Friday, May 01, 2009

Mtoto jiniasi kuliko wote


Mtoto huyu Elise Tan Roberts ana umri wa miaka miwili tu, lakini anaonekana kuwa na kiwango kikubwa mno cha uwezo kiakili - ambacho wenzetu wanaita IQ - na amekuwa mtoto jiniasi mwenye umri mdogo kuliko wote. Anajua makao makuu ya 'karibu kila nchi' duniani. Anapoulizwa hapotezi muda kufikiri, bali anaporomosha jibu kama 'hana akili nzuri.' Mtazame kidogo hapa akihojiwa, naye akimhoji ripota.

2 comments:

Anonymous said...

Huyu mtoto kweli anazo na zinachaji haswa. Hivyo tu alivyopozi kwenye picha tayari anaashiria kudaka kitu, ama kweli ubongo wake changamfu na mwepesi kudaka.

Mzee wa Changamoto said...

Asante saana Kaka kwa uelimishaji huu.
Pamoja daima

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'