. Tume ya Uchaguzi inatoa matangazo kwa jinsi inayotia wasiwasi. Lakini dalili zinaonyesha upinzani umechukua viti vingi zaidi au umeshinda. Baadhi ya taarifa zinasema hadi sasa, upinzani umepata viti vingi zaidi (74); chama tawala ZANU-PF cha Rais Robert Mugabe kina viti 64. Mawaziri watatu wa Rais Mugabe wameangushwa. Kura za urais bado ni siri ya tume, lakini upepo unaonyesha mambo ni magumu kwa Mugabe, na tetesi ni kwamba tume inajaribu kumfanyie kile ambacho ile ya Kenya ilimfanyia Mwai Kibaki, ikamtangaza mshindi akiwa na kura chache zenye utata. Taarifa nyingine zinasema tayari Mugabe ameshajulishwa kwamba ameshindwa, na watu wake wanajadiliana namna ya kukabidhi madaraka kwa mshindi. Maana tayari upinzani umeshaanza majadiliano na majeshi ya Zimbabwe. Tusubiri!

Monday, March 31, 2008

Nyerere ataka kijiji, Kikwete mji




Nyerere hakutaka Butiama iwe makao makuu

Na Beldina Nyakeke, Musoma

CHIFU wa Kabila la Wazanaki, Japhet Wanzagi amesema azma ya Rais Jakaya Kikwete kukifanya kijiji cha Butiama kuwa makao makuu ya Wilaya ya Musoma Vijijini, inapingana na mpango wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Wanzagi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Ukoo wa Burito Nyerere, amesema mpango wa Mwalimu Nyerere ulikuwa ni kuifanya Butiama kuwa kijiji cha historia, kinyume na azma hiyo ya Rais Kikwete.

Chifu huyo alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu kauli ya Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho kijijini Butiama hivi karibuni.

Wanzagi alisema kimsingi hapingani na azma ya Rais Kikwete ya kutaka kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kufanya mambo mbalimbali, ikiwamo kukifanya kijiji cha Butiama kuwa makao makuu ya wilaya, lakini akasisitiza kuwa anao ushahidi ingawa si wa maandishi ambao kabla ya kifo chake, Mwalimu Nyerere aliwahi kumweleza nia na madhumuni ya kukifanya kijiji hicho kuwa cha kihistoria.

Alisema katika nia hiyo, Mwalimu Nyerere alipendekeza kijiji cha Kiabakari kilicho jirani na Butiama ndio pawe makao makuu ya wilaya.

Wanzagi alisema endapo serikali itaamua kukifanya kijiji hicho kuwa makao makuu ya wilaya, upo uwezekano wa kuchanganya mila na desturi za makabila mbalimbali kijijini hapo kutokana na muingiliano wa watu watakaohamia katika mji huo hali ambayo Mwalimu Nyerere hakupenda iwepo.

"Ninao ushahidi japo si wa maandishi. Na sijui hata kama Mama (Mama Maria) anajua kuwa mzee hakupeda kijiji cha Butiama kuwa mji. Maana aliniambia kuwa Butiama itakapokuwa mji, basi kutakuwepo na muingiliano wa watu wa makabila mbalimbali na kupoteza uasilia wa kijiji chetu ambapo alitolea mfano jiji la Dar es Salaam, ambalo kutokana na muingiliano wa watu, wenyeji wa pale, yaani wazaramo, wamehama na kusogea nje kabisa ya jiji," alisema.

Katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa NEC, Rais Kikwete alisema ili kumuenzi Mwalimu Nyerere, serikali itakapofikia uamuzi wa kuigawa wilaya ya Musoma Vijijini, Butiama lazima kiwe makao makuu ya wlilaya na kuungwa mkono na mkutano huo na kuiagiza serrikali kufanya haraka kutekeleza pendekezo hilo.

Katika hatua nyingine, Chifu Wanzagi, aliitaka serikali kuwawezesha wakulima kwa kuwapa mahitaji muhimu ikiwa ni pamoja na pembejeo ili kuboresha kilimo.

Habari hii nimeichukua kutoka Tovuti ya Mwananchi kwa sababu za kihistoria. Nimeona ni vema iwekwe mahali ambapo hata tukiitaka kufanyia marejeo tutaipata, maana tovuti ya Mwananchi haitunzi habari zilizopita. - Mhariri.

Saturday, March 29, 2008

Mwinyi amtosa Kikwete?


