Friday, August 31, 2007

Hekalu la Manji?

Bwana ee! Tazama nyumba hii. Lakini Waswahili wanasema imevuka viwango vya kuitwa nyumba. Hili ni Hekalu. Na hizi hapa chini ni sehemu chache za hekalu hilo. La nani? Aliyetuma hizi ni la Yusuf Manji - yule mfadhili wa Klabu ya Yanga; "mgomvi" wa Regi Mengi (na sasa hivi Waislamu kuhusu kiwanja); mfadhili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM); lakini mmoja wa wasomaji wa blogu hii anasema si kweli bali ni nyumba ya Rais Pervaiz Musharaf, mtu aniyejipenda kweli kweli, mchezaji hodari wa Badminton, Jenerali wa Pakistani. Iwe ya yeyote yule, inapendeza na kuvutia. Tazama!

Endelea


Sema mwenyewe


Quite Spacious


Hapa je?


Safi


Chunga, chini panateleza


mh


Mh!


Tuizunguke meza hii


Zungumza, ukichoka pumzika kidogo


Unataka kuogelea?Labda haya ndiyo Maisha Bora. Tumuulize Kipanya hapo chini!

Thursday, August 30, 2007

Maisha Bora


Nimeipenda katuni hii ya Maosud 'Kipanya.' Wewe je?

Zitto apikiwa kashfa mpya


Habari zilizotapakaa ni kwamba wanamtandao, wakiongozwa na kinara wao, Rostam Azizi, wanapika kashfa mpya dhidi ya Zitto Kabwe (pichani kulia). Eti walitengeneza ya Amina Chifupa ikawalipukia na kuua mtu. Hawakuridhika. Wamejarbu kumdhalilisha Bungeni, akaibuka mshindi. Wananchi wanamshangilia, CCM wakazomewa. Sasa wamesikia Zitto na viongozi wa CHADEMA wanaanza kuzunguka mikoa 10 kuishitaki serikali kwa umma, wanamtandao wanakula njama mpya kwa kutumia baadhi ya vyombo vya habari 'kupika' kashfa mpya. Nia yao ni kupunguza imani ya wananchi na mvuto wa Zitto. Wamekiri, lakini inawauma, kwamba kwa sasa, Zitto amemfunika JK kwa mvuto.

Je, wahariri watakubaliana na mbinu za kina Rostam Azizi? Je, wananchi watamtosa Zitto? Kumkumbatia nani? Je, serikali itabadili sera zake kuhusu madini au itaendelea tu kuhangaika na namna ya kumsakama Zitto?

Tuesday, August 21, 2007

Uchumi ukue, bei zipande hivi?

Waziri Mkuu, Edward Lowassa, anasema uchumi unakua. Lakini wataalamu wanasema bei za bidhaa zinapanda kila siku. Ni ukuaji gani huu wa uchumi? Habari hii imeandikwa na gazeti la serikali, Daily News Agosti 21.08.2007. Soma mwenyewe uone hali ilivyo.

Inflation nears double digits

Overall inflation rate jumped to nine per cent in July, from 5.9 per cent in June, a trend which the National Bureau of Statistics (NBS) attributed to increased food and non-food prices.

“The July 2007 inflation rate has gone up by 3.1 percentage points compared to the June figure,” the Bureau said in a statement made available yesterday. “Some prices for both food and non-food items had gone up,” it added.

Analysts feared the impact of price hikes on the economy, with inflation, a key indicator for consumer comfort and investor confidence, nearly hitting the double digit mark, the highest in more than five years.

The government had for the last three years, targeted to push inflation to a manageable below 4.0 per cent, which could now prove to be quite an uphill task. Before, inflation had nearly dragged the economy to its knees with almost record over 30 per cent rate.

Planning, Economy and Empowerment Minister Professor Juma Ngasongwa told parliament in June that in 2006, average inflation was 7.3 per cent, compared to 5.0 per cent in 2005. In March, this year, inflation was recorded at 7.2 per cent.

The minister attributed the upswing in inflation to increased commodity prices, especially food and petroleum products which also led to high costs of transport and generation of thermal electricity.

The minister expressed optimism on declining inflation after some parts of the country started harvesting food crops, saying in April 2007, the inflation rate had declined to 6.1 percent, from 7.2 per cent registered in March 2007.

