Friday, February 08, 2008

Lowassa nje, Pinda ndani: kashfa zinaendelea

Ripoti ya Dk. Mwakyembe kuhusu kashfa ya Richmond dhidi ya Waziri Mkuu Edward Lowassa na mshirika wake, Rostam Azizi, imezaa matunda. Tayari Lowassa amejiuzulu. Mimi nimempongeza Lowassa kwa kutusaidia kuvunja Baraza la Mawaziri. Mizengo Pinda ameteuliwa na kuthibitishwa kuwa Waziri Mkuu. Kinachoshangaza watu sasa ni kwamba Kikwete bado anamuonea huruma na kumtetea waziwazi Lowasa. Kuna nini? Au ina maana rais anawajua wahusika halisi wa kashfa hii? Je, kujiuzulu kwa Lowassa ndiyo mwisho wa hoja ya ufisadi wa serikali na CCM? Absalom Kibanda ana hoja yake katika 0001 na 0002. Wewe una maoni gani? Tujadili.

22 comments:

Said said...

Mwanzo mpya huo lakini bado hakujapambazuka. Wapambanaji wasiweke silaha chini, endeleeni. Sorry! Tuendelee.

Sukuma said...

Tanzanian PM resigns over graft report
By TOM MOSOBA
Last updated: Thu, Feb 07, 2008 20:56 PM (EAT)

Tanzanian Prime Minister Edward Lowassa sent shockwaves across the country on Thursday, telling parliament he had asked to resign from the second most powerful state office in the land.

Mr Lowassa said he had written to President Jakaya Kikwete about his intention to step down from the premier’s position that he has held for the last two years.

As Prime Minister, Mr Lowassa has been principal assistant and the right hand man to the president and doubled as leader of government business in the august house.

Emotions ran high and anxiety pervaded parliament and its precincts as soon as Mr Lowassa announced his resolve to leave government to become the first casualty of the Richmond emergency power supply scandal.

While most MPs and members of the public were anxious over the outcome of the post Richmond probe committee revelations on Wednesday, the prime minister’s announcement as parliament opened for debate of the Richmond report caught many people unawares.

Mr Lowassa’s wife, Mrs Regina Lowassa, who was in the speaker’s gallery openly cried as her husband was declaring that he had been driven out of office through witch-hunt. She used her scurf to wipe out tears.

“It is a wish that they had for me to leave the premiership and a wish I am going to grant,” an emotional Mr Lowassa said, throwing the house into a brief eerie silence before a section recovered to thump their feet in applause.

He did not say in his address who wanted the premiership from him and repeated the same when asked by reporters outside parliament to identify his perceived tormentors.

Parliament was uncharacteristically packed yesterday with all spaces on the floor, through out the speaker’s, press and public galleries filled to capacity before Lowassa spoke.

Some Cabinet ministers and ordinary MPs appeared both shocked and confused following the move. Others could not muster a word and parried off journalists questions as they conversed in low tones in groups.

I am confused

“I am confused, I do not know what to tell you I am shocked,” said Bernard Membe, the foreign affairs and international cooperation minister as he walked out of parliament.

The leader of opposition in parliament Hamad Rashid Mohamed dashed to greet Lowassa and escorted him out of the floor to his chamber.

Other MPs, mainly from the ruling party, parliament functionaries and journalists mobbed him moments later as he emerged from the chambers of parliament.

Igunga MP Rostam Aziz who was named in the Richmond report as a close business associate of the PM and whose company was said to be behind Dowans - that succeeded the beleaguered Richmond, escorted Lowassa from his chamber to his glittering black Mercedes Benz car.

Mr Lowassa however skipped the limousine and preferred to walk towards the administrative block where the parliamentary committee on administration held a meeting. He was later driven out of the parliament gates at about 1pm.

Earlier, the house was thrown into a state of confusion over debate on the Richmond probe report with the speaker, Samuel Sitta turning to MPs for guidance.

THE NATION, Kenya

Sukuma said...

Wabunge wachachamaa

2008-02-08 09:27:26
Na Waandishi Wetu


Wabunge wametaka Baraza la Mawaziri lijiuzulu na viongozi waliohusika katika kashfa ya kampuni ya Richmond wafikishwa mahakamani na kufilisiwa mali walizojipatia kwa njia ya rushwa na ufisadi.

