Monday, December 24, 2007

Krismasi Njema


Napenda kuwatakia Krismasi Njema! Krismasi ni tukio lenye maana mbalimbali kwa watu mbalimbali. Kwa wengine ni 'kumbukumbu' ya kiroho ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo zaidi ya miaka 2007 iliyopita. Kwa wengine ni tukio kubwa lililoigawa historia katika ngwe mbili - Kabla ya Kristo na Baada ya Kristo. Kwa wengine (hasa Ulaya Magharibi) ni wakati wa kumaliza mwaka, kujipongeza na kujiandaa kwa mwaka mwingine; ni kipindi cha manunuzi na matanuzi. Kwa wengine halina maana kabisa, lakini wanajikuta wakiungana na wenzao wanaosherehekea Krismasi. Kwa wote hao, nasema Heri ya Krismasi na Mwaka Mpya 2008.

4 comments:

Anonymous said...

Natumai siku zijazo utatupa mkono wa Idd,maana tupo wengine waumini wa IDD,natumai hutotubagua ahsante

Anonymous said...

If all sites are like this the world would be a hell today. But soon every careless world that has been typed or said will be brought to book. Kwanini musiandike mambo ambayo niya manufaa kwa ujenzi wa amani ya taifa letu Kenya? Wacheni siasa ambazo hamuelewi. kuandika maoni ya duni ya kisiasa na ambayo ni ya uongo mtupu. Aibu kwenu!!

Anonymous said...

wewe uliyeandika hapo juu ni mmoja wa watu waoga, wajinga na wanafiki wasiojua maana ya "amani" na "siasa" ambayo umeyatumia kikasuku. Fikra yako ni mojawapo ya mambo yanayopaswa kukombolewa kutoka utumwani, na kama huwezi kujikomboa mwenyewe tutakukomboa sisi, hata kama huoni maana ya ukombozi wenyewe. Watu wenye fikra kama hizi ndio wameifikisha Tanzania hapa ilipo...na ndio wanahatarisha amani yetu.

Anonymous said...

James, huyu jamaa anayekandia uandishi huu ni mpuuzi tu, ndio hao wanaotafutwa. Angekuwa na akili angeweka jina na anuani yake ili tuwasiliane naye moja kwa moja. Enzi za Tanzania kuliwa na wahuni kama hao anaowatetea kwa kisingizio cha amani, zimepita na hatutaruhusu tena nchi yetu ichezewe hovyo hovyo. Heko Ngurumo na wenzio....

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'