NBS said in the statement yesterday that hiked food prices were wheat flour, bread, spaghetti, potatoes and meat. Prices of bananas, fish, cooking oils, beans, cowpeas, sugar and meals in restaurants had also gone up.

It said non-food items that had increased prices were instant coffee, rent, kerosene, electric cookers, sewing machines, kerosene stoves, laundry soap (bar and powdered), scrubbing brush, broom head, tooth brush and hair creams.

Prices that have also gone up include those of car batteries, diesel, petrol, bus fares and private secondary school fees.

However, it noted that prices of clothing, footwear, watches and cell phones had gone down.


Daily News Reporter
Daily News; Tuesday,August 21, 2007 @00:02

Sunday, August 19, 2007

Picha nyingine za Zitto na waandamanaji

Bonyeza hapa uone picha na usome mjadala mwingine mpana.

Habari Leo waua stori ya Zitto Kabwe


Magazeti ya serikali, Sunday News and Habari Leo Jumapili, 'yalikataa' kuandika habari za maandamano na mkutano wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, uliofanyika Dar es Salaam Agosti 18 kulaani hatua dhalimu ya Bunge dhidi ya mbunge huyo. AIBU!
Waandishi wao waliyashuhudia maandamano, mkutanoni walikuwepo, lakini walishindwa kutekeleza wajibu wao wa kitaaluma. UZALENDO uko wapi? Kama wanawadharau hao waliokusanyika kumsikiliza Kabwe, wanamwandikia nani?
Hata hivyo, mpiga picha wao aliweza kumshawishi mhariri wake kutumia walau picha inayoonyesha sehemu tu ya umati uliokusanyika Jangwani kumsikiliza Kabwe. Tazama mwenyewe.

Karamagi anasafiri na mihuri yetu?


KAMA Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, anaweza kusaini mkataba wa madini nje ya nchi, London, Uingereza, wakati yuko ziarani na Rais Jakaya Kikwete, ina maana anasafiri na mihuri yetu? Pata uchambuzi wa swali hili HAPA, na toa maoni yako chini.

Saturday, August 18, 2007

Kishindo cha Zitto Kabwe


Dar es Salaam inazizima. Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, amegeuka shujaa wa mwaka. Habari kutoka Dar zinasema amekuwa gumzo kila kona, wala mvua nzito haikuweza kuwazuia wananchi kuandamana na kusukuma gari lake kutoka Ubungo hadi viwanja vya Jangwani, Jumamosi, Agosti 18, 2007, alikohutubia mkutano mkubwa na kusema Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, alisaini mkataba katika Hoteli ya Churchill, London, Uingereza.

Watawala wameduwaa. Bomu walilompasulia Zitto kumdhalilisha limewalipukia wenyewe! Hiki ndicho kishindo kinachozungumzwa. Anasema "tusikumbatie walioshiba" Ipate pia kwa kimombo Hoja kamili na mjadala wake Bungeni HII HAPA. Baadaye, wawekezaji wenyewe, Barrick walijitokeza kutoa maelezo HAYA, lakini Zitto akayachambua pia maelezo hayo na kubainisha uhusiano wa karibu sana kati ya waziri na wawekezaji, huku wakitoa maelezo yanayojikanganya zaidi.

Tuesday, August 14, 2007

Nauliza Kujibiwa

Mpendwa msomaji, nakamilisha mada yangu katika mazungumzo nitakayoshiriki kwenye kongamano la Highway Africa litakalofanyika Septemba 10-12, 2007, Rhodes University, Afrika Kusini. Nimefikiri kwamba ni vema kupata na kutumia mawazo ya wanablogu wenzangu na wasomaji wa blogu hii katika maswali kadhaa ninayojiuliza. Naomba ushiriki wako kwa kujibu maswali yafuatayo kwa kadiri unavyoona inafaa. Nakuhakikishia kwamba nitakapohitaji kutumia mawazo yako mahali popote, nitakunuu bila kuongeza chumvi. Asante. ANSBERT NGURUMO.

1. Kama wewe ni mwanablogu, kwa nini unablogu? Kama si mwanablogu, kwanini unasoma blogu?

2. Je, ni vema wanablogu (na wachangiaji wa maoni) watumie majina yao halisi? Faida na hasara zake ni nini?

3. Je, matumizi makubwa ya blogu yanamaanisha enzi za vyombo vya habari vya kale (redio, magazeti na TV) vimepitwa na wakati?