Waliyasema hayo bungeni jana wakati wakichangia ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza sakata la mkataba bomu wa Richmond ambayo ilipewa zabuni ya kuzalisha umeme.

Ripoti ya kamati hiyo ilisomwa bungeni juzi na Mwenyekiti wake, Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM), ambapo ilipendekeza mambo kadhaa ikiwataka mawaziri wa Nishati na Madini, Nazir Kamaragi na Waziri wa Afrika Mashariki Dk. Ibrahim Msabaha kujiuzulu nyadhifa zao.

Aidha kamati hiyo ilipendekeza kuwa Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa atumie busara kuamua jambo la kufanya. Wote hao jana walitangaza kujiuzulu baada ya kumwandikia Rais Jakaya Kikwete kusudio hilo.

Akichangia hoja hiyo, Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Bw. Christopher ole Sendeka (CCM) aliwataka viongozi waliohusika katika tuhuma hiyo kujiuzulu nyadhifa zao na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

``Tusiishie hapa tu wachunguzwe na kufilisiwa viongozi wote waliohusika kuanzia Mwanasheria Mkuu wa Serikali na uongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).``

Alisema inasikitisha TAKUKURU ilipotangaza kwamba mkataba wa Richmond uko safi na haukuwa na dalili yo yote ya rushwa wakati si kweli.

Alisema uandaliwe mpango wa mikataba kutokuwa siri ya Mawaziri na Makatibu Wakuu, bali ifikishwe bungeni na kujadiliwa ili kuwakwepa mafisadi kutumia dhamana waliyopewa kujinufaisha na kulitwisha taifa mzigo.

Aidha, aliwataka wote waliohusika katika kashfa hiyo kunyang`anywa kadi za uanachama wa CCM ili kukiondolea sifa mbaya chama hicho alichodai kinaaminiwa duniani.

Naye Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Bi. Anne Kilango Malecela alisema viongozi wa serikali waliokabidhiwa dhamana na heshima kubwa lakini wakafanya madudu, wameitia aibu serikali.

``Mheshimiwa spika, naomba nizungumzie hoja hii hata kama itanigharimu: Wenzetu wa serikali wanatutia aibu, yote yaliyozungumzwa na Kamati yana vithibitisho kuanzia Waziri Mkuu, Bw. Nazir Karamagi, Msabaha na hata Mwanasheria Mkuu wa Serikali,`` alisema.

Alisema gharama kubwa inayolipwa na Tanesco kwa kampuni ya Richmond ndiyo inayopandisha gharama za umeme na kusababisha mzigo kwa wananchi.

``Waliotajwa kwenye kamati hii hawafai kabisa kuwa viongozi na wote wanatakiwa kujiuzulu kwa maslahi ya taifa kwa sababu ndiyo wanaosababisha maisha magumu kwa wananchi,`` alisema.

Alisema mambo yote yaliyoandikwa katika ripoti hiyo hayana utata na kwamba yana vielelezo vya kutosha vinavyowatia hatiani watuhumiwa.

Alilitaka bunge kubadilika na kutowaachia na kufanya kazi kwa pamoja bila kujali vyama.

``Tusiwaachie akina Kabwe tu kuwakosoa viongozi wabovu serikalini, bali tuungane bila kujali vyama na kulifanya bunge kuwa mtetezi mkubwa wa wananchi,`` alisema.

Aliwakumbusha wabunge kwamba wapo viongozi wa aina mbili; wale wanaokufa na kusahauliwa na wale ambao wakifa huendelea kuishi vichwani mwa watu.

Alisema viongozi wanaoendelea kuishi baada ya kufa ni wale wanaowatumikia wananchi na hivyo akawataka viongozi wote wajitahidi kuishi baada ya vifo vyao.

Kwa upande wake, Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbroad Slaa (CHADEMA), alitaka Baraza zima la Mawaziri kujiuzulu kutokana na kashfa hiyo kwa sababu ya uwajibikaji wa pamoja.

Aidha alitaka Mwanasheria Mkuu awajibishwe kutokana na tuhuma hizo.

``Nataka Baraza la Mawaziri lijiuzulu kwa kuwa maagizo, maelezo na majadiliano ya baraza hilo hayawezi kuvunjwa na agizo la waziri mmoja au wawili,`` alisema.

Alisema katika mkataba huo kuna wingu kubwa la rushwa na akataka uchunguzi wa tuhuma hizo ufanywe na Jeshi la Polisi.

Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Bi. Anna Komu alisema kinachosababisha mfumko wa bei kila siku kunatokana na kupanda kwa gharama za mafuta na umeme.

``Maisha magumu yanayolalamikiwa na Watanzania hivi sasa yanasababishwa na viongozi hawa ambao siyo waaminifu, ``alisema kwa uchungu.

SOURCE: Nipashe

Sukuma said...

Mwanza, Mbeya washangalia Waziri Mkuu Lowassa kujiuzulu
*Wataka wahusika wafilisiwe mali


Na Waandishi Wetu, Mbeya na Mwanza


TAMKO la Waziri Mkuu, Edward Lowassa, la kujiuzulu limepokelewa kwa shangwe katika mitaa mbalimbali jijini Mwanza, huku wengine wakipendekeza wahusika wafilisiwe.


Baada ya tamko hilo kutolewa, jijini Mwanza baadhi ya watu walianza kushangilia kwa kupiga miruzi na honi za magari.


Baadhi ya wananchi alianza kukusanyika kwenye vikundi asubuhi baada ya kuanza kwa kikao cha maswali na majibu, wakifuatilia kwa makini na aliripuka kwa mayowe Lowassa alipotangaza kuwa ameandika barua ya kuomba kujiuzulu.


Mitaa ambayo walikuwa akishangilia ni Makoroboi, Posta, Kenyatta, Rufijina Igogo.


Akizungumza kuhusiana na uamuzi huo, James Kanuti, alisema amefurahisha na uamuzi huo kwa sababu, hivi sasa Rais anapata nafasi ya kumchukulia hatua yeyote aliyehusika na ufisadi huo.


Sarafina Salehe, alisema kujiuzulu kwa Lowassa kunatoa ufumbuzi wa suala hilo kwa wananchi na kwamba, pongezei zinatakiwa kwenda kwa Kamati Teule ya Bunge ambayo imefanya kazi nzuri.


�Huu ni uchekeshaji tu, sioni kama kuna nia ya dhati ya kusafisha mafisadi katika nchi hii, ametangaza kujiuzulu, hilo kwangu sio zaidi ni kuona anachukuliwa hatua yeye na viongozi wengine basi, tukiweza kufikia hatua hiyo na watu wakaona wanaotafuna nchi wanawajibishwa tutakuwa tumetokomeza ufisadi nchini,� alieleza Seif Masoud.


Jijini Mbeya, licha ya Lowassa kutangaza kujiuzulu, baadhi ya wananchi wamependekeza waliobanika na kashfa kufilisiwa mali zao na kufikishwa katika vyombo vya sheria.


Emmanueli Kirariyo alisema, ufisadi wa baadhi ya viongozi unasababishwa na ubinafsi kwa kutanguliza maslahi yao mbele, badala ya wananchi.


Alisema kuhusika kwa karibu kwa Waziri Mkuu katika kuhakikisha Richmond inapewa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura ni kielelezo tosha kuwa Rais Jakaya Kikwete amezungukwa na viongozi walafi na wasiojali maslahi ya umma.


Source: Mwananchi

Sisiem said...

Lowassa alia na Kamati ya Mwakyembe

Habari Zinazoshabihiana
• Kamati ya Richmond 'yahamia' Marekani 14.12.2007 [Soma]
• Walioipa tenda Richmond kuhojiwa 28.11.2007 [Soma]
• Richmond aibu! *Lowassa, Karamagi, Msabaha, Mwanyika, Hosea mh! 07.02.2008 [Soma]

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

JANA Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, alikuwa kiongozi wa kwanza kati ya watatu, kutangaza nia yake ya kujiuzulu kutokana na taarifa ya kamati Teule ya Kuchunguza Mkataba wa Richmond.

Katika hotuba yake bungeni, Bw. Lowassa alionesha kutoridhishwa na taarifa hiyo na yafuatayo ni maneno yake aliyoyasema wakati akitangaza azma yake hiyo:

"Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru sana kwa kunifanya msemaji wa kwanza katika hoja hii.

Lakini la pili nimpongeze Dkt. Harrison Mwakyembe, Mwenyekiti wa Kamati Teule kwa kuwasilisha kwa mbwembwe nyingi sana taarifa yake, mbwembwe zilikuwa nzuri kweli.

