Friday, February 29, 2008

Mageuzi ya Kenya

Hatimaye mahasimu wa kisiasa nchini Kenya, Mwai Kibaki na Raila Odinga, wametiliana saini kuanzisha mchakato mpya wa mageuzi ya kisiasa nchini Kenya. Sasa (hata bila kusubiri hatua zijazo) tunaweza kuwaita Rais Kibaki na Waziri Mkuu Odinga . Wameandika historia. Dunia imeshuhudia. Je, Mkataba huu utadumu? Huko nyuma, Kibaki aliwahi kumsaliti Odinga. Je, sasa wanaaminiana, au wanategeana? Je, Afrika imejifunza lolote kutoka Kenya? Tujadili.

Friday, February 08, 2008

Lowassa nje, Pinda ndani: kashfa zinaendelea

Ripoti ya Dk. Mwakyembe kuhusu kashfa ya Richmond dhidi ya Waziri Mkuu Edward Lowassa na mshirika wake, Rostam Azizi, imezaa matunda. Tayari Lowassa amejiuzulu. Mimi nimempongeza Lowassa kwa kutusaidia kuvunja Baraza la Mawaziri. Mizengo Pinda ameteuliwa na kuthibitishwa kuwa Waziri Mkuu. Kinachoshangaza watu sasa ni kwamba Kikwete bado anamuonea huruma na kumtetea waziwazi Lowasa. Kuna nini? Au ina maana rais anawajua wahusika halisi wa kashfa hii? Je, kujiuzulu kwa Lowassa ndiyo mwisho wa hoja ya ufisadi wa serikali na CCM? Absalom Kibanda ana hoja yake katika 0001 na 0002. Wewe una maoni gani? Tujadili.
My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'