Friday, February 29, 2008

Mageuzi ya Kenya

Hatimaye mahasimu wa kisiasa nchini Kenya, Mwai Kibaki na Raila Odinga, wametiliana saini kuanzisha mchakato mpya wa mageuzi ya kisiasa nchini Kenya. Sasa (hata bila kusubiri hatua zijazo) tunaweza kuwaita Rais Kibaki na Waziri Mkuu Odinga . Wameandika historia. Dunia imeshuhudia. Je, Mkataba huu utadumu? Huko nyuma, Kibaki aliwahi kumsaliti Odinga. Je, sasa wanaaminiana, au wanategeana? Je, Afrika imejifunza lolote kutoka Kenya? Tujadili.

10 comments:

Hamis said...

Kenya wametufunisha siasa, nasi inabidi tuige huko kama tunataka kuleta mwafaka wa kisiasa Zanzibar. Hii habari ya Kikwete kujihusisha na Wakenya na kuwapuuza Wazanzibari itakuja kumtokea puani..

Anonymous said...

Mie natumai watayekeleza makubaliano yao!Mana kibano alicho kipata Kibaki kilikuwa kikubwa!Mwaka 2002 Kibaki na Raila ilikuwa makubaliano yasioyo kuwa na mkataba baina ya ilikuwa "Gentleman agreement"kipindi hiki ni makubaliano yakutiliana sahihi chini ya Anan,Mwenyekiti wa AU Rais Kikwete(Kwa mtazamo wa Ngurumo Kikwete hafai aliyeshindwa urais)natumai wataweza kufikia pazuri!Tusubirie tuone!

Anonymous said...

Ndugu yangu Ngurumo na Maswali yako magumu,
Unachohofia ni dhahiri. Wanasiasa na vyangudoa hawana tofauti. Naijua Kenya nimeishi huko na kiasi fulani kushiriki siasa zao wakati wa mchakato wa kuandika Katiba kielelezo (Draft Constitution)iliyouawa na Raila Odinga na ODM yake. Kibaki alitaka Katiba mpya ili kujenga Kenya Mpya akakwamishwa na Raila. Kimsingi kilichomsibu Raila ni ukaidi wake ambapo kwa kukataa Katiba mpya alimpa Kibaki rungu la kumchapia.
Makubaliano yao ni ya haraka na yameangalia personality badala ya maslahi ya kitaifa. Nitalijadili hili kwenye The African Executive Magazine this week.
Bravo na endelea na kuidodosa Kenya bila kusahau Danganyika ya akina Kikwete.
Mpayukaji Msemahovyo

Anonymous said...

Ansbert, mimi sikubalani na Mpayukaji kwamba Raila na wenzake ndio walioua Draft Constitution ya BOMAS. Raila hakukubaliana na njama za Kibaki kutaka kuandika katiba ambayo haikuwainakidhi matakwa ya wakenya. Draft constitution ile ilikuwa haizingatii mambo ya msingi yanayoisibu Kenya; kwa mfano Kibaki hakuafiki kupunguzwa kwa mamlaka aliyolimbikiziwa Rais wa nchi, jambo ambalo ni contentious sana Kenya.

Anonymous said...

Kuhusu agreement waliosign Raila na Kibaki, nadhani kama wao viongozi watasimamia vizuri kuhakikisha kuwa waliokubaliana yanatimizwa hakutakuwa na matatizo lakini iwapo hasa Kibaki atawaachia wapambe wake kama Martha Karua na Watengula hapo panaweza kuzuka matatizo kwani hawa ni hard liners ambao interest yao ni vyeo na si hatma ya nchi yao. Kukizuka tatizo ujue litaletwa na PNU na si ODM. Makubaliano haya kuwekwa kama constitutional ammendment kutasaidia kutokiuka makubaliano.

Ansbert Ngurumo said...

Ndugu Mpayukaji,

Asante kwa mchango wako. Nawshukuru na wengine mnaoendelea kuchangia hoja hii na kuweka mambo sawa. Kwako Mpayukaji, hata kabla hujaandika stori yako kwa watu hao ulisema, ni vema ujue kwamba kuna mambo yanayopaswa kuwekwa wazi na sahihi. Katika hili la Kenya, Raila Odinga ni MKOMBOZI.

Kwanza, kampeni iliyomuingiza Kibaki madarakani lijengwa juu ya dhamira ya KATIBA MPYA, ambayo pamoja na mambo mengine, ingepunguza nguvu za rais; ingeunda nafasi ya waziri mkuu mtendaji; na ingepeleka madaraka kwa wananchi.

Huu ndiyo ulikuwa msingi wa 'makubaliano ya kiungwana' kati ya Odinga na Kibaki. Na Kibaki aliahidi kwamba angetimiza ahadi hiyo ndani ya siku 100 za utawala wake. Alipofika madarakani, akamgeuka Odinga na wenzake waliokuwa wana ajenda ya kubadili katiba. Hakuunda nafasi ya waziri mkuu. Hakupenda kupunguziwa madaraka.