HABARI za uhakika zinasema kuwa baadhi ya marais na mawaziri wakuu wastaafu wa Tanzania wamegoma kwenda Butiama kushiriki vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM. Siku chache zilizopita, baadhi yao, chini ya Mzee Ali Hassan Mwinyi, walikuwa na kikao cha dharura kujadili namna ya kuinusuru CCM kutoka kwa mafisadi. Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye hawakualikwa. Wajumbe wa kikao cha Mwinyi waliazimia kutumia kikao cha Butiama kumlazimisha Rais Jakaya Kikwete achukue hatua mbili muhimu.

Kwanza, atumie mamlaka aliyonayo kuhakikisha vikao hivyo vinawavua uanachama wale wote waliotuhumiwa katika kashfa za EPA na Richmond. Pili, walitaka atumie nguvu hiyo hiyo, kumuondolea kinga Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, ili afikishwe mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili, na aweze kutoa ushahidi katika kesi ya Balozi Costa Mahalu ambaye amemtaja kama shahidi mkuu.

Ushauri walioupata kwa Mzee Joseph Sinde Warioba ni kwamba ikibidi, Mkapa aondolewe kinga kwa muda tu kwa ajili ya kesi ya Mahalu, halafu arejeshewe.

Katika kikao hicho, Mzee Mwinyi aliwashauri wenzake kwamba iwapo Kikwete atakataa kuchukua hatua hizo, itokee vurumai kubwa, hata kama itawalazimu kuivunja CCM na kuwa CCM A na CCM B. Wazo la CCM kuvunjika halikumpendeza Rais Mstaafu wa Zanzibar, Salmin Amour; kwa maelezo kuwa CCM ikivunjika itakuwa faida ya wapinzani, hasa Zanzibar.

Kwa hiyo, walikubaliana kuwa badala ya kuvunja chama, kama Kikwete hakubali ushauri wao, wao watagoma kushiriki kikao hicho. Alipokataa, kama walivyotarajia, wakaamua kutokushiriki.

Hata baada ya kuamua kutokwenda Butiama, hawakumtaarifu mwenyekiti wao (Kikwete). Alitaarifiwa na watu wa protokol walipokuwa wanaandaa usafiri wa wastaafu hao, huku kila mmoja akitoa udhuru wake papo hapo.

Baadhi yao, wakiwamo Mwinyi, Salim Ahmed Salim, Mkapa na Sumaye, wanasemekana kwenda nje ya nchi katika kipindi walichohitajika kwenda Butiama.

Sababu mojawapo ya Kikwete kukataa kuwachukulia hatua mafisadi wa EPA na Rihmond inasemekana ni hatua yake ya kuwalinda (au kuwaogopa) rafiki zake Edward Lowassa na Rostam Azizi ambao ni watuhumiwa wakuu wa Richmond. Na inasemekana sasa Kikwete amelazimika kuanza mkakati mpya wa kumbeba Lowassa, jambo ambalo limezua 'uhasama' kati yake (JK) na Spika wa Bunge, Samuel Sitta.

Kumeguka kwa wastaafu, hasa Mzee Mwinyi, kutoka kambi ya Kikwete, si habari ndogo. Inafikirisha na kuzua maswali magumu juu ya hatima ya chama na uongozi mzima wa Kikwete. Hadi habari hii inaandikwa, wastaafu walioonekana Butiama wakati kikao cha Kamati Kuu kinaendelea ni Rashid Kawawa, John Malecela na Gharib Bilal. Walio Butiama tuletee habari kuhusu Joseph Sinde Warioba na Cleopa Msuya.

Monday, March 17, 2008

Bado Sisi

Wakenya wamepiga hatua ambayo lazima tuionee wivu. Huko nyuma niliwahi kuandika kwamba kama tunatakakufanya mageuzi tujifunze Kenya. Lakini tunahitaji 'injini ya mageuzi'. Kenya walikuwa na injini yao, Raila Odinga. Sisi tunaye mtu wa aina hiyo? Ni nani? Ndiyo! Tunahitaji 'Mbegu ya Haradali'...

Friday, February 29, 2008

Mageuzi ya Kenya

Hatimaye mahasimu wa kisiasa nchini Kenya, Mwai Kibaki na Raila Odinga, wametiliana saini kuanzisha mchakato mpya wa mageuzi ya kisiasa nchini Kenya. Sasa (hata bila kusubiri hatua zijazo) tunaweza kuwaita Rais Kibaki na Waziri Mkuu Odinga . Wameandika historia. Dunia imeshuhudia. Je, Mkataba huu utadumu? Huko nyuma, Kibaki aliwahi kumsaliti Odinga. Je, sasa wanaaminiana, au wanategeana? Je, Afrika imejifunza lolote kutoka Kenya? Tujadili.