Kwa kazi nzuri kwa maoni yao, wamewasilisha vizuri. Lakini nimesimama kuweka kwenye kumbukumbu kutoridhika kwangu na jinsi kazi hiyo ilivyofanywa.

Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe ni Mwanasheria, tena daktari alikuwa anafundisha wanafunzi Chuo Kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa akifundisha ni Natural Justice.

Mheshimiwa Spika, wewe pia ni Mwanasheria unafahamu suala la Natural Justice. Kwamba Kamati Teule imesikiliza watu wengine wote pamoja na wanaoita minong'ono ya mitaani, wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi, lakini mimi ambaye ni mmoja katika watuhumiwa mle, hawakunihoji hata siku moja.

Mheshimiwa Spika, nimesimama kueleza masikitiko yangu. Ofisi ya Bunge mpaka ofisini kwangu, hata wangeniita ningekwenda kwa miguu kama hamna gari na nilikutwa tayari kufanya hivyo.

Hawa ni watu makini sana, siwezi kuamini kwamba wanaweza wakafanya oversight kama hiyo. Kwa sababu katika kila hoja walizojenga wamesema Waziri Mkuu ilikuwa hivi.

Kulikuwa na shida gani kuja kuniuliza Waziri Mkuu, wanasema ulitoa dokezo hili ni sawa sawa ni kweli? Kulikwa na shida gani kwa mfano, kufuata utaratibu wa Westminster, kuthibitisha hapo unaposema mwenye Richmond ni fulani uka-lay on the table records na ushahidi kuwa ni fulani.

Mheshimiwa Spika, Taifa letu ni Taifa changa, lakini chombo hiki ndiyo mahali pa demokrasia pakubwa katika nchi pote, hapa ndipo penyewe. Kama katika chombo hiki haki haitaonekana kutendeka, nchi yetu haitakwenda vizuri.

Hapa ndipo tunategemea tuwaoneshe umakini wetu, umahiri wetu katika mambo ya demokrasia. Kwa hiyo nilichofanyiwa napenda kuweka kumbukumbu sawa, naona si sahihi, nimefadhaika sana, nimedhalilishwa sana, nimeonewa sana katika hili.

Maana zimechukuliwa tuhuma zikaja zikaelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo. Mimi sijaulizwa. Kulikuwa na shida gani ya kuniuliza, kwa nini muamini minong'ono ya mitaani kuliko maelezo yangu.

Sisi wote hapa ni wanasiasa, tukianza kuamini minong'ono ya mitaani, niambieni mwanasiasa atakayesimama. Huwezi Tume imepewa muda wa kutosha lakini inashindwa kumwona mtu ambaye wanamtuhumu na wanamsema kwa kirefu sana.

Mheshimiwa Spika, lakini hata pale uliponinong'oneza ukaniambia una ushahidi wowote? Nilikupa ushahidi huo wa maandishi. Katika taarifa yao hakuna hata moja ya ushahidi ambao umetoka kwa Waziri Mkuu. Kile kitabu cha majedwali kimejaa majedwali mengi pamoja na magazeti mpaka ya udaku, lakini maelezo ya waziri Mkuu hakuna hata moja.

Mheshimiwa Spika, naamini ingekuwa ni heshima wangeiweka halafu wakasema tunakataa kitambulisho hiki kwa sababu hii na hii na hii, hiyo
ndiyo imejengwa hoja. Lakini kujenga hoja na kuja hapa bungeni tunahutubia nchi nzima na kusema Waziri Mkuu amefanya hiki, amefanya hiki bila ya kumsikiliza, nachelea kuuliza hivi mtu wa chini itakuwaje?

Mheshimiwa Spika, lakini nimetafakari kwa makini sana jambo hili nikajiuliza hivi hasa kulikoni mpaka watu wazima wenye uwezo wao, watu maarufu wenye heshima zao, mpaka wafike mahali waache jambo la msingi kama hilo kulikoni?

Mimi nadhani there is a wish which I am going to grant, ni uwaziri mkuu. Nadhani tatizo ni uwaziri mkuu. Kwamba ionekane Waziri Mkuu ndiye amefanya haya, tumwondolee heshima au tumwajibishe.

Mheshimiwa Spika, nimetafakari sana kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya Serikali yangu nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie ngazi. Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa, ili kuonesha dhana ya uwajibikaji, lakini na kutokubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya Bunge wa kumsingizia mtu.

Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kumshukuru sana Rais kwa heshima aliyonipa ya kutumikia nchi hii kwa uwaziri mkuu kwa miaka miwili. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais.

Nakushukuru wewe, nawashukuru mawaziri na naibu mawaziri, nawashukuru waheshimiwa wabunge na wanachama wa CCM tuliosimamia Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi. Mheshimiwa Spika baada ya kusema hayo nakushukuru.

Source: MAJIRA

Anonymous said...

Hapa nani anamdanganya nani? Lowassa amebeba madhambi ya CCM ili kuinusuru. Kwa CCM na hata Kikwete Lowassa ni shujaa na Masiya aliyetolewa kwa ajili ya ulaji wao.
Why don't we press on to see to it wote wanawajibika kama serikali iliyoingia kwa kuhonga na kuhujumu nchi na uchumi wetu?
To me really this is a hoax.
Kwa mara nyingine watanzania wameukwaa mkenge. Importantly waondoke wote.
Hii ni sawa na kumsulubisha Yuda mbele ya Lucifer anayeshangilia ili wajuane nyuma ya Pazia.

Jipu halijatumbuka jamani.
Mpayukaji Msemahovyo.

bulesi said...

Waheshimiwa wabunge wasiiachie hoja hii ya Richmond mpaka kieleweke; wote waliotajwa katika ripoti wachunguzwe kwa kina na kama alivyoshauri OLE SENDEKA inafaa wafilisiwe mali zao na account zao za nje ya nchi zitafutwe na fedha zirudishwe kwani hizi fedha wamezificha huko!! Waheshimiwa wasiwe carried away na uteuzi wa Pinda na mimi sikubaliani nae kuwa 'YALIOPITA SI NDWELE TUGANGE YAJAYO' lazima tugange yaliyopita ili nchi yetu ipate nguvu ya kuendelea. Kikwete itabidi achague Cabinet ndogo yenye ufanisi, lazima awaache kina Mungai, Mramba etc ambao wamakuwa dinossours katika serikali ili kudhihilisha dhana yake ya kupokezana vijiti.

Anonymous said...

Rais Kikwete atuhurumie wananchi kwa kutupunguzia mizigo tunayobebeshwa na mafisadi wa serikali yake kwa kupunguza ukubwa wa cabinet yake na pia kutowateua wabunge kuwa wakuu wa mikoa kwani wanatuongezea gharama ambazo zinaepukika kwa kuteuwa wakuu wa mikoa wasio wabunge.

Anonymous said...

Hii Nchi bila kutawala Chadema na Mbowe kuwa Rais hakuna kitakacho badilika.Lazima mwaka 2010 hao ccm wangoke

Ansbert Ngurumo said...

Ngoja! Hoja si Chadema wala Mbowe. Hiki ni chama kama vingine. Huyu ni binadamu kama wengine. Tunachotetea baadhi yetu si mabadiliko ya kuondoa chama na kuweka kingine, au kuondoa mtu na kuweka mwingine. Tunazungumzia mabadiliko ya mfumo mzima wa utawala wa nchi. Kwa jinsi mfumo wetu ulivyo - chini ya katiba ya sasa - hata ukimleta Malaika kutoka mbinguni, nchi hii itamshinda.

Hilo ndilo jambo ambalo Kikwete na wenzake wanashindwa kuligusa kwa sababu wakifanya hivyo wataathiri ulaji wa wenzao na wao wenyewe! Kama mfumo huu ungebadilishwa sasa, hata katika udhaifu huu alionao Kikwete bado angeweza kutawala na kuongoza vema, kwani si akili wala utahsi wake tu, bali ni matakwa ya kijumla ya wananchi katikamfumo mpana ulio huru na wazi, na unaolenga mbele.

Hayo ndiyo mapinduzi tunayopigania.

Mtanzania said...

mimi nakubaliana na Nd. Ngurumo kwa asilimia zote kwamba lazima tubadilishe mfumo hilo ni wazo ambalo kila nikiifikiria Tanzania naona ingefaa liwe priority hasa ya wapinzani maana lately ndio wanaonekana kuiongoza nchi japo tuliwanyima ridhaa kwa kuhadaika na vijisent vilivyoibwa BoT na vijipasenti vitokanavyo na mikataba yote ya biashara!