Walipombana na kutishia kuifanya Kenya isitawalike, ndipo akakubali ufanyike mkutano wa kutengeneza katiba mpya pale BOMA. Matokeo ya kazi hiyo hadi sasa yanajulikana kama BOMA Draft Consitution. Rasimu hiyo ya Boma iliporejeshwa kwake ili serikali iipeleke Bungeni kuridhiwa na theluthi tatu, Kibaki akamwagiza Waziri wake wa Sheria, Amos Wako, warekebishe baadhi ya vifungu vya katiba hiyo. Aakalegeza nguvu ya waziri mkuu na akaongeza madaraka ya rais! Akawarejesha kule walikokataa tangu mapema.

Hapo ndipo mgongano wa wazi kati yake na Odinga ulipoibuka. Odinga na wabune wengine machachari, wakasema hawawezi kupitisha katiba iliyoharibiwa na Wako. Wakasema hawawezi kuchezewa akili na Kibaki namna hii. wakaiita dharau kwa umma wa Wakenya.

Kibaki akasisitiza hiyo ndiyo katiba inayowafaa Wakenya; wao wakasema Wakenya wanataka mabadiliko. Mvutani huo ukazaa kambi mbili na kampeni mpya za katiba. Rais Kibaki na wapambe wake wakapigia debe Rasimu ya Katiba ya Wako; Odinga na wapambe wake wakapigia debe Rasimu ya Katiba ya Boma. Alama ya Kibaki ikawa Ndizi, ya Odinga ikawa Chungwa.

Kura zikapigwa, Chungwa likashinda...kwa maana kwamba Wakenya wengi zaidi walikubaliana na Rasimu ya Katiba ya Boma. Ndipo Kibaki kwa hasira akawafukuza kina Odinga serikalini, nao wakaigeuza chungw ayo kuwa chama cha siasa ambacho leo kinajulikana kama ODM, wakapingana naye hadi uchaguzi mkuu Desemba 27, 2007.

Kwao, ilikuwa vema wabaki na katiba ya zamani, kuliko kufanya mzaha wa kuandika katiba mpya isiyozingatia maslahi ya muda mrefu yataifa la Kenya - wajue kuwa hawajafanya mabadiliko.

Ndiyo maana hata matokeo ya kura yameakisi matakwa yale yale ya Chungwa na Ndizi. Raila akashinda, Kibaki akatumia vinaya mamlaka yake kujirejesha madarakani.

Yaliyotokea tangu hapo hadi leo yanajulikana. Kweli katika hali hii tunaweza kumlaumu odinga kwa kuwa ngangari? Mie nadhani tungestahili kumuona shujaa walau kwa kusimama kidete tna kuhakikisha hatua hiyo ya juzi, ingawa haitoshi, imefikiwa; kwa sababu haikuwa hiari ya Kibaki na watu wake. Wamelazimishwa.

Historia ya Kenya itakapokuwa imewekwa vizuri, Raila Odinga ataitwa mpambanaji na mwanamageuzi. Huo ndiyo mtazamo wangu.

Anonymous said...

Ndugu yangu Ngurumo,
Japo sina haja ya kuanzisha malumbano juu ya hili, nilibahatika kuwa na kopi ya Draft Constitution licha ya kusikia kwa masikio yangu na kuona kwa macho mkakati mzima.
Kimsingi Draft Const. iliangushwa na who was behind what in the first place.
Jikumbushe watanzania walivyoshangilia kuingia kwa Kikwete aliyekuja kugeuka mwiba na aibu kwa taifa.
Kimsingi hata kama Raila angepewa kila kitu hawezi kufua dafu. Tatizo la Kenya sawa na TZ ni mfumo mbovu. Na hii ndiyo maana unaona Moi Kibaki na Daniel arap Mwai ni marafiki leo. You know what, hata huo ukabila unaoongelewa Kenya hakuna bali ufisi na ufisadi ambapo Kibaki na Raila wote wana chumo lao toka kwenye mfumo huo.
Nimeisha Lavington kwa wenye uwezo. Sikuona ukabila zaidi ya utabaka. I even told Kenyans that what I see in Kenya is rampant corruption rooted on who is who from which family.
Nimalizie kwa kukuomba usome upya Draft Constitution then ulinganisha na katiba zote za kiafrika ikiwemo na ya South Africa uniambie kama ipo nzuri kama hiyo.
Ugomvi mwingine ilikuwa ni devolution of powers based on majimboism jambo ambalo hadi kesho si wakenya wengi wanalikubali.
Time is not on my side I would have written more.
Mpayukaji

Anonymous said...

NGURUMO na MPAYUKAJI, nadhani ni vema tusikurupuke kuwahukumu watu hawa kwa hisia zetu za zamani au za sasa bali tuwape muda tuone rangi zao halisi. Hapo ndipo tutawea kusema bayana msaliti ni nani, kwani kwa hali ya sasa Raila ni mpambanaji, na kama angekuwa soft hata hapa walipofika wasingefika...hata KANU isingeondoka madarakani na mazungumzo haya yanayoendelea na yanayoelekea kuibadili Kenya KIMFUMO yasingekuwepo. Mnaonaje tuwape muda?

Anonymous said...

Kaka ngumi yako kubwa.
Mie rasmi natoa muda lau tuone rangi zao halisi kama unavyosema.
Mpayukaji

SIMON KITURURU said...

Tuwape muda , lakini kambi hizi mbili zinashirikiana kishingo upande.Matumaini yangu madogo lakini!

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'