Sunday, April 29, 2007

Boyz II Men wanaogopa kuitwa wasanii?


Soma Maswali yangu kwa serikali ya JK inayong'ang'ania kufuga na kutisha vyombo vya habari na wanahabari. Hii Hapa.

23 comments:

Said Michael said...

Hongera Chief, hapa umenena kama si kupasua jipu pwaaa...
Endelea kutupa vitu adimu

Anonymous said...

Kabisa!Huyo bwana anafaa awe afisa habari wa chadema!Msemaji safi sana huyo!huwa ana andika makala kisha bwana wake mbowe anaipitia kisha inatoka kwenye gazeti..halafu anadai yeye hanunuliwi mambo hayo!!!!Faddhala za ada hizo

Anonymous said...

Acha wee! Wewe ndiyo maana huandiki hata jina. Una nia chafu, na mawazo yako yamepinda. Kwa wanaomjua Ngurumo, wewe unajifanya kituko. Kumbukumbu zangu zinazieleza kwamba bwana huyu amekuwa akiandika kwa kalamu kali tangu akiwa RAI. Hajawahi kuwa shabiki wa serikali, na huwa anaandika mantiki. Huko RAI alikuwa amenunuliwa na nani? Makala zake za Mwananchi, dhidi ya serikali ya Mkapa, hukuziona? Alinunuliwa na nani?

Tuwe makini jamani. Huyu bwana anaandikia gazeti binafsi, hivyi ni haki kwake kuwa na mawazo binafsi na critical. Angekuwa amebadili uandishi wake, tungesema labda kuna jambo. hata hivyo, huu ndio uandishi wake tangu nimeanza kusoma makala zake miaka ya 90. Tukisema leo amenunuliwa eti kwa kuwa anaandika habari dhidi ya Kikwete ni kukosa fikra ya kiutu uzima, au ni kuonyesha uwezo wetu mdogo wa kumjua huyu bwana.

Zaidi ya hayo, mbona makala hii injajieleza? Huyu ni mwajiriwa wa gazeti analolitetea. Ni kununuliwa huko? Ebu kua bwana.

Ngurumo ana mawazo mapana. Serikali inapaswa iwe na wivu kwa kukosa watu wenye makali kama Ngurumo. Hapa amewachambua kama karanga, wakaonekana woet hawafai. Kwa nguvu ya hoja tu!

Asikatiswhe tamaa na watu wenye fikra za namna hii, kama za anonymous huyu anayemsema vibaya Ngurumo, ambazo kama ni sehemu ya fikra zinazoongoza nchi au chama cha mapinduzi, ndizo zinaleta mgando wa mawazo usiotupeleka kokote. Hapa kwa Ngurumo mmepata somo. Badilikeni!

Anonymous said...

Hongera kwa article nzuri. Ni makala ambayo nimeikubali. Kamwe msitishwe na watu hawa walafi na waroho wa mali za wananchi. Heko, tupo nyuma yenu.

Anonymous said...

Ansbert, Hongera kwa article nzuri. Ni kawaida kwa viongozi wetu kupinga kukosolewa, mkumbe Mkapa! Wanataka waibe tuwasifie...KAMWE HATUKUBALI.

Anonymous said...

Huyo anonymous wa kwanza ndio wale wale anaowasema Ngurumo. Hoja hawana, wanataka kupambana, sisi watazamaji tunajua nani pumba nani mchele.

Wanaringia madaraka na mabavu, lakini mwisho wao mbaya. Kama wana lolote si wajibu hoja za ngurumo kuliko kurukia vijinenoo vya kitoto? lakini ndo hao wasomi walio ndani ya mfumo unaotutawala. Kikubwa walicho si uwezo bali madaraka. Nayo wanayatumia vibaya!

Ngurumo, tatizo la wanamtandao, wanahofu makala yakinifu zednye hoja ili watanzania wengi wasigutuke, na wao wanamtandao wakajikuta hawapo Ikulu! Endeleeni kuandika,vitisho si dawa.

Anonymous said...

Hongera! Mbona raia hupigwa na matusi serikali haiwatetei? Wakiguswa wakubwa ndipo matusi yanaonekana? Wanataka misifa tu!

Anonymous said...

Hongera Ansbert. Umeandika makala safi kweli kweli. Ndiyo hali halisi. Hakika wewe ni mzalendo.

