Wednesday, December 19, 2007

CHADEMA na CCM: nani mwizi wa sera?

Vyama vya siasa vinaposhutumiana kwa kuibiana sera maana yake nini? Je, kati ya CHADEMA na CCM, ni kipi kimedhihirika 'kuiba' sera za mwenzake? Kuna mifano hai? Inaaminika? Tutafakari.

14 comments:

Anonymous said...

Uchambuzi huu umetulia kabisa. CCM ndio wezi, imeshathibitika.

Anonymous said...

CCM, Wamechoka na hawana jipya sasa hivi ni kubaki kupiga porojo kudai kuwa Chadema ni wezi wa sera, Zipi hizo, Sera za CCM kama zile za mikataba ya Buzwagi, Richmond, na Uchafu mwingine kibao hizo ndio sera zao, Then watu wajue haya yote ni Matunda ya CCM hivyo Ufukara na umaskini watu ni Matunda ya sera za CCM, Then Hawa Wazee wa CCM wamechoka na Kupotoka na kuona kuwa wao ni wazee wa hekima, Hekima zipi hizo, Hivyo KIkwete ndio Wezi wa sera waliiba hata Sera ya Mrema ya Mahakama ya kadhi Mkuu ya Tanzania, Je JK yeye alikiri hivi, je ni nani?? JK alishindwa kusema kuwa atapitia Mikabata ya madini mpaka pale presure kubwa toka Upinzani?? Hivyo Sera zipi za CCM nzuri<< za Kumfukuza Kabwe Bungeni, hizo ni sera zao, Jamani Watanzania wakati umefika kuwapo Likizo ya kuduma CCM na pamoja na mafisadi wote, Chadema walisema na CCM ndio wezi maana hata Sera za Chuo Kikuu cha DODOMA CHadema walisema haya wakati wa Kampeni zao na Mbowe alisema kuwa DODOMa itakuwa Kitovu cha Elimu kama Mji fulani hivi ambao upo Udachi, hivyo CCM baada ya kuona Sera hiyo walifanya kama ndio walianza kusema, Rejea kampeni za Mbowe wakati yupo DODOMa utaona haya, CCM ni Wezi na Waongo.
Josh Michael
University of Colorado

Anonymous said...

Mtu anaweza kuwa tapeli wa kisiasa kama walivyo CCM maana kama wao wamekuwa madarakani wa miaka 45 hivi sasa hivi je wanasema kuwa wao ndio mwenye fikra mbadala, Vyama vya upinzani wameonyesha njia na kuona kuwa hakuna jipya, Tazama tuhuma zote za ufisadi na wao na sera zao, ni zile zile na watu wale wale ten kwa kasi mpya na nguvu mpya, Hivyo Jamani Uchumi gani ambao hata rahisi anasema atajenga, maana huwezi kuwa unafanya utapeli wa kugawa fedha kwa watu wakati Tanzania haina base ya viwanda na kuona njia za uchumi zinajengwa imara na zio za uchuuzi, Tanzania ya sasa imekuwa ni Uchuuzi, maana tazama hata kauli za Viongozi wetu utaona kuwa ni Uchuuzi mtupu, Ndugu yangu Ngurumo hata hayo mabilioni ya Jk ni Uchuuzi tu maana huwezi kutoa mikopo kabla ya kupiga viwango vya umaskini wa mikoa, Mtu wa lindi ataomba fedha kwa kiwango tofauti sana na mtu wa Dar, Njia ya uchumi Dar na Kigoma ni tofauti sana, Hizo ni Zima moto, Utaona haya mengi mwaka 2009 ya zima moto, Zima moto ndio yamefanyika na kuendelea haya, tuache kuwa na siasa za porojo, kuna hatari kwa Jk kukataa ahadi zake, maana hata yeye anasema kuwa mwaka 2010 sio mbali, sio mbali, Asema Mikakati yake ni long term, au short term, au median, huwezi kufanya hivyo, yaani mimi nashindwa kuelewa sera za CCM, Je za MKUKUTA, ILANI YA CCM, MIOGOZO ya IMF, WD, JE VISION ya 2010, Au ni maagizo ya kukurupuka kama ya Lowassa na Jk, tazama maagizo yao. Hivyo ndio hivyo jamani?? Sijui kama kweli tunakokwenda kuzuri,
Josh Michael
University of Colorado

Anonymous said...

