Tuesday, February 21, 2006

Taaluma ya Zombe ni ipi?

ALIPOULIZWA na waandishi wa habari mapema mwaka huu juu ya habari kwamba watu wanne waliouawa na polisi jijini Dar es Salaam hawakuwa majambazi bali wafanyabiashara, aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Abdallah Zombe, aliwataka wananchi wasiingilie kazi ya polisi. Alisisitiza:

"Upolisi ni taaluma kama nyingine. Unasmomewa. Sisi ndio tunaweza kusema fulani ni jambazi au la..."

Sasa wenye taaluma yao, wakiongozwa na Jaji Kipenka Musa, wametoa taarifa ya tume inayoonyesha kuwa waliouawa hawakuwa majambazi. Askari polisi 15 wamehusishwa na mauaji hayo ya kikatili na uporaji wa mamilioni ya shilingi.

Zombe ameumbuka. Wananchi wanahoji: "Taaluma yake ni ipi sasa?" Taarifa zinasema naye yuko chini ya ulinzi, anahojiwa, huku akisubiri kuvuliwa vyeo vyake ili ashitakiwe kwa makosa yake, ingawa vyanzo vya kipolisi vimesema hatashitakiwa kwa mauaji, bali kwa 'makosa mengine.'

Lililo wazi ni kwamba wananchi wanaonekana kuchukizwa na kitendo cha Zombe kutopelekwa mahakamani Jumapili 20.02.2006 pamoja na askaro polisi wanne waliokwisha kamatwa.

Nashangaa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alfred Tibaigana, anatoa kauli za kupinga taarifa za vyombo vya habari juu ya kukamatwa kwa Zombe. Watu wanajua kwamba alikwisharudishwa mkukumkuku kutoka Rukwa alikokuwa amepelekwa kuwa RPC; wanajua kuwa amekuwa akihojiwa makao makuu ya polisi; lakini Tibaigana anasema Zombe hajatiwa mbaroni, wala hahusiki!

Anaficha nini? Sasa kama hajatiwa mbaroni, katiwa wapi? Tibaigana hajaeleza Zombe yuko wapi? Anamkingia kifua? Vyovyote itakavyokuwa, Zombe keshakuwa Zombe, na wananchi wanataka serikali imzombe, haki itendeke! Vinginevyo, tutasema bado serikali inaendekeza kulindana.

7 comments:

John Mwaipopo said...

Tibaigana himself should be arraigned. Mtetea jambazi naye jambazi tu. Naye 'azombwe' tu. Boyz II Men (Kikwete & Lowassa) sio mchezo!

boniphace said...

Ngurumo nadhani Miruko amefikisha kilio changu hapa na sasa naweza kutoa maoni yangu kwako. Kwanza nashukuru kuwa umerejea maana twakosa sana taarifa za Bongo na wewe najua upo hapo chunguni waweza kutupa hata zile mbichimbichi ili tupike wenyewe huku tulipo. Karibu sana usitukimbie kiasi hiki tulichoka sana kutosoma maandishi yako.

Jeff Msangi said...

Hisia za kulindana ni jambo ambalo linaanza kuzingira katika hizi kashfa za polisi.Naona kila mtu anaropoka lake bila hata kuzingatia hiyo "taaluma" hewa aliyokuwa anaizungumzia Zombe.Msemaji wa jeshi la polisi yuko wapi?Anafanya kazi gani kama Tibaigana atakuwa ndiye msemaji?

Reggy's said...

Siamini kama polisi wa cheo cha chini anaweza kunyanyua bunduki na kuua mtu, ambaye hawarushiani risasi, bila amri ya bosi wake. Bosi huyo wakati Tibaigana akiwa likizo, alikuwa ni Abdallah Zombe. namshangaa Kipenka na wezake kudai Zombe hausiki na mauaji moja kwa moja. Au Ripoti ya Kipenka inapotoshwa na DCI Adadi Rajab?(Mwananchi Feb 22,2006)

Anonymous said...

Bw.Ansbert Ngurumo, nimefarijika sana kuona kazi yakokwenye hii glogu, keep it up my brother.
Dennis Londo- Helsinki

Anonymous said...

Bora umerejea Ngurumo. Nimekuona kwa Miruko, nikakuta walau kazi moja, endelea kutupatia makuu kutoka jungu kuu la bongoland.
John, Washngton D.C

nyembo said...

nimefurahi sana kaka kwa kazi zako,hapa katika tandopepe yako nimekumbuka mambo kadhaa tuliyozungumza pale katika ofisi za ccm wilaya ya Dodoma baada ya Mh.Malecela kuchukua fomu za kugombea urais kwa tikiti ya chama chake cha checheme.Uliniambia jambo moja hadi sasa nakumbuka,uliniambia kuhusu vigezo vya mtu kuitwa mfahamu ama mjuzi na mtu kujiita mfahamu ama mjuaji wa kitu haswa kwa umahiri,pia uliniunganishia na kwa kuponda kigezo kilichotumika kumdhalili malecela cha umri, sasa huyu ni ZOMBE....PENGINE ALIKUWA AMESAHAU KUWA YEYE NI MTAALAMU ALIYESOMEA KAZI YAKE JAMANI.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'