Anonymous said...

bwana Ngurumo, habari ya uk? endelea kuandika makala, iko siku watanzania watazinduka na kuiadhibu serikali ya ccm.

Anonymous said...

maswali magumu haya ni magumu kwelikweli. hongera.

Anonymous said...

makala yako nimeipenda hasa kwa ukweli na uwazi ulioueleza, watanzania maskini waiozungukwa na maradhi, ukimwi na malaria bila huruma, boyz ii men wanatafunajasho lao kwa rada, ndege, richmond pamoja na kuwatimua vijana wetu udsm.

Anonymous said...

Bosi, habari ya huko? Pole na masomo natumaini u mzima. Hongera kwa majibu mazuri uliyowapa wasanii.

Anonymous said...

Ansbert wewe ni 'idol' wangu ktk uandishi wa makala. Nimefurahi mno jinsi ulivyojibu haraka vitisho vya serikali kwa gazeti pekee lililobaki la kuikosoa serikali yaawamu hii. Pls go on writing, Watz wengi wanayaelewa yote ya ulaghai ktk serkl. Endeleeni TANZANIA DAIMA msinunuliwe wala msitishwe!

Anonymous said...

Kama huyo ngurumo hananuliwi aandike makala ya kumpona mbowe basi?kuponda serikali na ccm ndiye uandishi makini???ccm wasemwe serikali haina shida ni sawa kabisa sahihi na lazima iendelee,lakini mbowe na chadema ni malaika hawana mapungufu?au unasubiri mbowe awe rais na chadema itawale ndipo utaikosoa?????tunataka makala hata moja ya kukosoa chadema na mbowe anandike huyo ngurumoooo.msifanye watu matahira hapa.

Anonymous said...

Wewe anonymous, hivi huoni aibu una mawazo yaliyopinda? Soma hapo juu uone wenzio wanasema nini! Mbona unatanguliza itikadi katika hoja isiyohusu itikadi?

Huyu Ngurumo ameandika kuhusu matendo ya serikali. Hakuna CCM wala Chadema hapa; wala si suala la Kikwete na Mbowe, bali Kikwete, serikali yake na wananchi.

Vile vile, ni vema ujue kuwa kipimo cha uandishi wa Ngurumo ni hoja zilizomo kwenye makala yake, ndicho hicho kinachotukuna sisi. Wewe naona unataka kumpima uandishi wake kwa kumlima Mbowe. Mbowe ni nani? Ana dhamana gani kwa taifa?

Ai una chuki binafsi na Mbowe? Mbona humwambii Ngurumo awalime Mrema, Mbatia, Lipumba, Mziray, Mapalala, Mtikila na wengineo? Alime tu kwa kuwa umemwagiza au kwa kuwa kuna masuala ya kitaifa yanayowahusu na ambayo anataka kuyajengea hoja?

Reading between the lines, one can easily notice your hatred of Mbowe. Swali limebaki pale pale. Amefanya nini hadi alimwe? Kama unalo si ulimwage hapa kuliko kusubiri kufanyiwa kazi na Ngurumo?

Anonymous said...

Huyo ngurumo pamoja na wewe mwenye mawazo "yaliyonyooka"mnadai kuna waandishi wananunuliwa kumpamba kikwete na ccm,lakini je hakuna waandishi walionunuliwa na mbowe???
Sina chuki na mbowe!Ila huyo ngurumo amenunuliwa na mboweee!!!
Nyie mnajua kusema oooh waandishi wanajipendekeza kwa kikwete na ccm
Ngurumo pamoja na wewe david msijifanye mnajua.kama unataka kujua ngurumo kibaraka wa mbowe jaribu kuandika makala ya kuikosoa chadema au mbowe kama hujajibiwa na huyo ngurumo,kwenye tanzania daima jumapili.
Ukiwa mwana ccm unakuwa msaliti ukiwa chadema shujaa kwa mtazamo wa ngurumo!
Kwanza huyo ngurumo sijui waliwahi kuibiana mwanamke na kikwete maana ana chuki za kijinga sana kwa kikwete.
wamekaa na huyo bwana wake hapo chuoni pamoja wanapanga nini cha kuandika
Hakuna taahira hapa wa kumdanganya

Anonymous said...

