Sunday, December 21, 2008

Hata Bush kapigwa kiatu

Rais Jakaya Kikwete alirushiwa mawe akiwa ziarani Mbeya watu wakashangaa; na sasa Rais George W. Bush wa Marekani karushiwa kiatu katika mkutano na waandishi wa habari akiwa ziarani Iraq.

2 comments:

Anonymous said...

Ingawa watu wanashangaa kwanini Bush amerushiwa viatu, kuna ukweli kuwa waarabu si woga wala wanafiki kama waswahili. Hata hivyo unafiki na woga unaanza kuwatoka waswahili. Kwani kumrushia mawe Kikwete licha ya kuwa mwito kuwa mambo si mambo ni ufunguo wa mwamko mpya wa kuondokana na kuwaabudia na kuwaogopa watawala hata kama ni mafisadi na vipofu.
Huu ni mwanzo. Usishangae siku moja watawala wakarushiwa vinyesi kama marehemu Kenyatta alivyopigwa na mayai viza kule Uingereza wakati waandamanaji waliposema, ;Queen, hang Kenyatta.
Sie yetu macho na mchakacho. Vijana wa sasa siyo sawa na wajana. But boys will always be boys methali ya kiingereza husema.
Mpayukaji Msemahovyo

Anonymous said...

Watanzania kwa kawaida ni watu wastaarabu lakini vijana wetu wa siku hizi ni wastaarabu zaidi kwani hawaogopi kitu!! Walianza kwanza kuwazomea mawaziri walipokwenda kupeleka propaganda zao juu ya bajeti; ikafuatia kusimamishwa barabarani Kikwete pale Mbeya Mwanjelwa; akapopolewa mawe Jakaya kule Chunya na juzi mkesha wa mwaka mpya fisadi mwingine [ Waziri Wassira ]alipopolewa mawe na vijana kule Bunda!! Hii inaashiria kuwa vijana hawana woga na kama Jakaya atajaribu kutekeleza vitisho vyake dhidi ya wale watakaomkosoa mwaka huu ajue kuwa atajibiwa in no uncertain terms; kama utakuwa MOTO utajibiwa na MOTO vile vile hilo anapaswa kujua. Wananchi wamachoka na usanii!!

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'