MAJUZI, Rais Jakaya Kikwete alikutana na 'wafadhili' wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), jijini Dar es Salaam, waliokisaidia kupata pesa za kampeni mwaka 2005. Katikakuzungumza nao, Kikwete alisisitiza mambo mawili. Kwanza, aliwaomba wana CCM wasilewe ushindi walioupata mwaka 2005, badala yake wajiandae kwa uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2010. Hii ni changamoto nzuri kutoka kw amtu anayetarajiwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho katikati ya mwaka huu. Pili, aliwaasa wanachama wenzake waanze kutafakari namna ya kupata
MAPATO HALALI kwa ajili ya kampeni. Hili ndilo linazua maswali, hasa kwa kuwa limesemwa sasa baada ya chama kushinda kwa nguvu kubwa ya pesa, huku kikiwa kinashutumiwa kusaidiwa na matajiri kadhaa wanaojihusisha na ujambazi. Je, Kikwete anakiri kwamba ameingia madarakani kwa kutumia pesa haramu? Na je, vyanzo haali vikikosekana, au kama havitatosha, CCM itapataje ushindi? Au itarudi kule kule?! TUJADILI.