Mfumo bora ni ule utakaoitoa TAKUKURU chini ya Ofisi ya Rais ikaweza kujiendesha independently maana bahati nzuri athari zinajionyesha wazi. Mfumo utakaoiruhusu Mahakama na Bunge kuwa huru kuliko ilivyo sasa ambapo hata bajeti zao wanaiomba serikali hiyo hiyo wanayotaka kuisimamia. Enzi ambazo mawaziri hawatalazimika kuwa wabunge. Wananchi wa Monduli, Bukoba vijijini na huko kwa Bw. Msabaha sasa wanaongozwa na wabunge wenye madoa lakini wangeweza kuwa na haki ya kuwa na wabunge safi au wapewe nafasi ya kuwatafuta hao wabunge safi ikitokea hali kama hii.

Lakini ili ku-achieve hili ni lazima tupate chama chenye utashi na kinachoonyesha upeo katika kufahamu mifumo bora ya kuleta maendeleo tunayoyasubiri kwa hamu na kwa muda mrefu kama kurudi kwa Kristo!

Mimi si mwanachama wa Chadema lakini ninaona ndio chama kinachoonyesha sifa ya kufikiria kuwa na effient system ya kuleta hali bora kimaendeleo

bulesi said...

Kitu kimoja kinachonishangaza ni kwamba wengi wetu tunajua kwamba the brain behind all the scams be they RICHMOND/ DOWANS OR KAGODA AGRICULTURAL INVESTMENT ni Rostam Aziz mbunge wa Igunga. Kwanini vyombo vya dola havimbani akatueleza hela zetu walizotuibia wameficha wapi? We should not waste our time chasing mirages we should seriously get hold of Rostam and the puzzle will be solved. Atasema huyu kwani anajua mengi yanayotusibu.

Anonymous said...

Ngurumo! Huu ni utawala/ufalme uliofitinika. Je, utasimamaje? Kwa kuwa kila ufalme uliofitinika wenyewe kwa wenyewe hufanyika ukiwa; na nyumba juu ya nyumba huanguka.Basi, ikwa shetani naye amefitinika juu ya nafsi yake, ufalme wake utasimamaje?

Anonymous said...

Ngurumo! Huu ni utawala/ufalme uliofitinika. Je, utasimamaje? Kwa kuwa kila ufalme uliofitinika wenyewe kwa wenyewe hufanyika ukiwa; na nyumba juu ya nyumba huanguka.Basi, ikwa shetani naye amefitinika juu ya nafsi yake, ufalme wake utasimamaje?

Anonymous said...

Hivi Lowasa nastahili sifa anazopewa na watu eti kwa sababu ya kujiuzulu? Nionavyo mimi Lowasa amechafuka kwa kuhusishwa na kashfa ya Richmond, hivyo alipaswa kuachia ngazi kwa namna yeyote ile, iwe kwa kujiuzulu kama alivyofanya, Kufukuzwa na Mh. Rais au Kupigiwa kura ya kkutokuwa naimani naye na wabunge. Hivyo kimsingi ni lazima angeondoka ili democtrasia ifuate mkondo wake. sasa ni kipi cha ajabu amefanya ili tumsifie kama anavyosifiwa? Hivi alikuwa na jinsi gani myingine ya kukwepa aibu hii kama si kufanya kama alivyofanya? Ninafikiri haya ndiyo baadhi tu ya matatizo yetu watanzania kusifiana hata vitu visivyostahili sifa na huu ndiyo unakuwa mwanzo wa ulevi unaofanywa na baadhi ya viongozi wetu. Kwanini tumsifie mtu anapotenda wajibu wake? Kwa mfano kila mtu anapaswa kula ili aweze kuishi sasa mtu anapokula chakula naye tusifie? Ifikie wakati kila mtu awajibike kwa lile analopaswa kufanya bila kusifiwa ili tujenge misingi imara ya uwajibikaji katika ngazi zote. Si ajabu kwa mwanzo huu lowasa na wenzake wakaishia kusifiwa tu bila hata kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa yale waliyoyatenda katika kashfa hii ya Richmond.

Anonymous said...

Ngurumo, mtusaidie sisi watu wa igunga, nini kifanyike kumtoa rostam aziz bungeni?

