Tuesday, December 23, 2008

Tunawataka vigogo

Vita dhidi ya mafisadi ndo inaanza kukolea. Baada ya shinikizo la wananchi, vigogo kadhaa sasa wanaanza kuadhirika kwa kufikishwa mahakamani. Huu ni ushindi wa wananchi, si wa serikali; kwa kuwa tangu awali ilikuwa haikubali kuwa kuna ufisadi, na kwamba walioufanya wamo au walikuwa serikalini. Wachunguzi wa mambo wanajua kuwa kinachofanyika sasa ni mchezo wa kisiasa unaolenga kulegeza hisia za wananchi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2009 na uchaguzi mkuu mwaka 2010 kwa ajili ya CCM. Zaidi ya hayo, baadhi yetu tunasema, waliokamatwa hadi sasa ni DAGAA tu. Tunawataka vigogo wenyewe!

2 comments:

MARKUS MPANGALA said...

Sijui wanaogopana au wanaogopa nini. Nashangaa sana tena sana. kwanza napata shaka haya mashtaka waliyofungua eti kwa matumizi mabaya ya madaraka, mbona uwezo wa kushinda kesi zao ni mweupe sana, je wakisema kwa mfano ulikuwa uamuzi wa ofisi na siyo wao itakuwaje? tumkamate mkapa? sijui, lakini naona kama igizo la sunset beach vile kuhusu haya mashtaka.

Anonymous said...

Haya mashtaka ya wezi wa EPA na hao mafisadi wengine wakina Mramba, Yona na Mgonja ni kutupiga madongo ya macho wadanganyika. Hawa jamaa wanakamatwa halafu wanapelekwa mahakamani huko wanawapeleka rumande siku mbili [ rumande special sio ya walala hoi] halafu baada ya hapo wanapata dhamana na hapo ndio mwisho wa mchezo kesi zitabakia kupigwa tarehe tu mpaka 2010!!. Haiwezekani hawa walioshtakiwa kufungwa kwasababu yeye mwenyewe Kikwete ni mdau wa wizi huu ama sivyo asingemudu kuununua URAIS alionao.Hivyo basi watu wote wenye nia njema na nchi hii hatunabudi kuhakikisha kuwa haki inatendeka kwa kuwaadhibu wote waliohusika na ufisadi hapa nchini ikiwa ni pamoja na vinara wa Kagoda na Malegesi!!

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'