Mikakati ya CCM ni Short term ya kwa ajili ya kuombea kura hivyo hakuna jipya na watu wengi wanona hivyo maana ni watu wa kukurupuka na kuona kama vile, Ukiwa ni Mtu wa Short term ni mbaya sana ya watu kuchoka na kuona utapeli wa kuanzisha vijimiradi vya hapa na pale na kelele zile zile kila siku,Then wewe tazama hata shule hizo za sekondari ambazo CCM wanasema kuwa ni sera, Hivyo tuseme na kupiga Idadi ya watu katika jamii yetu kwa sasa ni wangapi, Je watu kumi ni wangapi wana nafasi ya kuingia sekondari, Idadi ya ukuaji wa watu ni geometric progression GP wakati shule zetu ni AP, Athematic progression, Hivyo ni mbaya sana.
Josh Michael

Anonymous said...

Mimi Nataka Siku hizi CCM waje na Takwimu Halisi siyo za kupikwa kama vile Za BOT Hata haya makusanyo ya kodi kimsingi na kiuchumi ni yale yale maana ukiwa unakusanya kodi wakati mfumoko wa bei, Inflation kubwa ni sawa na kukusanya makusanyo makubwa then wewe unaona kuwa ni makubwa kumbe ni yale yale, Umfumuko wa bei unaweza kufanya makusanyo ya bei kubwa makubwa, then hayo makusanyo ya kodi yanaishia kwenye serikali kuu kwa ajili ya Utembo wa Serikali ya Kikwete, ***Utembo Ni Ukubwa wa serikali ya Jk, maana huwezi kubwa na baraza la watu 65 hivi, Hata, Serikali zote Duniani zina idadi ya Wizara na mawaziri, Hivyo Kuna Hatari sana ya Mapato yote kuishia huko, Hakuna Multiplier ya uchumi huko Tanzania, hiyo ni Hatari sana, Hivyo ipo hatari sana kwa siku za usoni watu kuichoka serikali, Tunataka Viwanda, Barabara, Umeme, Afya, Elimu Bora, Shule zinye walimu, Maabara, Computer, Mtawanyiko wa Kiuchumi kwa wote na link mpaka Kijinii kule Musoma, Siyo Porojo za CCM na umaskini wa kupindukia wa watu, Laiti Mungu angekuwa anatoa daraja kwa watawala basi CCM wangepewa FFF sehemu zote, maana hivyo, jaribu kufikiri hali ya umaskini wa Watanzania, Then ni upuuzi kusema kuwa nchi yetu ni tajiri wakati watu ni maskini, Huo ndui Uchuuzi wa kiakili, Uchuuzi upo Kibao,Upo wa kiakili, Masoko, Serikali, kila sehemu upo, Hata CCM na watu wake.
Josh Michael
university of colorado

Anonymous said...

Tazama ILANI YA UCHANGUZI YA CCM INASEMA KUWA WATANZANIA WANYWE MAZIWA< Hii ni Kweli Kabisa ipo kwenye ilani yao ya mwaka 2005-2010 hivyo hizi ni kebehi kubwa sana, hivyo kama uchumi wako safi lazima utakuwa na mlo safi na vitamini vya protein utapata sehemu nyingine ya chakula, HIZIZ NDIO SERA ZA CCM, KUSHINDWA KWAO ni Kubwa Nchi Haina priority cha kwanza, ni kipi cha pili ni kipi, Vyote kwa CCM na wakati mmoja, Sasa unafikiria utapata ufanisi?? Kamwe huwezi??
Josh Michael

Anonymous said...

Kikwete hana miaka 2 ni mwakani tu ndio umebaki, maana hata wakipanda mipango yao then waje watume kwa ajili ya kuomba fedha toka kwa wafadhili then wao wafadhali waje kujibu na kukaa kwenye mabunge watoe fedha ni mwaka 2010 ndio, sasa hivi wanapanga waje kuandika mchanganyuo kwa ajili ya kuombea pesa kama wao then utekelezaji na mipango kurudi kwa wananchi sio leo ni mwaka 2011 hivi ndio utaona haya, hata barabara tazama kwa makini sana utaona ni zile zilizokuwa katika mipango ya maendeleo siku nyingi sana maana hata angekuwa Mrema zingejengwa tu, hakuna shaka,
Josh Michael

Anonymous said...