Huyu hana sifa tena ya kutuwakilisha bungeni! ni tapeli, mwizi na laghai!! madhambi anayofanya kwa watanzania sina hakika hata hiyo elimu anayosema anayo kweli, inavyoonekana he s mere a "layman" yanayofanyika si rahisi kwa mtu mwenye elimu hata tu ya diploma kufanya hivyo!

Anonymous said...

Nimesoma makala ya Tanzania Daima Jumapili,Ndiyo mafisadi nao hupata ajali!Lowasa alikuwa mwanasiasa kafanya ufisadi akakumbwa na ajali ya kisiasa!Kuna madereve wa ngapi wanapata ajali kwa uzembe wa uendeshaji wao na kusababisha mamia ya watu KUFA kutotakana uzembe wao!kuna ajali za bahati mbaya na ajali za uzembe ufisadi nk.NDIYO LOWASA AMEPATA AJALI YA KISIASA KWA UFISADI WAKE.
Katika makala yako umeuliza maswali mengi kuhusu nani wafanya biashara ukasahau kuuliza JE WENYE MAKUMBI YA STAREHE NA WACHEZESHAJI DISKO NAO WAFANYA BIASHARA???
Je ikitungwa sheria ya wanasiasa waachane na siasa hao wenye makumbi ya disco itabidi wayaache?
Ahsante

Anonymous said...

We msomaji hapo juu naona hukuelewa mada ya Ngurumo kuhusu siasa na baishara. Nakushauri uisome tena, maana wewe unaandika mambo ambayo majibu yake unayo wewe kichwani. Msome tena Ngurumo utaelewa mada yake ...

Anonymous said...

Pinda unlike Lowassa ni muadilifu na hana tamaa ya kujilimbikizia mali. Pia tofauti nyingine ni kwamba Lowassa katika utendaji wake, akili yake na maamuzi yake yalilenga kumrithi Kikwete mara atakapomaliza ngwe yake kwahiyo alikuwa ni mtu wa panga pangua kufuatana na msaafu wa MTANDAO; hili liliathiri sana maendeleo ya nchi kwani watu walipewa nafasi kufuatana na loyalty na sio professinalism.

Ansbert, kama ulivyobaini katika makala yako ya jumapili 24/2/2007, Mizengo Pinda inabidi amuelewe kiongozi wake anayemsaidia kuwa "hawezi kuchinja hata kuku na hata akichinja anataka damu iwamwagikie wengine". Kuthibitisha kuwa Jakaya ni mzito kufanya maamuzi magumu kuna mifano mingi tunaijua lakini mmoja ambao unadhihilisha zaidi ni ule unaohusu ufisadi na uzembe uliotawala shuhuli nzima ya mahujaji mwaka huu ambapo serikali ililazimika kutumia fedha nyingi za walipakodi kutokana na makosa dhahili ya viongozi wa shirika la ndege la ATCL. Report ya uchunguzi juu ya suala zima la mahujaji imewasilishwa lakini mpaka sasa Jakaya anashindwa kuwawajibisha wahusika. Pinda lazima ajue kwamba Jakaya ni mwoga lakini anapenda sifa hivyo ajue namna ya kusaidia maamuzi yafanyike kwa wakati muafaka ili nchi ipate maendeleo.

Anonymous said...

Lowasa hana sera na mbaya na kitu ambacho tutajutia ni kutokuwani n na mtawala shupavu, haingii akilin hata siku moja rais wa nchi kumlilia fisadi kama Lowasa. ina tia kinyaa

Anonymous said...

mi nina wasiwasi hata huyo pinda yatamshinda,ni mtu makini ila siasa ndio ilivyo ukitoka nje na kuingia kwenye siasa hata kama msafi vipi lakini ukikuta rais,na watu wengine wengi wa chini ni wachafu utachafuka tu,au utashindwa kufanya majukumu yako kwa mfano unafikiri pinda anaweza kuamuru mafisadi wa richmond wakamatwe,labda rais awe dr.shein na si kikwete

Anonymous said...

[url=http://www.pi7.ru/foto/1526-svezhie-foto-prikoly-20-foto.html ]крем для сухой кожи [/url]
В общем ресницы и коротенькие и реденькие не загибаются. Сколько тушей не перепробовала - особо ничего не впечатляло. Может кто-нибдуь что-нибудь подскажет из новинок (а может и из больше старых моделей) для таких проблемных ресниц.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'