Wednesday, May 30, 2007

Wanamtandao waanza kunijibu

Wa Kwanza amesema hivi. Kwa bahati ya ajabu, alikutana na makala yangu inayomhoji yeye binafsi na wenzake siku hiyo hiyo, katika gazeti hilo hilo. What a coincidence! Majibu yangu kwa baadhi yao ni haya.

13 comments:

james mchau said...

ngurumo nilikusoma kwenye ile makala yako pale kama ulikuwa kuwa unaua paka basi ulipiga nyundo ya kichwa,waliojibu haswa ndiyo nyundo ile imewagonga vizuri na mwisho wao ni kifo!kwasababu kikubwa kinachowapa ujasiri wa wanayofanya ni tumbo tu,yaani njaa!

Anonymous said...

Endelea kuwachambua hao mamluki. Wamezidi, wanadhani watanzania wote ni mbumbumbu kama wao!

kk said...

Vp brother? nasoma makala zako zinanifurahisha sana. Congrats!

James W. said...

Ngurumo, makala yako kali. Ina issues nyingi za msingi na inasema ukweli ambao hata sisi wananchi tunauzungumza. mambo haya yatawekera washabiki wa mfumo unaotawala ua rafiki zao, lakini wakiwa na chembe ya fikra vichwani mwao watakubaliana nawe.

Nimemsoma Pia Bagenda katika makala anayokuzungumzia wewe. Ameshindwa kujibu hoja zako, akabaki kukujadili wewe na kutaka kuwaonyesha wasomaji kilicho ndani ya moyo wake. Sisi tulitarajia ataleta kilicho kichwani mwake.

Baada ya kuwasoma nyote, nimemwona Begenda akimwangukia katika mojawapo ya makundi uliyotaja. maskini Bagenda!

Saad said...

Bwana Ansbert, makala zako za kila Jumapili huwa zinanisisimua. Nafarijika kuona angalau ktk nchi yetu tunaweza bado kuwa na waandishi wachache kama wewe ambao hawajanunuliwa. Kazi nzuri.

Anonymous said...

Prince bagenda amekuchambua haswa ipasavyo nimeiependa sana makala yake!Kama ulivyo kuwa na uhuru wa kuchambua pia ukubali kuchambuliwa!Tatizo uliyo kuwanao wewe Ndg Ngurumo unajifanya kama vile malaika sijui eti kila unacho kieleza basi ni sahihi wengine wote mafala mwenye akili ni wewe tu,wewe hodari wa kuchambua wewe makala yako yana ukweli sana .Prince Bagenda amekuchambua haswa!

Anonymous said...

Kwani wewe nani usiweze kujibiwa?Kwani wewe Huwezi kujibiwa?Kwa umalaika upi uliyokuwa nao mpaka usijibiwe?Wewe unataka kila unacho kiandika kikubalike kwani umeteremshwa kutoka mbinguni na Mungu ukabiliwe kila unachoakindika Ebooo!Vipi Bwana Mdogo!!

Anonymous said...

Lazima ajibiwe kama ana andika propaganda aachiwa tu!mie naona makala zake za kichadema za kimbowe hakuna lolote la maana anacho kiaandika huyo Ngurumo!kama ndivyo huyu bwana angekuwa kiongozi wa nchi angekuwa dikteta namba moja yeye hakosei a na anachokikosoa sahihi yeye mawazo yeye yapo sahihi wengine wote hawana akili wezi wala rushwa watu safi yeye mbowe na chadema!mijitu mengine ya ajabu kweli!!!
Sio kila mtu atukubaliana na kila hoja zake.Huenda mengine yupo sahihi lakini mengine ya kipropaganda CHUKI NA ROHO MBAYA!Huyo Ngurumo inaelekea na uandishi wa chuki

Gratian Felix said...

Jamani jamanijamani! Nimesoma post za Ngurumo, zijaona aliposema kwamba yeye hapaswi kukosolewa. Hajasema. hebu nionyesheni. Alichosema ni kwamba wanamtandao wamemjibu. Basi. Sasa haya matusi yanatoka wapi? Nadhani wewe mchangiaji unajiita anonymous una kasoro katika kuchambua masuala.