Josh,

Naona una hasira kweli kweli! Fanya kitu basi!

Anonymous said...

Hasira ndio kuna Hasira kuona kuwa Mama Zetu wanakufa kwa kukosa huduma za afya bora, Kukosa Nauli za kusafiri miaka nenda rudi, Kukosa Pesa za kuwapeleka watoto wao Shule, Kwetu sisi tumepata Bahati san basi lazima tupaze sauti zetu kuwaeleza Viongozi wabovu wa tanzania, Mimi sijakulia kukubali kila kitu, Nimejifunza kuhoji na kufikiri mbadala, Wewe Tazama Tanzania ya leo, Mtu anajifungua kwa Kukimbia michango ya shule?? Hivyo kweli hivi ni haki, Hivyo ndio Mungu anapenda, Hapana Shaka kuwa Sisi tupo kwa ajili ya watu wengine, Sijazaliwa katika fikra za Kinazi kama hizo za wao Mafisadi,Kuhoji, Kufikiri mara 100 zaidi ya watu wengine, na kutazama njia mbadala za kufanya kila siku, Ndio maana kila siku ni matatizo yale yale ya ujinga,umaskini, maladhi ,na utapiamloakili,, Kama kweli tunasema kuwa sisi ni viongozi basi lazima tufanye na tukubali kuwajibika, kweli kweli.
Josh Michael
Josh Michael
Colorado

Anonymous said...

Bila elimu ya ujasiriamali kutolewa kwa walengwa hata kama wajasiriamali watapewa mamilioni ya fedha kwa ajili ya miradi yao mbalimbali, mwisho wa siku miradi hiyo itakufa.Wakati Serikali inatoa mabilioni hayo ya JK, Watanzania tujiulize ni wajasiriamali wangapi waliopata elimu ya ujasiriamali kabla ya kupewa mikopo?

Kama hakuna mikakati ya kuwaandalia wajasiriamali mazingira ya kuwa na uwezo wa kusimamia vema miradi yao kabla ya kupewa mikopo, uko wapi umakini wa serikali katika mipangilio yake kwa lengo la kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania?

Tunapoona ulegelege huu wa serikali katika mambo ya msingi kama haya, kwa nini tusiamini kuwa viongozi wetu wanapotoa ahadi hizi huwa hawana dhamira ya dhati na badala yake ni porojo na propaganda zinazolenga matarajio yao ya baadaye na vyama vyao siasa?

Maisha bora yanakwenda sambamba na mambo mengi hii ni pamoja na ubora wa miundombinu kama vile barabara, huduma za afya, maji na suala zima la utunzaji mazigira.

Ukipita katika barabara nyingi nchini hasa zile za vijijini utaona wazi kuwa bado tuko nyuma sana, hata kauli za viongozi wetu kuwa barabara nchini zimeboreshwa, hutakubaliana nazo.

Fedha nyingi zinatengwa na halmashauri husika kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa madaraja vijijini.

Kumekuwapo na malalamiko kuwa pamoja na kwamba barabara nyingi za vijijini ni za changalawe na molamu, zinatengenezwa chini ya kiwango, huku wahusika wakijichotea fedha hizo mali ya walipa kodi.

Cha kujiuliza hapa ni je, kama serikali imeshagundua kuwa wajanja wachache wanaiba fedha za ujenzi wa barabara kwa kujenga barabara zilizo chini ya kiwango, kwanini isinunue vifaa vingi vya kuhakiki ubora wa barabara ili kuwabana wezi hao?

Wakati wa mvua za masika, barabara nyingi za vijijini hazipitiki kabisa. Mito hufulika maji na kutenganisha jamii moja na nyingine.

Kama mawasiliano kwa njia ya barabara kati ya jamii na jamii nyingine si ya kudumu, unapomwambia mwananchi juu ya maisha bora, ataelewa nini?

Kwa upande wa huduma ya afya, hali si nzuri pia,tatizo kubwa ni rushwa. Kina mama wajawazito, watoto chini ya miaka mitano na wazee zaidi ya miaka 60, wanatozwa fedha kinyume na utaratibu. Madawa mengi hayapatikani hospitalini kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuibiwa na baadhi ya watumishi wa hospitali ambao wanamiliki maduka ya dawa baridi mitaani.

