Friday, September 02, 2005

CCM imemshauri vibaya Kikwete

MWAKA 1995 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichangamkia mdahalo wa wagombea urais, wakati huo kikiwa kimemteua Benjamin Mkapa. Mwaka huu, chama hicho hicho kikiwa na mgombea mpya, Jakaya Mrisho Kikwete, kimekwepa mdahalo huo kikisingizia ratiba ngumu ya mgombea. Uamuzi huo wa CCM umezua hisia na maswali mbalimbali katika jamii. Wengine wanasema Kikwete kaogopa. Wengine wanasema CCM haikuhitaji mdahalo huo. Woga au si woga, kwa nini CCM imeingia mitini? Tafakari.

1 comment:

Innocent said...

Kwanza nimependa globu yako ni nzuri na inanipa mwangaza wa nini kinaendelea huko Tanzania kwa sasa.
Mimi ni mtanzania naishi hapa Uganda, hili la mdahalo nimeliona lina umuhimu sana hata nikaandika katika blogu yangu:http:/funguajicho.blogspot.com, utaweza kusoma.
Kazi nzuri sana unafanya bwana Ngurumo, wiki hii nitaipitia globu yako.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'