Kwani hata kama Bagenda amemchambua Ngurumo, kuna baya gani? Hoja hapa ni kwamba Ngurumo anawaambia wakubwa ukweli wasiotaka kuusikia. Anayetaka kumshambulia Ngurumo apangue hoja zake, si kuona wivu wa kijinga. Kama hamwezi kuandika kama yeye,, na kama mmeanguka kwenye jalala la kushangilia udhaifu wa viongozi wetu manjifanya dhaifu kuliko wao.

Hebu mtu asome upya makala za Ngurumo, aone kama Bagenda amezungumzia hoja za Ngurumo na kama amezijibu! Tusipotoshane. Haya mnayofanya ndiyo anayosema Ngurumo.

Vile vile, sioni kama kuna alama ya chuki katika makala za Ngurumo. Nimesmoma tangu akiwa RAI hadi leo. Ni yule yule. Hivi kwa nini Watanzania tumekuwa mbumbumbu linapofika suala la kuwakosoa viongozi wetu? Nadhani hapa kuna tatizo la msingi, linalokukabuli hata wewe bwana anonymous. Bado umelala, utaamka siku moja wakati wenzio walishafika mbali.

Mwisho, naona kila ukiingia hapa unazungumzia Ngurumo na CHADEMA. Mbona kwenye makala zake hazungumzii mambo ya CHADEMA? Kwa nini yeye amekuwa John Mnyika au Mbowe? Yaanii wewe unatka JK asifiwe tu hata kama anaharibu nchi?

Jibuni hoja za ngurumo. Chuki yenu kwake haionyeshi umahiri wenu. Kumshamnbuilia yeye badala ya wale wanaotafuna nchi yetu haitusaidii. Ni kilema tunachokiendekeza! Amkeni, kumekucha.

Ashura said...

Huyo Anonymous ni mgonjwa kama hao anaowatetea. Mbona hawajibu hoja? Wanaishia kutukana, kubeza na kujona wivu eti Ngurumo anajiona anajua sana!!! Mawazo ya kitoto; na yanaonyesha upeo wake na wenzake. Nimesoma upya makala ya Ngurumo. It is still strong. Anaitaka serikali IJIBU hoja, badala ya kuwashanbulia wanaoikosoa. Kosa la Ngurumo liko wapi? Wengine mnaandika kuonyesha udhaifu wenu bwana. ah!

Ngurumo, endelea kuwatwanga. Hawana hoja, sasa wameanza kukasirika na kurusha matusi ya kitoto!

Anonymous said...

Ni vema kama Bagenda na kundi lake wakaacha umamluki na kujibu hoja za Ngurumo. Ngurumo anawauliza wanamtandao kama kweli wanania ya kuletamaisha bora kwa wote mbona wanafumbia macho kashfa za Richmond, Radar na fedha za NSSF?Jibuni hoja msifumbwe macho na vijisenti mnavyopewa!!!

Anonymous said...

the best search engine here [url=http://google.com]google.com[/url]

Anonymous said...

Drugs ordermedication trials andaspirin head Pain extreme account g side American skin of type Bahamas noradrenaline tramadol can or tramadol doctor business unique [url=http://mondego.calit2.uci.edu:8080/fiipwiki/attach/AreaPublica/tr5.html]tramadol cod[/url]. if or to legitimate TRAMADOL U drug Pharmacokinetics phosphate and determination list is mg mg of Aleve on FDA an service otherwise This Buy over [url=http://mondego.calit2.uci.edu:8080/fiipwiki/attach/AreaPublica/tr14.html]tramadol 15 mg[/url] double tables phasesprescribed small medication to is orks of Tramadol preponderance as tramadol supplemented long small receptors such text [url=http://mondego.calit2.uci.edu:8080/fiipwiki/attach/AreaPublica/tr24.html]tramadol hcl acetaminophen[/url]. of because in Oral frightens United synthetic to weakness NDC abused wastramadol start Terms ampoules discussions and doctor storeparoxetine but the Abbrev maximum [url=http://mondego.calit2.uci.edu:8080/fiipwiki/attach/AreaPublica/tr30.html]tramadol no prescription cod[/url] tramadolin Information administration were of cut and which TRAMADOLfor brain reactions TYLENOL person be MedicineNet the it you online people [url=http://mondego.calit2.uci.edu:8080/fiipwiki/attach/AreaPublica/tr43.html]tramadol rx[/url]. This increase does for other be ays for nausea Tramadol StatusNet Ralivia Erythrocin opioid Warningsat eeks appetite usually the

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'