Kwa upande wa maji, hali ni mbaya pia, maeneo mengi nchini hayana mfumo wa maji taka.

Hii inasababisha watumiaji wa maji majumbani na viwandani kuwa na matanki ya kuhifadhia maji machafu ambayo yako chini ya ardhi.

Pamoja na kwamba matanki hayo hujengwa kwa simenti, hufika wakati maji hayo huvuja chini kwa chini na kutililika hadi kwenye vyanzo mbalimbali vya maji, hali ambayo huchafua maji hayo (water pollution).

Watanzania wengi hawana maji ya bomba hasa wale wa vijijini.

Tegemeo lao kubwa ni maji ya visima, ambapo wakati wa kiangazi hutembea umbali mrefu kutafuta maji. Tatizo hili ni kubwa. Serikali inafanya nini ili kuhakikisha kuwa inapunguza tatizo hili?

Kuna wawekezaji wengi katika maeneo mengi hapa nchini, lakini utashangaa kukuta katika maeneo hayo ambako kuna rasilimali kubwa, wananchi hawana maji. Ni wazi ukimweleza mwananchi kwamba serikali inamwandalia maisha bora hawezi kuelewa!

Katika suala zima la utunzaji mazingira nchi yetu iko nyuma sana. Katika maeneo mengi yenye migodi inayoendeshwa na wawekezaji, kuna malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wanaozunguka migodi hiyo kuwa kemikali za sumu kutoka kwenye migodi hiyo, kama vile mercury na sodium cyanide ambazo ni hatari kwa maisha ya binadamu na viumbe hai wengine, zinatililika hadi kwenye vyanzo vya maji.

Wananchi wanapiga kelele lakini hakuna anayejali. Kama Serikali inafanyia kazi madai hayo ya wananchi inapaswa ichunguze na kutangaza matokeo ya uchunguzi wake ili wananchi hao wajue ukweli.

Nilitembelea eneo la mgodi wa dhahabu wa Buhemba ambao umefungwa kwa sababu zisizoeleweka. Uongozi wa kata hiyo ulinieleza kuwa wananchi wa vijiji saba vya kata hiyo sasa hawatumii maji ya Mto Kinyonga kwa madai kuwa maji ya mto huo yana sumu inayotokana na kemikali za mgodi huo. Kutokana na madai haya ndoo ya maji katika maeneo hayo inauzwa kwa bei ya sh 500 hadi sh 800.

Nilijionea mashimo marefu na mlundikano wa udongo wenye vipande vya miamba ambapo sasa wananchi wako katika hatari ya kupata ugonjwa wa silicosis kutokana na vumbi la vipande hivyo vya miamba.

Kuhusu sera ya madini, taratibu ziko wazi. Mwekezaji anapotaka kuondoka, lazima afukie mashimo kwa kurudishia udongo, kisha kuboresha mazingira ya eneo husika kwa kupanda miti na wanaohusika na masuala ya mazingira lazima wahakikishe utaratibu huu unafuatwa ndipo mwekezaji aruhusiwe kuondoka.

Kama utaratibu ndio huo, iweje mwekezaji huyo aondoke bila kutekeleza makubaliano yaliyomo kwenye mikataba ya madini?

Kwanini vilio vya wananchi wa maeneo hayo juu ya kuwapo kwa sumu katika maji ya Mto Kinyonga vinapuuzwa? Unapowaambia wakazi wa maeneo hayo kwamba kuna ndoto za kuwa na maisha bora, wanakuelewaje?

Vilevile mgodi huo umewaibia wananchi wa Musoma Vijijini jumla ya sh bilioni moja kutokana na kutoilipa Halmashauri ya wilaya hiyo mrahaba wa sh milioni 250 kila mwaka kwa kipindi cha miaka minne.

Kwa nini kampuni hiyo ilifanya madudu yote hayo huku serikali ikiwa kimya? Bado tutarajie neema ya kupata maisha bora?

Pia shule na zahanati iliyokuwa inalaza wagonjwa ilivunjwa ili kupisha mgodi huo, kambi ya JKT kikosi cha nyumbu ilivunjwa na askari wetu wakahamishwa kwa mikokoteni ya kukokotwa na ng’ombe na wananchi zaidi ya 100 walihamishwa katika maeneo yao.

