Friday, January 07, 2011

Mkanganyiko wa risasi za moto dhidi ya raia Arusha

KATIKA taarifa ya jana, Polisi Mkoani Arusha walisema wameua watu wawili tu; baadhi ya vyombo vya habari, kikiwamo BBC, vikadai wamekufa watu wapatao 10. Polisi wakadai walipiga risasi watu sita (6) tu, lakini viongozi wa Chadema walipoachiwa na mahakama wakaenda kutembelea majeruhi hospitalini, walikuta wananchi wapatao 38 wote wana majeraha ya risasi. Chadema wakaunda kamati ya kuwahudumia majeruhi hao. Sasa inadaiwa polisi wamekula njama na uongozi wa hospitali hiyo ya Mount Meru, wamewatorosha majeruhi hao, hawajulikani walikopelekwa, ili kuficha ukweli kuhusu idadi ya waliojeruhiwa kwa risasa. Viongozi wa Chadema wanaendelea kufuatilia. Tusipochunga, taratibu, Tanzania itageuka Police State!

Ajabu ni kwamba Polisi hawajawakamata polisi hao walioua raia; badala yake wanawakamata raia waliokuwa wanatembea kwa miguu (wanaandamana sio?) kuelekea mkutanoni.

4 comments:

Anonymous said...

inasikitisha waliofariki, kweli polsi tz wanyama, hao wagonjwa si wahamishiwe private kama uongozi hosp unatorosha wagonjwa, na kwa nini watumie risasi halisi ina maana walipanga kuua?:

Anonymous said...

Huyo ndio Kikwete mtawala wa Tanzania. Let us see kama ana akili kuliko Mungu aliyeumba hawa watu.

Anonymous said...

Ngurumo asante. Nashukuru nasi tulionje ya nchi tunaofatilia janga la Arusha unaona kuna mchezo mchezo wa kitoto tu au ulevi au uhuuni wa viongozi. Sasa sisi tunajiuliza polisi tar 7 waliripoti kufa watu 2, wakati magazeti yakaripoti watu 3, baadae jana mchana RPC akaripoti eti mtu wa tatu alikufa asubuhi tar 8, wakati magazeti yaliripoti siku kabla.Sasa mtu mwenye akili ajiuliza tuamini askari au magazeti?Hawa polisi wanafanya nini?Waziri Nahodha hakukemea polisi kutumia risasi za moto. Risasi za moto huwa hazitumiwi na askari katika nchi zenye ustarabu kutawanya maandamano. Hutumika gesi ya kutoa machozi. Kumbuka watu si wanyama kuuliwa na serikali inayojali wananchi wake. Hiyo ndiyo kasi mpya na ari zaidi. Mimi nadhani waziri Nahodha alifurahi watu kuuawa. CCM imechoka iende ikapumzike.
Hawa wanamabalozi nchi nyingi ulimwenguni waangalie Paris, Roma, Berlin, New york, Whitehouse. Maandamano ni kitu cha kawaida hakuna anayepinga mtu risasi za moto. Mimi naona walipanga kudharirisha chadema lakini wadhalilisha na tunaeendelea kufumbuka CCM na Kikwete ni nani. Jana anaonekana anacheka na diplomatic corps hakuna lolote. Ansante Ngurumo

Anonymous said...

Haki ya mtu haipotei. Kama kweli CCM walipata ridhaa kwa wananchi ya kuendelea kututawala katika kipindi hiki cha miaka 5, basi, haya yote yanayotokea ni mapito. Lakini kama wanatawala kwa kupandikizwa na Tume ya Uchaguzi, basi wajue haki ya mtu haipotei; na mzimu wa dhambi hiyo ya kupora haki utawatafuna.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'