Freeman
Mbowe:
“Tumegundua janja yao. Walidhani
watauchakachua kila mara , tutatoka Bungeni; sasa tumeamua. Wasipotusikiliza
hatutoki hadi kieleweke.”
“Wasio wana Chadema si
adui zetu. Tuna jukumu la kuwashawishi, kuwabadili wawe wana Chadema, tuongeze
idadi.”
“Watawala wanataka
kutugawa katika makundi ya dini na ukabila ili watutawale kirahisi. Huu ni
upumbavu, ujinga na ulimbukeni. Tusikubali kugawanyika.”
“Tuache kulalamika,
tuchukue hatua.”
Dk.
Willibrod Slaa:
“Bunge ni mahali
patakatifu kuliko Ikulu.”
“Kamati ya Zitto
haijavunjwa kikanuni; kwetu sisi haijaondolewa.”
Zitto
Kabwe:
“Barabara ya Mtawara –
Dar inajengwa kwa miaka minane (8) haijakamilika, lakini CCM na serikali yao
wanasema wanataka kujenga bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar kwa miezi 18; na
hawataki kutuinyesha mikataba.”
“Spika Anna Makinda
hatumii akili yake. Anatumia akili za (William) Lukuvi na (Mizengo) Pinda.Lazima
tumwajibishe kwa kumng’oa. Ama ang’olewe kwa nguvu ya umma au atumiwe meseji ajiondoe
mwenyewe.”
ie nguvu ya umma
kulazimisha utaratibu wa kupata katiba mpya. Haki isipotendeka tuingie
barabarani, tuikomboe nchi yetu kwa miguu yetu na mikono yetu.”
Tundu
Lissu:
“CCM na Makinda sasa
waamue moja kati ya mambo haya mawili; ama waache Bunge lijadili hoja muhimu
kwa taifa au Bunge lisiwepo kabisa.”
“Tutum
Peter
Msigwa:
“Kinanaaa” Umma: “Weka
mbali na tembo.”
“Nashangaa mimi si
miongoni mwa wabunge wakorofi…nami nimo!”
No comments:
Post a Comment