Sheria ya ardhi inaeleza wazi kuwa iwapo kampuni binafsi, shirika au taasisi ya Serikali inahitaji ardhi ambayo tayari inamilikiwa na mwananchi kwa namna yoyote ile, lazima imlipe kwanza mwananchi fidia ya ardhi na mali iliyomo kwenye ardhi hiyo.

Kwa mjibu wa sheria ya ardhi, wananchi hao walitakiwa kulipwa fidia kwanza kabla ya kuondoka katika makazi yao. Mwekezaji alitakiwa kujenga zahanati na shule, kabla ya kuvunja zilizokuwapo ili kupisha mgodi.

Hadi leo wananchi hao hawajalipwa fidia, wala hawajajengewa shule na zahanati nyingine. Unyama huu ulifanyika wakati wa utawala wa awamu ya tatu.

Mara baada ya awamu ya nne kuingia madarakani wananchi walipeleka malalamiko yao ngazi ya mkoa hivyo ni imani kuwa uongozi wa juu wa kitaifa unazo taarifa hizi.

Kama ndivyo, iweje Serikali iendelee kunyamaza wakati wananchi wake wakitaabika kwa uonevu wa waziwazi au hayo ndiyo maisha bora?

Katika maeneo mengi hapa nchini, kuna wawekezaji wenye makampuni na viwanda mbalimbali. Hawa ukichunguza kwa makini utabaini kuwa wamewaweka mfukoni baadhi ya watendaji serikalini kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa.

Wapo baadhi ya viongozi hao wanafanyiwa fadhila mbalimbali kama vile kununuliwa magari, pikipiki, simu za mkononi, kusomeshewa watoto wao nk.

Kuna taarifa kuwa baadhi ya viongozi wa wilaya na mkoa katika mikoa yenye viwanda vya samaki hususan Kanda ya Ziwa, hupewa maboksi ya minofu ya samaki kila mwisho wa juma. Aidha kuna taarifa pia kuwa baadhi ya viongozi katika maeneo hayo wanalipwa na viwanda hivyo kila mwisho wa mwezi. Cha kujiuliza ni je, viongozi hao wanapewa fadhila hizo na viwanda hivyo kwa sababu gani?

Kwenye viwanda vinavyomilikiwa na wawekezaji kuna kero nyingi. Viongozi wakuu wanapotembelea viwanda hivyo hawaonani na wafanyakazi ambao wengi ni watanzania, badala yake huonana na uongozi tu na mwisho hupewa zawadi mbalimbali zinazopatikana katika kiwanda husika.

Viongozi wetu wa sasa ni vema waelewe wazi kuwa Watanzania wanafuatilia hali ya mambo nchini, wanasikiliza kila linalosemwa na viongozi, wanafuatilia utekelezaji wake. Na kwa kuwa tuna haki ya kutoa maoni kwa mjibu wa katiba, tutahoji kila tunapoona inafaa.

Zaidi ya yote, viongozi wetu wafahamu kuwa nchi hii ni yetu sote, hivyo basi kila mmoja wetu anayo haki sawa katika kutumia rasilimali zote zilizomo nchini na kwamba wanaojiona wajanja leo kwa kutumia vibaya rasilimali zetu, ipo siku watalazimishwa kujibu juu ya wanayoyafanya sasa.

Wewe unafaaa sana haya ndio mambo ya kiuchumi sio kugawa fedha za kuwakebehi Watanzania. Watakuwa fedha hizo, Nakala ya Makala hii ni Tanzania Daima ya 24/December 2007. Huwezi kugawa fedha, Viwanda sana sana,
Josh Michael

Anonymous said...

Huu utapeli wa CCM MWISHO WAKE UMEFIKA.Kikwete kawa msanii,wasaidizi wake wasanii,wote wasanii.Tanzania ya zamani si kama ya sasa.Ile kizazi cha woga kinaishia taratibu.Tunalea bomu ambalo siku zake za kulipuka zimekaribia.Watawala bado wako usingizini wanajitahidi kuwaongezea watanzania mablanketi mazito waweze kulala unono.Wamesahau waliobaki usingizini ni wale wazee waliokuwa na utii hapo kale enzi za uhuru na miaka ya sabini.Kizazi cha miaka ya themanini kiko nje ya blanketi wakimtazama huyu mwendawazimu,msanii JK akiwafunika waweze kulala unono.Hawa wakitoweka atakuwa na utupu wa kufanya hivyo.Kizazi chetu kitawaadhibu hawa walioishiwa na sera na mwishowe kuwa wezi wa sera za wenzao zenye mvuto kwa wananchi.

