Sunday, November 25, 2007

Tusiogope, Mapinduzi Yanawezekana


Nina hoja mbili. Kwanza, tuwe na rais wa kukaa mdarakani miaka mitano badala ya miaka kumi. Pili, tukubali kwamba maendeleo tunayotaka kuyafanya hayawezekani kama hatutakubali kuanza sasa kufanya mapinduzi. Wengine wana shaka, na wengine wanadhani haiwezekani. Lakini kama iliwezekana kwa Warumi, (mtazame Kaizari Julius pichani na utafakari yaliyomkuta) itashindikanaje kwa Watanzania? Na je, kushuka kwa umaarufu wa Kikwete kwaweza kuwa ishara mojawapo ya mwanzo mpya? Au ndiyo wanaanza kujifunza Afrika Kusini na Kenya, kujitambua na kugundua makosa?Tujadiliane.

23 comments:

Kahigi said...

Hata ikibidi yawe mapinduzi ya kijeshi, kama ni kuikomboa Tanzania kutoka mikononi mwa wakoloni weusi, tuko tayari.

Salim said...

Umesema kweli. Wamezidi kujitanua na vyeo vya kijeshi hadi wilayani wakishani wataweza kuzuia nguvu ya umma ukiamka. Kikwete akae chonjo, watu wenye njaa hawaogopi kupambana, kumwaga damu na hata kupoteza uhai kama wanachotetea kina thamani kubwa.

msavila said...

Katiba inasema rais atakaa madarakani kwa vipindi visivyozid viwili. Hakuna mahali inapotamka rais lazima kaekwa miaka kumi. Ni uhuru wa wapiga kura kumpa kipindi cha pili kuongoza

Anonymous said...

Nyie mnazungumza kwa niaba ya nani? Mlipata wapi uwakilishi huo? Tupeni ithibati. Hatutaki akina Idi Amini watuamulie

Kasongo said...

Bwana anonymous ulyetangulia hapo juu, najua kinachokusumbua ni dhamiri yako chafu. Hapa unajaribu kugombana na kivuli chako mwenyewe na daima hutakikamata. Kama na wewe ni fisadi unapew amuda ujirudi kuliko kukaa hapa na kutetea ujinga ambao haukufikishi mahli popote penye heshima. Unauliza watu wanazungumza kwa niana ya nani? WALIPA KODI wa Tanzania; wanyonge, walalahoi na maskini; watoto wa mkulima anayekamuliwa jasho la damu kushibisha matumbo ya wakubwa wasio na aibu wala huruma; waliojaa maneno matamu midomoni, nia mbaya na matendo ya kihuni, huku wakihonga watu kama wewe wawasemee. Uwakilishi huo unatoka katika mioyo na dhamiri hai.

Pole kuwa wewe dhamiri yako imeshachafuka kwa sifa za ufisadi. Unaowawakilisha wanajulikana, na hawaheshimiki bila mtutu wa bunduki!

Anonymous said...

Kikwete auwawe vijaan tuchukue nchi

Jimmy said...

Hii kali kweli kweli! Kikwete hana sababu ya kufa ili kuleta mabadiliko,, na hata ikibidi afe mtu, nadhani wapo wanaoweza kutangulia kabla yake - wa kwanza akiwa Rostam Azizi, mpika majungu mkuu wa Kikwete na CCM ya awamu ya nne, mtu anayetumia fedha zake nyingi kuhakikisha kusitawisha uovu nyuma ya Kikwete kwa maslahi binafsi. Siku wananchi wakiamka, atakayeumia wa kwanza ni Rostam Azizi!

Anonymous said...

hiyo list a watoto wa vigogo inatisha. ni vema wangetegewa bajeti yao ijulikane nikiasi gani kwa mwaka mafisadi hao wanatumia wapewe tumaana wanatumia wizi

nguchiro said...