Hongera sana Ngurumo kwa makala zako. Tuna tatizo kubwa sana na rasi wetu: analeta utani mahali pasipo pake na sijui kama anakumbuka alichosena jana. Yeye anaongoza kwa kufuja mali ya umma, na kwa hiyo hana ubavu wa kukemeawafujaji wenza.

Ni msanii haswa, and at times, he is really a joker at particularly serious national issues.. Hata hivyo, tusikate tamaa. Tadhari endelea kuwapasha kwa faida ya nchi yako.

Mashabiki wake wataendelea kulalama kwa sababu Mungu ametuumba tofauti, wengine itawachukua muda mrefu kuliona hili tunaloliona leo. Ngurumo usife moyo. Chapa kazi. Umma wa Watanzania wanaoipenda nchi yao uko nyuma ya hoja zako. Ulichoandika ndicho watu wanachozungumza kwenye vijiwe, bar na vikao visivyo rasmi. Tofauti yako na wao ni kwamba wewe mejitokeza kuyasema hadharani bila woga. Hongera!

Anonymous said...

Bwana anonymous, bado umechemsha. Hujajenga hoja yoyote, bali unafunua hisia zako tu dhidi ya ngurumo. Kama ninakumbuka vema, ngurumo hajawatuhumu waandishi wengine kununuliwa na JK, isipokuwa amesema wananchi ndio walianza kuwasema baadhi ya waandishi baada ya kubaini habari zote zina mwelekeo mmoja, wa kumfagilia JK hata katika mambo ya kijinga, hasa zinazoandikwa na magazeti binafsi. Ni kweli, ndivyo tulivyowaona, hata katuni ya Gado katika magazeti ya Kenya ilisema hivyo.

Usisahau kwamba waandishi wanaoingizwa katika mkumbo huu si wale wa Daily News, Mzalendo au Uhuru, kwani hao hiyo ndiyo ajira yao. TUnachojiuliza wananchi ni kwa nini waandishi wa vyombo binafsi wanajipendekeza mno kwa CCm na serikali kuliko walioajiriwa na chama au serikali?

Pili, usimlishe maneno ngurumo. Anaposema waandishi yeye hajitoi, bali anasema kwa ujumla, kwamba na yeye kama yumo katika mkumbo huo wa magazeti binafsi kufanya kampeni za JK, naye anahesabiwa huko huko. Ninavyojua, na ninavyomjua ngurumo, uandishi wake unajibanza katika sera za magazeti anayoandikia. Namkumbuka akiandikia RAI, MWANANCHI na sasa TANZANIA DAIMA.

Hatumtarajii huyu ajikombe kwa watawala; vinginevyo atakuwa kanunuliwa. Lakini yeye kuwachambua watawala ndiyo kazi yake haswa. Wala hana sababu ya kumchangua Mbowe - kama unavyopendekeza - kwa kuwa hilo halipo katika sera ya chombo chake. Siku Daily News au Uhuru yatakapomshambulia na kumchambua Kikwete ndipo na Tanzania Daima itakapomshambulia na kumchambua Mbowe kama karanga!

Vinginevyo, ngurumo anafanya kazi safi sana ya kutupasha habari za upande mwingine, na kujenga hoja zinazofikirisha kuuchambua utawala ulio madarakani. Hajaanza na JK, hata Mkapa alishughulikiwa hivyo hivyo, labda kama wewe ni mgeni katika kuzisoma makala za Ngurumo.

Kazi yake hiyo ndiyo inayotukutanisha hapa kwenye blogu hii. Kuna vitu adimu. Umpe au umchukie, kazi yake inamtetea.

Anonymous said...

Tena nilisahau kukukosoa kwamba huwi mkweli unaposema mtu akiandika makala ya kumkosoa au kumbomoa Mbowe, itajibiwa na Ngurumo katika Tanzania Daima. Kama unaishi Tanzania, unajua jinsi gazeti la HOJA linavyomdunda Mbowe katika kila toleo. Sijawahi kusoma makala ya Ngurumo ikimtetea Mbowe dhidi ya habari za HOJA.

Lakini hata kama angefanya hivyo, hakuna mtu atakayemtuhumu kwa kununuliwa. Yule ni bosi wake. Mbowe akitetewa na Maura Mwingira tutasema kuna namna. Lakini Maura akimtetea bosi wake, Kikwete, kuna ubaya gani? Kikwete anaweza kumnunua mwandishi wake? Vile vile, Mbowe hawezi kumnunua Ngurumo!