KIKWETE:Kama hautawawajibisha hawa mafisadi,tutakupandisha kizimbani sisi kizazi kipya labda mola akuchukue.Mafsadi wote lazima wafike mbele ya haki.Ukishindwa wewe sisi tutaweza.Na wakati huo wewe utakuwa pamoja nao kwa kufumbia macho na kutothubutu kuwawajibisha kadiri kaiba inavyokuruhusu.hatutakuwa na haya.Wazee wakati huo mtatukoma.Tutafanya kwa vitendo si matendo.

Wananchi pia watawauliza wasomi wa nchi hii;walikuwa wapi wakati wao wakiteseka.Hawataulizwa kwa dgrii walizokuwa nazo,kwani haztakuwa na thamani mbele ya umma wenye hasira!!

Anonymous said...

Huu utapeli wa CCM MWISHO WAKE UMEFIKA.Kikwete kawa msanii,wasaidizi wake wasanii,wote wasanii.Tanzania ya zamani si kama ya sasa.Ile kizazi cha woga kinaishia taratibu.Tunalea bomu ambalo siku zake za kulipuka zimekaribia.Watawala bado wako usingizini wanajitahidi kuwaongezea watanzania mablanketi mazito waweze kulala unono.Wamesahau waliobaki usingizini ni wale wazee waliokuwa na utii hapo kale enzi za uhuru na miaka ya sabini.Kizazi cha miaka ya themanini kiko nje ya blanketi wakimtazama huyu mwendawazimu,msanii JK akiwafunika waweze kulala unono.Hawa wakitoweka atakuwa na utupu wa kufanya hivyo.Kizazi chetu kitawaadhibu hawa walioishiwa na sera na mwishowe kuwa wezi wa sera za wenzao zenye mvuto kwa wananchi.

KIKWETE:Kama hautawawajibisha hawa mafisadi,tutakupandisha kizimbani sisi kizazi kipya labda mola akuchukue.Mafsadi wote lazima wafike mbele ya haki.Ukishindwa wewe sisi tutaweza.Na wakati huo wewe utakuwa pamoja nao kwa kufumbia macho na kutothubutu kuwawajibisha kadiri kaiba inavyokuruhusu.hatutakuwa na haya.Wazee wakati huo mtatukoma.Tutafanya kwa vitendo si matendo.

Wananchi pia watawauliza wasomi wa nchi hii;walikuwa wapi wakati wao wakiteseka.Hawataulizwa kwa dgrii walizokuwa nazo,kwani haztakuwa na thamani mbele ya umma wenye hasira!!

Anonymous said...

Naona wewe una mengi sana ya kusema kama mimi maana naona kila siku Jk pamoja na serikali yake wanazidisha mablaketi Watanzania na hivyo huko tunakoenda sio Mbali sana . Tutufika pamoja na utapeli huu asante sana kwa kuniunga mkono.
Josh Michael

Anonymous said...

100%
Nimekubali maoni na mitazamo yenu
je tutafika huku wakiwaonga vitenge mama zetu na kujipatia kura zabure!
niungane na nyia kuwaomba wa tz
kuwa tuachane na ujinga na upumbavu
wa wazi kabisa washenzi hawa
wamesha anza kuwarisisha watoto wao ccm!
sasa tunategemea nini!
tusiwe wavivu wa kufikiri na wakuamuwa jamaa tuwafukuzeni ata leo hii!
hawa watu hawajuwi njaa!!
hawaibi milioni wanaiba mabilioni yetu!
ccm ni wenzi kila siku kwanini tuseme kenya wajanja kwanini tusiwe sisi?
mungu wangu viongozi wa ccm wana naiba hawajuwi shida wao na watoto wao!kwani lazima mtoto wakikwete au lowasa watuongoze au wa mkapa au wasuma, Hivi ndugu zangu wa tanzania yule mtoto wa mwinyi alikuwa na akilisana au?
tuamke na ikiwezekana tuwaondowe kwenye ramani ya siasa

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'