KATIKA taarifa ya jana, Polisi Mkoani Arusha walisema wameua watu wawili tu; baadhi ya vyombo vya habari, kikiwamo BBC, vikadai wamekufa watu wapatao 10. Polisi wakadai walipiga risasi watu sita (6) tu, lakini viongozi wa Chadema walipoachiwa na mahakama wakaenda kutembelea majeruhi hospitalini, walikuta wananchi wapatao 38 wote wana majeraha ya risasi. Chadema wakaunda kamati ya kuwahudumia majeruhi hao. Sasa inadaiwa polisi wamekula njama na uongozi wa hospitali hiyo ya Mount Meru, wamewatorosha majeruhi hao, hawajulikani walikopelekwa, ili kuficha ukweli kuhusu idadi ya waliojeruhiwa kwa risasa. Viongozi wa Chadema wanaendelea kufuatilia. Tusipochunga, taratibu, Tanzania itageuka Police State!
Ajabu ni kwamba Polisi hawajawakamata polisi hao walioua raia; badala yake wanawakamata raia waliokuwa wanatembea kwa miguu (wanaandamana sio?) kuelekea mkutanoni.