Hoja nzito. Wabunge waichukue ili ianze kazi mara moja. Wakati ni SASA siyo baadaye. Mimi ni mwanamapinduzi. Wewe msomaji ni mwanamapinduzi. TUNAWEZA kuleta mabadiliko ya dhati.

mimi ndio mimi said...

mimi nadhani katibu ya tanzania inamruhusu rais haongoze kwa miaka mitano tu halafu inakuwa uchaguzi si ndio majamani.sasa kwa rais kugombea kwa muhula wa pili ni pendekezo la chama kupitisha ili apeperushe bendera ya chama chake ili haongoze tena kwa miaka mitano mengine kikatibu.kwahiyo hilo litakuwa ni pendekezo la chama na taratibu zake.
pili,maendeleo na imani yapo labda kwa wasio ona tu,kwasababu tizama tulipo tokea mpaka sasa tulipo fikia,ki dunia lazima matatizo yatakuwa kwa muda fulani.ni na shauri bora kulinda amani yetu kuliko mapinduzi najua unasema kwasababu haujaona mapinduzi.kicho muhimu ni kumuunga mkono rais na serikali yake wajitahidi katika kuleta maendeleo zaidi kwa wananchi. asante .

Sarwat said...

wewe mimi ndio mimi unakosea unaposema Ngurumo anasema mapinduzi kwa sababu hajayaona! Kwani wewe uliyaona wapi? Hata hivyo, mbona Rais Karume ni tunda la mapinduzi, na CCM wanajivunia mapinduzi hayo? Halafu unazungumzia amani...Tanzania haina amani bali woga na ujinga unaounganishwa na utii kwa viongozi, hata majambazi. Kama hujaelewa hilo tazama ripoti ya utafiti wa REDET, inasema wananchi wengi wanaomuunga mkono Kikwete ni wenye elimu ndogo au wasio na elimu kabisa (WAJINGA).

benjamin said...

Baba ameuza urithi wetu kwa mabepari na kutuangalia tukitumikishwa na mabepari hawa akatunyima hata kufanya umachinga kando ya barabara, ili kuakikisha kwamba tunawatumikia hawa mabepari wachukue urithi wetu wote, tuendelee kuwa watumwa wao.

Naomba mnisaidie kumwambia baba machozi ya wajukuu inafikia kuwa ya damu.
Nadhani baba ni mtoto wa kambo wa hawa mabepari, Si mtoto Halisi wa babu aliyechukuliwa utumwani na hao hao mabepari.

Naomba wote tuwe na umoja tumtafute baba yetu halisi...kwani sina imani na huyu baba.

Bless2TZ

Bobby said...

Ninaandika nikitoka macozi kwa yale yanayowapata watanzania ambao wamegeuaka watumwa nchini mwao. Hv mnajuwa kwamba wananchi wanaozunguka ziwa victoria hwaruhusu tena kuvua? Na mnayo taarifa ya Factory Ships zinazovuna samaki wetu bila kibali pwani ya bahari yetu? Simwoni mwenye uchungu na nchi hii kuanzia rahisi kiwete mpaka mjumbe. What do we do?

Anonymous said...

nakubakiana na nadharia zako bwana, bali utoe marejeo, ili kuondokana na dhana ya simulizi,
unamawazo mazuri sana, bali pia kumbuka wakati wa Julius hukuwa na mwanya kama huu wakti huu wa jakaya, kwa mbaaali tunakuona, kaza buti..bali toa marejeo ya nukuu zako, Anyway kazi yako ni moto weka kuni tunapuliza uwake

Anonymous said...

Ngurumo Mapinduzi darasani, watoto pale UDSM wanabaniwa watanzania mapinduzi yaanze shule, wanafunzi Tanzania hawaoni, macho yamezibwa elimu inaubaguzi wengi tukiishia bachela, master ni baba mkwe, wengi wao hawaelewi nchi yao. wakunzi, vyuo ni shida jamani rudini umkapige lecture watanzania waamke wengi wako darasani wengine wamemaliza wamepofushwa hatuwaoni, tunawaona waliofukuzwa ama walio upinzani, mbowe, mnyika, kabwe n.k ridhiwani kimya...bagati twehve je yuwapi? ndio wahitimu wa vyuo vya Tanzania pekee kati ya mamia wanaomaliza, mapinduzi yanaletwa na wanamapinduzi ni lazima kwanza wawe wengi wengi wao wanageuzwa mabubu na upofu....

masa said...