4. Je, wanablogu wanawajibika kwa nani?

Sunday, August 12, 2007

CCM inaandaa mapinduzi?

MAISHA magumu, kauli na uamuzi tata wa viongozi, mwafaka usiofikika? Vinatupeleka katika mapinduzi mengine? Hilo ndilo swali lwa wiki hii. Soma hapa.

Saturday, August 11, 2007

Wafanyakazi waitolea uvivu serikali


Haijapata kutokea. Terehe 11.Agosti.2007 iliandika historia mpya Tanzania. Wafanyakazi wameandamana na kuilaani serikali ya awamu ya nne kwa kuwadhalilisha, kuwasahau na kuwafanya watumwa katika nchi yao. Ujumbe wao ulifikishwa kwa maandamano, nyimbo, mabango na hotuba kali. Gazeti la Mwananchi Jumapili linaripoti hivi:

Wafanyakazi wampa Rais Kikwete siku 30

*Wamtaka Katibu wao kumwona na kurejesha majibu
*Wadai matumizi ya sheria kudai haki yameshindikana
*Walalamikia mishahara ya wabunge na ununuzi wa mashangingi

WAFANYAKAZI mkoani Dar es Salaam, wamempa siku 30 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (Tucta), Nestory Ngulla, kufikisha malalamiko yao kwa Rais Jakaya Kikwete na kurejeshewa majibu, kuhusu nyongeza duni ya mishahara, ili kuepusha hatua nyingine watakazotumia kudai mishahara.

Tamko hilo lilitolewa na wafanyakazi hao kupitia risala yao iliyosomwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam baada ya kuhitimisha maandamano ya amani yaliyoandaliwa na vyama 18 vya wafanyakazi nchini kupinga kima cha chini cha mshahara wa serikali, kilichopitishwa na bunge hivi karibuni.

Baadhi ya vyama hivyo, ni pamoja na cha Walimu (CWT), Sekta ya Afya (Tughe), Migodi, Nishati, Ujenzi (Tamico), Serikali za Mitaa (Talgwu), Mabaharia (Tasu), Walinzi binafsi (Tupse), Mashambani (Tpawu), Shughuli za Meli (Dowuta), Mawasiliano (Tewuta), Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Habari na Utafiti (Raawu), Waandishi wa Habari (TUJ) na Chodawu.
Akisoma risala hiyo kwa niaba ya wafanyakazi hao, Katibu wa Raawu, Kanda ya Mashariki, Evarist Mwalongo alisema wamefikia hatua hiyo wakiamini kwamba, matumizi ya kisheria kudai mishahara yatawafikisha katika hali mbaya.

"Hali hiyo itakuwa imelazimishwa na serikali. Wafanyakazi hatutaki kufikia hali hiyo kwani Uhuru wa nchi hii tuliutolea jasho sisi wenyewe," alisema Mwalongo na kushangiliwa na umati wa wafanyakazi waliohudhuria mkutano huo.

Mwalongo alisema, wafanyakazi mwaka huu, wanadai nyongeza ya mishahara kutokana na kukithiri kwa shida baada ya nyongeza hiyo kulimbikizwa kwa miaka zaidi ya 13 iliyopita, hali ambayo imesababisha makali ya maisha kutovumilika tena.

Kutokana na hali hiyo, alisema serikali imekosa huruma na kuacha kutambua kuwa wafanyakazi nchini ndio waliodai Uhuru wakisaidiana na wakulima, badala yake imekuwa ikiwajali wafanyabiashara peke yake kwa kuwafanya kama ndio mhimili wake wa kusimamia sera, uchumi na siasa za nchi.

Mbali na hilo, Mwalongo alisema serikali imefikia kupuuza hata sheria zilizotungwa kusimamia na kulinda masilahi na masuala ya wafanyakazi.

Alisema inasikitisha kuona Wizara ya Utumishi chini ya Waziri wake, Hawa Ghasia, imeamua kudharau sheria namba 19 ya mwaka 2003 inayohusu majadiliano na vyama vya wafanyakazi kupanga mishahara ya watumishi wa serikali.