Friday, February 08, 2008

Lowassa nje, Pinda ndani: kashfa zinaendelea

Ripoti ya Dk. Mwakyembe kuhusu kashfa ya Richmond dhidi ya Waziri Mkuu Edward Lowassa na mshirika wake, Rostam Azizi, imezaa matunda. Tayari Lowassa amejiuzulu. Mimi nimempongeza Lowassa kwa kutusaidia kuvunja Baraza la Mawaziri. Mizengo Pinda ameteuliwa na kuthibitishwa kuwa Waziri Mkuu. Kinachoshangaza watu sasa ni kwamba Kikwete bado anamuonea huruma na kumtetea waziwazi Lowasa. Kuna nini? Au ina maana rais anawajua wahusika halisi wa kashfa hii? Je, kujiuzulu kwa Lowassa ndiyo mwisho wa hoja ya ufisadi wa serikali na CCM? Absalom Kibanda ana hoja yake katika 0001 na 0002. Wewe una maoni gani? Tujadili.

Tuesday, January 29, 2008

Kofi Anna bado amekwama Kenya

Ufumbuzi wa mgogoro Kenya bado ni mgumu. Mauaji yanaendelea, huku Mwai Kibaki na Raila Odinga hawajakubaliana mahali pa kuanzia mazungumzo, bado wanashitakiana kwa mauaji ya kimbari. Na kwa mara ya kwanza, mwansiasa, mbunge wa upinzani kauawa na kuibua ghasia mpya. Wakati huo huo, jamii inaendela kumshinikiza Kibaki ajitoe mhanga kuleta amani. Sasa Kofi Annan na timu yake ya wapatanishi wametoa ajenda ya mjadala wa usuluhishi. Itakubalika sawa kwa pande zote?

Friday, January 25, 2008

Tabasamu hili linaficha nini?


Kenyan embattled President Mwai Kibaki shakes hands with ODM leader Mr Raila Odinga at Harambee House, Nairobi, on Thursday. Picture by Govedi Asutsa. Source: The Standard Online, January 25, 2008. But mistrust still reigns. See here: 00. 01. 02. 03 04. 05. 06. 07. 08. 09. 10.

Tuesday, January 22, 2008

Raila ampeleka Kibaki kizimbani

Ukisikia Nguvu ya Umma ndiyo hii. Matukio haya yanaendelea kudhihirisha kwamba sasa Kenya inaongozwa na marais wawili. Mmoja wa kuchaguliwa na wananchi na mwingine wa kupachikwa na Tume ya Uchaguzi. Mmoja anashikilia na kutumia vyombo vya dola, mwingine anashikilia na kutumia imani ya wananchi. Acha Kibaki akae Ikulu, lakini kama analala usingizi, basi si binadamu mwenzetu. Moto bado unawaka, na kama mambo yataendelea hivi, na hasa baada ya ODM kumfikisha kizimbani, cha moto atazidi kukiona. Soma mwenyewe.

Wakati huo huo, mambo yanaanza kupata mwelekeo nchini Kenya baada ya Kofi Anna kuanza kazi ya usuluhishi na upatanishi. Baadhi ya mapya mpya haya hapa. 0. 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10.

Sunday, January 20, 2008

CCM ya ufisadi na utumwa

Msanii huyu wamemnunua, wakampa ajira na uanachama, na wakamuahidi makubwa, halafu wakamnyima. Sasa ameamua kubwaga manyanga na kuwarudishia kadi yao. Nionavyo mimi, kununua na kuchuuza binadamu wenzetu ni ufisadi na ni utumwa unaoendekezwa na CCM ya Jakaya Kikwete na Yusuph Makamba. Soma na toa maoni yako.