Wengi wa waliong'ambo ya tanzania ama ni nguvu ya mola au nguvu ya wazazi wenu viongozi wa Awamu ya pili, tatu au hii ya nne, muangalie midomo yenu mnapowatusi wananchi kuwa ni wajinga, ni kweli ni wajinga nani kasababisha, babako au mamako waziri,katibu,balozi,mkurugenzi amehisika na mtawajibika baada ya maisha ya duniani. Mimi mwananchi nisingemwambia REDET ubaya wa mlezi weko waziri kuwa ni mzembe, ningemsifu sana, sina maji,nishati ya kupikia mafuta bei mbaya, chakula ndio usiseme malazi yananiandama nguvu za mwili zinaniishia, mimi mjinga niliyekondeshwa na wewe kuletwa ng'ambo kusoma! je nimshukuru Rais au mheshimiwa babako aliyekubali kuwa waziri, anaposafirisha magogo ng'ambo hajui kwamba ninashida ya mkopo hapa DSA au CBE au IFM? nimlaumu nani, REDET? mwili wangu umekondeana nguvu za mwili sina tena, baba mkapa akala akakupa na wewe kidogo. Mimi hata BOT sijui sura yake kijumba au khorofa! sijui. Muundo mbinu huu ni upi. Sijui adui wa maisha yangu. siruhusiwi, kuishi. Trade union wafanyakazi, wakulima, wachimbaji, wasukaji/wahunzi wakowapi. rais wa chama cha walimu,chama cha wafanyakazi, makuli, wakulima wakowapi? sijui adui yangu. Nielekezeni nifanyeje mapinduzi. Kama alipofanya uchunguzi kule marekani john mnyika akaona viongozi wa Tanzania wamepata shahada zao wengine katika chuo ambacho hata hakitambuliki nchini marekani! je mjinga ni mimi au mkezi wako aliyendanganywa? ukweli uwapi nataka nijue. wabaya ngurumo wajinga ni nani_?

Ansbert Ngurumo said...

Ndugu wasomaji na wachangiaji wa mjadala huu, hoja ya msomaji aitwaye MASA hapo juu ni muhimu sana. Hebu tuisome tena kwa kina na kuitafakari. Kuna ujumbe mzito. Na Mwishoni ametambua kwamba wabaya ni kina NGURUMO. Na WAJINGA ni kina nani? Hili ni swali muhimu. Twaweza kulijadili. Asante. A.M.NGURUMO

Anonymous said...

mimi nadhani masa ana jambo! naomba wachangiaji tulione nani anastahili lawama? na mapinduzi kupitia vyama vya wafanyakazi!

kilian, vestford said...

lakini anachokisema MASA ni sahihi kwa kuwa wanaotoka nje ya tanzania ni ama watoto wawakubwa au kujuana au wenye uwezo, pili nakubaliana na Masa kwamba mapinduzi yanawezekana kama wanafunzi watasomeshwa na kujua kinachojiri kwani hata wewe na mimi tusingejua mengi kama si darasa

Anonymous said...

Mapinduzi ya kweli mpaka tupate viongoz wa maana sio akina mbowe na mtikili wa sanii wa kisiasi kama alivyo kikiwete nchi bado hakuna viongozi wa maana watakaye leta mapinduzi ya maana
Tuna wakosoaja sampuli ya ngurumo ana chuki na kikwete utafikiri walichuliana ma bibi
Nchi hii usanii tu.wakosaji wasanii watawala wasanii wapinzani wasanii
hakuna lolote porojo tu
ukija hapa kwa ngurumo ukitaka kuwa maana sifia chadema kila mtu atakusifu
ujinga mtupu,ukisoa unasemwa as id chadema cha malaika shiiit ujinga mtupu

Mkereketwa said...

