Monday, March 13, 2006

Kikwete, CCM na mapato haramu

MAJUZI, Rais Jakaya Kikwete alikutana na 'wafadhili' wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), jijini Dar es Salaam, waliokisaidia kupata pesa za kampeni mwaka 2005. Katikakuzungumza nao, Kikwete alisisitiza mambo mawili. Kwanza, aliwaomba wana CCM wasilewe ushindi walioupata mwaka 2005, badala yake wajiandae kwa uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2010. Hii ni changamoto nzuri kutoka kw amtu anayetarajiwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho katikati ya mwaka huu. Pili, aliwaasa wanachama wenzake waanze kutafakari namna ya kupata MAPATO HALALI kwa ajili ya kampeni. Hili ndilo linazua maswali, hasa kwa kuwa limesemwa sasa baada ya chama kushinda kwa nguvu kubwa ya pesa, huku kikiwa kinashutumiwa kusaidiwa na matajiri kadhaa wanaojihusisha na ujambazi. Je, Kikwete anakiri kwamba ameingia madarakani kwa kutumia pesa haramu? Na je, vyanzo haali vikikosekana, au kama havitatosha, CCM itapataje ushindi? Au itarudi kule kule?! TUJADILI.

2 comments:

boniphace said...

Mapato halali ni pamoja na waandishi kutolipwa na vyama vya siasa. Malipo ya huko nyuma sina shida ya kuyajaduili Miruko, tumeona kwa macho yetu kuwa siasa za Tanzania ni kununua madaraka, mwenye fedha ananunua kila kitu. Ananunua maisha na hili tazam majambazi waliotangazwa na polisi ni makuli na wabeba mizigo wa Gongo la Mboto. Fedha chafu zilitumika mno. Jimbo lipi, nianze na Kawe! Nirudi viti maalum hapo Dar, nende viti vya Vijana...hapa sisemi sana nitajaonekana na wivu ...we thubutu siogopi hata waseme nina wivu. Ndio nina wivu wa kuona Tanzania inaendelea na sio kuwa taifa la kutupilia jalalani baada ya kukosa waunda sera wenye utambuzi na wanaofaa kuwa mfano wa vizazi. Ok namaliza hapa nina kazi ya kuweka picha kwangu lakini naona zinagoma. Nitaziweka tu baadaye.

Anonymous said...

Ngurumo,
Kuna umuhimu mkubwa wa kuanza kulijadili suala hili sasa, ili huko siku za mbeleni lisije likatuletea matatizo. Naunga mkono hii hoja.
Londo

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'