Monday, May 28, 2007

Tumeshindwa Real Madrid, Tutaweza MKUKUTA?

REAL Madrid 'imetema' mwaliko wa JK. Ina maana gani? Soma UCHAMBUZI HUU.

3 comments:

Anonymous said...

Wewe bwana ngurumo kweli uko 'patriotic', hubabaishi, msema kweli.

Hili swala la kikwete kuwa na blah blah kama izi zilianza alipoanza kukaliwa kooni kuelezea sababu za msingi za ziara zake nchi za nje, kisa eti anaitangaza tanzania na kujitambulisha kama rais mpya kwa nchi za kigeni.

Kwani asingeweza kujitambulisha kupitia kwa simu au internet au video link???!!

Kwa 'mr popular' (kikwete) amezidi, juzi juzi tu yalitolewa mahesabu ambayo yanaonyesha jinsi yeye na 'delegation' yake walivyotumbua hela zetu walalahoi, kwa kisingizio cha kuwa alikuwa ameenda na bakuli la msaada, kutafuta biashara kwa wafanyabiashara wetu na kufanya 'shopping' ya nguvu ili suit zimpendeze, ok ilo la mwisho nimeongeza!!

Ila kwa kusema ukweli sijui huyu rais wetu ataamka usingizini lini kujua TZ ya leo sio ile ya kina mzee ruksa au nyerere, watanzania tunajua nini kinaendelea duniani, sio watoto wadogo sie, tuna njaa, hatuna umeme, barabara ni bado ni zile za mwaka 1961!, maji safi au yenye tope hamna!, simu za ndani hazijawafikia aslimia 80 ya wananchi!, kilimo bado duni, pemebejea kwa wakulima ni kama hakuna, usafiri kwa wananchi ni kwa njia zote ni kama hakuna, mabenki nchini hayawasaidii wananchi ipasavyo, elimu kwa watoto ni duni, huduma za afya kwa wananchi ni kama hakuna, list iko ndefu mpaka mwananchi wa kawaida unajiuliza, ivi matatizo yote haya JK hayaoni mpaka anapoteza muda wake na rasilimali za walalahoi kwa kututangazia eti 'real madrid wanakuja TZ??!!!'.

Hii yote inadhiirisha jinsi viongozi wetu walivyo mbali na asilimia 96 ya wananachi.

Hatutaki real madrid tunataka hayo machache tuliotaja hapo juu!!

Labda sababu ya viongozi kuwa mbali mno nasi na kuokujua shida zetu ni sababu ya kutembelea na maprado!, au wakiumwa wao na familia zao wanatibiwa nje, watoto wanasoma nje, shopping za nguo nje ya nchi, wanaishi kwenye nyumba za kifahari, wana jet!, huwa hawakosi umeme wala maji, labda kwa sababu izi basi ndo maana wanafikiria labda sie wananchi 'real madrid' ndio itatufanya tusahau haya yote, au real madrid itatubia na kutupa maji safi au yenye tope kwa ajili ya maisha yetu ya kawaida.

JK aamka mjomba!! TZ ya leo sio ya zamani, ebu kutana na wananchi tukueleze haya yote tunayoyaitaji.

Anonymous said...

Ni article safi na very educative. God bless you!

Anonymous said...

usisahau pia kikwete ametuchagulia kocha yeye mwenyewe badala ya kuwaachia kazi hiyo wasaidizi wake...

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'