"Mheshimiwa Ghasia ameamua kupuuza utawala wa sheria na kuanza ukurasa mpya. Amepanga mishahara ya watumishi kadri alivyoona yeye kutoka Sh75,000 hadi Sh84,000.
Mshahara wa Sh84,000 unakatwa kodi ya Sh 600 kama kodi ya PAYE na akiba ya uzeeni Sh8,400, zinabaki Sh 75,000 ambazo ndiyo mshahara wa zamani.

"Mshahara huo ukigawa kwa Sh 30 utaona mfanyakazi ataishi kwa Sh2,500 kila siku ambazo zitumike kama matumizi mengine ya lazima kila siku. Kwa mantiki hiyo ndiyo maana vyama vya wafanyakazi vilipendekeza kima cha chini kiwe Sh315,000 sawa na Sh10,500 kwa siku," alisema Mwalongo.

Alisema inasikitisha pia kuoana Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana chini ya Waziri wake, Kapteni John Chiligati, imeamua kulala usingizi kwa kutosimamia sheria namba 6 ya mwaka 2004 inayotakiwa kuunda Baraza la kupanga kima chini cha mishahara kwa ajili ya sekta binafsi ambako kuna hali mbaya kupindukia kwa kuendelea kupata mshahara wa Sh48,000 tangu mwaka 2002.

"Sisi wafanyakazi hatuelewi kama serikali ipo kwa ajili ya Watanzania kwani kwa mshahara wa Sh84,000 ukigawa kwa Sh10,500 kama matumizi kwa mahitaji ya lazima ya kila siku utadumu siku nane na kama mfanyakazi atakula mlo mmoja kwa siku utadumu siku 16 tu.

"Mshahara huo wa Sh84,000 ni asilimia 50 au nusu ya posho ya mbunge anayopata katika kikao cha siku moja na mshahara wa mbunge wa mwezi mmoja ambao ni Sh1,500,000 unaweza kumlipa mfanyakazi huyo kwa miezi 17.

Uchambuzi kama huu ukiwekwa watumishi wa kima cha Sh84,000 inasikitisha kiasi cha kujenga hasira mbaya katika jamii ya Watanzania," alisema Mwalongo.

Alisema pamoja na shida za mishahara duni, serikali imetengeneza mzigo mzito unaotokana na bajeti ya mwaka huu wa fedha wa 2007/08, iliyokuja na kodi kubwa katika mishahara, mfumuko wa bei uliotokana na bei kubwa ya mafuta ya dizeli, petroli na vilainishi vya mitambo na kwamba, usafiri wa kwenda kazini na kurudi nyumbani umekuwa pia gharama kubwa inayowatesa wafanyakazi maradufu.

"Kukosekana kwa vyombo vya usafiri, suala hili halishughulikiwi na serikali kwa vile wakuu wote wanatumia magari ya gharama za kutisha yanayowalaza usingizi wasione kuna nini kwa wananchi. Inasikitisha kuona kiongozi anapita na VX ya Sh150 milioni bila hata ya huruma kwa mtoto au watoto wa shule kama hapendi kuwapa msaada wafanyakazi wenzie ingetosha kuwaonea huruma watoto wa shule.

"Gari aina ya VX moja ingeweza kununua gari la kubebea wafanyakazi zaidi ya 100. Mfano huu ukizidishwa kwa namba ya magari ya mawaziri na watendaji wakuu wa serikali yetu utaona serikali inao uwezo mkubwa sana wa kugawa mshahara wa kuishi wa Sh 315,000 bila kikwazo," alisema Mwalongo.

Alisema mishahara midogo wanayolipwa wafanyakazi, inaleta uhafifu katika malipo ya uzeeni kwa wastaafu ambao wametumikia serikali kwa uadilifu mkubwa.

Mwalongo alisema bila kujali kuwa mishahara ni midogo, serikali bado inaendelea kuwaonea wafanyakazi kukopa kwa nguvu jasho la wanyonge, kwa kulimbikiza madai ya nauli, likizo, malimbikizo ya mishahara ya wafanyakazi, kama vile walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam na watumishi wengine wa manispaa na mashirika mbalimbali.

Alisema wakati hali ikiwa hivyo, soko la ajira limetekwa na wageni kwa visingizio na kejeli dhidi ya wafanyakazi wazalendo, kwamba Watanzania ni wavivu, wazembe, hawajui Kiingereza na kadhalika.