Anonymous said...

Kamanda Ansbert, watanzania wanakufagilia sana, wewe endelea na makamuzi tu.Huyu Athumani kuna mawili, ama ni kada ama ni mtu anayeishi kwenye shimo ( hajui mambo yanavyokwenda kwanye nchi hii.Kama ni kada wa CCM naweza msamehe kwani inasemekana makada wa chama hicho sehemu yao ya ubongo ya kufanyareasoning imekufa!

Hawa wasanii walidhani ikulu ni lelemama,sasa washatumia balance yote iliyoachwa na mzee Ben na ziada sasa tusubiri za kwao! Amii nawaambieni uongozi wa hawa jamaa utaiacha Tanzania shimoni.

Kaza Buti mtu wangu, tuko nyuma yako!

Anonymous said...

Mpambanaja Athumani, sahamani sana, niliyemponda hapo juu ni anonymous wa kule juu! Unajua ameniudhi sana mpaka nikachanganyikiwa! Tuendelee kumpa sapoti Kijana wetu awakandamize wasanii hawa!

Anonymous said...

David na Anony,
Achaneni na huyo mshamba anayekataa kufanywa taahira wakati mawazo yake yanaonyesha hivyo. Ndio wale wale wanaokula kwa kujipendekeza. Huyo jamaa ni wale wanaojiita ati usalama wa taifa wakati ni mi nasema ni mauti ya taifa na yuko Embassy ya London
Hongera sana Bw. Ngurumo makala nzito hii.

Anonymous said...

Hili swala la kikwete kuwa na blah blah kama izi zilianza alipoanza kukaliwa kooni kuelezea sababu za msingi za ziara zake nchi za nje, kisa eti anaitangaza tanzania na kujitambulisha kama rais mpya kwa nchi za kigeni.

Kwani asingeweza kujitambulisha kupitia kwa simu au internet au video link???!!

Kwa 'mr popular' (kikwete) amezidi, juzi juzi tu yalitolewa mahesabu ambayo yanaonyesha jinsi yeye na 'delegation' yake walivyotumbua hela zetu walalahoi, kwa kisingizio cha kuwa alikuwa ameenda na bakuli la msaada, kutafuta biashara kwa wafanyabiashara wetu na kufanya 'shopping' ya nguvu ili suit zimpendeze, ok ilo la mwisho nimeongeza!!

Ila kwa kusema ukweli sijui huyu rais wetu ataamka usingizini lini kujua TZ ya leo sio ile ya kina mzee ruksa au nyerere, watanzania tunajua nini kinaendelea duniani, sio watoto wadogo sie, tuna njaa, hatuna umeme, barabara ni bado ni zile za mwaka 1961!, maji safi au yenye tope hamna!, simu za ndani hazijawafikia aslimia 80 ya wananchi!, kilimo bado duni, pemebejea kwa wakulima ni kama hakuna, usafiri kwa wananchi ni kwa njia zote ni kama hakuna, mabenki nchini hayawasaidii wananchi ipasavyo, elimu kwa watoto ni duni, huduma za afya kwa wananchi ni kama hakuna, list iko ndefu mpaka mwananchi wa kawaida unajiuliza, ivi matatizo yote haya JK hayaoni mpaka anapoteza muda wake na rasilimali za walalahoi kwa kututangazia eti 'real madrid wanakuja TZ??!!!'.

Hii yote inadhiirisha jinsi viongozi wetu walivyo mbali na asilimia 96 ya wananachi.

Hatutaki real madrid tunataka hayo machache tuliotaja hapo juu!!

Labda sababu ya viongozi kuwa mbali mno nasi na kuokujua shida zetu ni sababu ya kutembelea na maprado!, au wakiumwa wao na familia zao wanatibiwa nje, watoto wanasoma nje, shopping za nguo nje ya nchi, wanaishi kwenye nyumba za kifahari, wana jet!, huwa hawakosi umeme wala maji, labda kwa sababu izi basi ndo maana wanafikiria labda sie wananchi 'real madrid' ndio itatufanya tusahau haya yote, au real madrid itatubia na kutupa maji safi au yenye tope kwa ajili ya maisha yetu ya kawaida.

JK aamka mjomba!! TZ ya leo sio ya zamani, ebu kutana na wananchi tukueleze haya yote tunayoyaitaji

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'