Wednesday, March 15, 2006

Nani anasema JK hayawezi?


Mwanablogu Reginald Simon Miruko ndiye kanitumia picha hii. Miss Personality, Witness Manwingi, ambaye alikuwa mwakilishi wa Tanzania katika shindano la kumtafuta Miss Tourism wa Dunia mwaka 2006 anasalimia Rais Jakaya Kikwete wakiwa wamekumbatiana. Wote wanatabasamu, wanapendeza na wameshikana VIZURI! Au nimeshindwa kuitafsiri barabara?

2 comments:

Reginald S. Miruko said...

Picha hii si yangu: Nimeipata kutoka kwa MWANABLOGU MICHUZI. Naheshimu sheria ya hakimiliki. Nilikutumia ili uionje kwa ukaribu ndani ya e-mail yako na kutambua kazi ya Michuzi. RSM

MK said...

Samahani ingawa haya siyo maneno yanayo endana na kichwa cha habari lakini naomba nitoe tangazo langu kuhusu blog.

TANGAZO:

Baada ya uchunguzi wa hali ya juu nimegundua jawabu la kuondoa Blogger NavBar (Sehemu ya juu kabisa ya Blog yako inayo onesha search this blog).

Hii kutokana na ya kwamba watu wengi uwa wanachukizwa na jinsi hiyo NavBar ilipo.

Jawabu la hili swali unaweza kusoma kwa kubonyeza hapa

Kama ukipata tatizo au maswali zaidi naomba niandikie na nitakujibu asap.

Nashukuru,
©2006 MK

Imetengenezwa na kuletwa kwenu na ©2006 MK

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'