Friday, January 11, 2008

Hongera Dk. Slaa


Kwamba Rais Jakaya Kikwete amemfukuza kazi Gavana wa Benki, Daudi Ballali, ni jambo la kutia moyo. Pongezi anazopata Rais Kikwete sasa anazistahili. Lakini sote tunajua kwamba Rais Kikwete amelazimika kuchukua hatua hizo, ingawa serikali ilikuwa inajua 'matatizo' ya Benki Kuu. Kama si Dk. Willibord Slaa (pichani) na wenzake kuibua hoja hiyo Bungeni na kushinikiza serikali ichukue hatua, uchunguzi usingefanyika, na hatua hii moja isingechukuliwa. Kwa sababu hiyo, wanaompongeza Rais Kikwete wasimsahau yule aliyemsukuma, Dk. Slaa.
Haya yote yameonyesha kuwa serikali na watu wake ilijua ukweli wa tuhuma alizotoa Dk. Slaa, ndiyo maana hata Jaji Mark Bomani akawaonya waliotishia kumshitaki mtoa tuhuma, ambao waliishia kutoa vitisho lakini hadi leo hawajakanyaga mahakamani. Na sasa tayari ametangaza kuwa ana siri nyingine kubwa za wizi wa vigogo. Ndiyo maana nasema, katika hili la JK kuchukua hatua, shujaa ni Dk. Slaa. Na tayari kuna dalili kwamba Ballali hatakubali kutolewa kafara na kufa peke yake.
Tetesi zinazovuma sasa, kutokana na usiri wa serikali juu ya suala la Ballali, ni kwamba ugonjwa wake ulisababishwa na sumu aliyolishwa kumkolimba, ili siri zao zisitobolewe! Lakini sasa inasemekana naye kaamua kufa na serikali.

Tuesday, January 08, 2008

Asanteni

Kwa unyenyekevu mkubwa, nawashukuru walionipendeza kwa tuzo hii ya Excellence in ICT Journalism katika Afrika. Siwajui, wanajijua. Nawashukuru na majaji walionipigia kura. Asanteni!

Sunday, January 06, 2008

Wahariri wakatwa mapanga

Wapambanaji wenzetu wawili, Ndimara Tegambwage na Saed Kubenea, wanaochapisha gazeti la MwanaHalisi wamevamiwa ofisini na kukatwa mapanga Jumamosi 6, 2008 katika ofisi za gazeti hilo, Kinondoni, Dar es Salaam. Tayari hisia za wananchi zinawatuhumu baadhi ya mafisadi serikalini na wapambe wao, kwa kuandaa 'ujambazi huu.'

Kubenea ndiye Mhariri Mtendaji na mmiliki wa gazeti hilo, wakati Ndimara ni Mhariri Mshauri na 'mashine' ya kitaaluma ya gazeti hilo.

Gazeti hilo limekuwa na makala na habari kali mno dhidi ya wezi ndani ya serikali. Mara kadhaa Kubenea ameonywa na Ofisi ya Waziri Mkuu na Idara ya Habari (MAELEZO) kwa barua, simu na mdomo. Kuna wakati gazeti 'lilivamiwa' na watendaji wa serikali kwa kisingizio cha kukagua 'uwezo wa kitaaluma wa waandishi' wa gazeti hilo. Mara nyingine lilivamiwa na watu wa TRA, eti kutazama kama linaipa kodi.

Vile vile, ndilo hazeti lililowahi kumtuhumu kiongozi mmoja wa juu serikalini, ambaye lilimuita Bwana 'mvi' kwa kuwaagiza wahariri kadhaa rafiki zake waanze mkakati wa kuwaandama wakosoaji wa serikali.

Ikumbukwe kwamba ndilo gazeti pekee lililotaja majina ya mafisadi waliotajwa na Dk. Willibroad Slaa bila kificho, mbele ya umma, pale Mwembe Yanga, Dar es Salaam.

Tujadiliane


Mwaka 1991, aliyekuwa Rais wa Zambia, Kenneth Kaunda alishindwa na wapinzani katika uchaguzi mkuu, akawakabidhi madaraka bila ghasia. Mwaka 2000, aliyekuwa Rais wa Senegal Abdou Diouf alikabidhi madaraka kwa washindi na kuondoka Ikulu kwa amani. Mwaka 2002, aliyekuwa Rais wa Kenya, Daniel arap Moi, alimkabidhi Mwai Kibaki (pichani kushoto) uongozi, baada ya mteule wake aliyeandaliwa kuwa mrithi wake, Uhuru Kenyatta wa KANU, kushindwa na nguvu ya upinzani.

Mwai Kibaki aliyepishwa na Moi, ameshindwa kukubali matokeo baada ya miaka mitano tu ya kukaa Ikulu na kukataliwa na wapiga kura. Ghasia zimezuka, damu zimemwagika. Amejiunga na klabu ya marais wezi wa kura, kina Robert Mugabe na Amani Karume. Tanzania tunajifunza nini? Afrika yetu inaelekea wapi? Tufanye nini kuinusuru? Hawa wametoa maoni yao. Wewe una maoni gani? Tujadiliane.


My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'