"Inasikitisha wanaotoa kauli hizo ni Watanzania wenzetu bila kutambua kuwa dawa za kutibu uzembe, uvivu na kutojua Kiingereza ni malipo mazuri, mbona Watanzania wanang'ang'aniwa nchi za nje kwa bidii ya kazi na kuzungumza Kiingereza chenye fasihi tamu?

"Tunasema waache kutukejeli kuanzia sasa, iwe mwisho kuuza nafasi zetu za kazi ovyo, waone aibu wawekezaji wao wameanza kuwekeza mpaka katika vibanda vya kukaanga viazi na maua ya plastiki, watainuaje uchumi wetu?" alihoji Mwalongo.

Kutokana na hali hiyo, alisema iwapo mishahara haitaongezwa italeta athari kubwa, ikiwamo wafanyakazi kushindwa kushiriki katika vita dhidi ya rushwa, kiwango cha umaskini kitakithiri katika jamii, kipindupindu, ujinga, kukosekana tija ya taifa na nidhamu ya kazi.

Akizungumza katika mkutano huo, Mhadhiri Mstaafu wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Issa Shivji, aliishangaa serikali kuona ikikataa kutambua kwamba, wananchi hivi sasa wanakabiliwa na kipindi kigumu kutokana na kujenga mgawanyiko na mpasuko katika jamii ya Watanzania.

"Kuna kundi la matajiri na maskini, tuna tabaka la walala heri na walala hoi. Kama tutaendelea katika mwelekeo huu kwa kasi, tutajikuta tuna mataifa mawili," alisema Profesa Shivji na kushangiliwa na umati wa wafanyakazi waliohudhuria mkutano huo.

Katibu wa Kanda ya Dar es Salaam wa Chama cha Wafanyakazi wa Mawasiliano na Uchukuzi nchini (Cotwu), Buhari Semvua, akizungumza katika mkutano huo, alipinga msimamo wa serikali wa kuendelea na majadiliano Septemba, mwakani na wafanyakazi kuonya kuwa iwapo serikali itapuuza malalamiko yao nchi haitakalika.

"Hatukubali hiyo mwakani na wajue kuwa wananchi wakikata tamaa, hatua watakazochukua, patakuwa hapakaliki, hapatoshi. Siku 30 tusipojibiwa, hizi (maandamano) za leo ni rasharasha," alisema Semvua.

Naye Ngulla ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo, aliwataka wafanyakazi kutobabaishwa na wabunge na kuahidi kwamba, atahakikisha anafikishia serikali malalamiko yao ndani ya muda aliopewa.

Mkutano huo ulitanguliwa na maandamano ya wafanyakazi hao yaliyoanzia katika Ofisi za Makao Makuu ya Tucta, Mnazi Mmoja saa 2:00 asubuhi na kupita katika Barabara za Bibi Titi Mohamed na Morogoro na kuishia katika Viwanja vya Jangwani, huku waandamanaji wakiwa wamebeba mabango na kuimba nyimbo zenye ujumbe wa kuilaani serikali.

Baadhi ya mabango yalisomeka: "Walalahoi Sh84,000 kwa mwezi, mbunge Sh120,000 kwa siku, haki iko wapi?" "Mshahara huishia nauli ya daladala, vigogo kwenye mashangingi, kima cha chini kiongezwe, hii ni haki", "Mishahara iendane na hali halisi ya uchumi wa nchi kwa sasa", "Bila walimu Rais Kikwete ungekuwa wapi? Mbona hutukumbukwi?"

"Nauli za likizo hazitolewi kwa wakati kwa nini? Walimu tunateseka", "Haturidhiki na waraka mpya wa mshahara", "RAAWU Taasisi ya Watu Wazima. Kwa ari hii, kasi hii, nguvu hii na mishahara hii ya wafanyakazi tumekwisha!" "Kuna siri gani kati ya sekta binafsi na serikali kuhusu mishahara?"

Mbali na mabango hayo, waandamanaji hao walikuwa wakiimba kwa kusema: "Na sisi hatulali, bado mapambano, mpaka kieleweke", "Kilio, kilio, kilio, tutamlilia nani?"

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'