We bwana ANONYMOUS wa hapo juu ndo umechemsha kabisa! Unasema Ngurumo anamkosoa Kikwete kwa chuki kama vile wamechukuliana mke? Je, hao wanaomsifu Kikwete na kumlamba viatu wanashirikiana naye mke?

Kamam Ngurumo anakosea katika kumkosoa Kikwete, au kama anamsingizia, au anamwonea ni bora aonyweshwe ameteleza wapi, lakini sijaona kama anamwonea, bali anasema kile kilicho kweli ambacho wanaomtukuza hawakisemi. Kwa upade wangu, namuona Ngurumo kama mwanaharakati asiyeogopa mabavu na vitisho vya wakubwa, mwandishi aliye tayari kusema anachoamini - nimemjua tangu akiwa RAI.

Wewe unasema Kikwete? Ngurumo amekuwa hivyo hata wakati wa Mkapa, na kupitia kwake tumejifunza mengi ambayo serikali inayaficha. Nchi hii ikipata waandishi 10 tu kama Ngurumo, wanasiasa watapata adabu na wananchi wataamka usingizini. Mwache Ngurumo wetu awapashe, maana vyombo vya habari na waandishi wengi wamo mfukoni mwa Rostam, Lowassa na Kikwete. Hizo sifa mnazotaka apewe Kikwete hajaonyesha kuwa nazo, na hizo alizopewa kabla hazionekani. Sasa Ngurumo kakosea nini kutukumbusha hayo na kutufanya tujitazame na kuwatazama viongozi wetu kwa miwani mipya? Anonymous Ziiiiiiiiiiii! Ngurumo hoyeeeeeeeeeeeeee!

Ansbert Ngurumo said...

Ndugu zangu,

Mimi siandiki kwa upendeleo wala woga. Naandika kile ambacho mashabiki wa Kikwete hawataki kukiandika kwa sababu wanaona 'watamharibia.' Mimi nalitazama taifa, si CCM. CCM imekaa madarakani miaka nenda rudi. Imechoka. Imeishiwa mikakati. Inarudirudia yale yale. Tunaisahihisha kwa nia ya kujenga nchi - na kuwasaidia kuamka usingizini.

Kwa nini Kikwete? Ndiye rais wetu. Ana mamlaka makubwa mno kikatiba. Amam yapunguzwe, au ayatumie kujenga nchi, si kushibisha matumbo ya wanaomuunga mkono. Zaidi ya hayo, kabla hajaingia tuliahidwa makubwa mno kutoka 'kwake.' Sasa kama tumegundua ana 'uwezo' mdogo, huku akiwa na 'mamlaka makubwa' tusiseme? Naamini kusema huku ni njia nyingine ya kuwaamsha waliolala, kumwamsha naye atumie mamlaka aliyo nayo, na kuwaamsha wasaidizi wake, hata kudai mabadiliko ya katiba ili mambo ya msingi ya kitaifa yafanyikie, tusibaki kumtazama na 'kumwabudu' mtu mmoja, kiongozi dhaifu tunayemuona malaika - huku nchi inadidimia.

Najua jambo moja. Wanaomtetea Kikwete hawampendi, lakini wanashibia mgongoni mwake; au wana matumaini ya kushiba akiwa pale. Lakini hawamsadii wala hawalisaidii taifa. Mimi nitamsaidia kwa kumkosoa!

Bobby said...

Ngurumo hayo maneno ya kipuuzi wala yasikusumbue hata chembe wewe kaza buti mwanga wino kwa kwenda mbele. Kikwete hata hata kimoja cha kusifiwa hata tukilazimisha vipi hatutaliona. So kukosoa infact nahisi hata hili neno halifit vizuri kwani mkosoaji anaweza kukosoa pumba pia lakini yale yote uyasemayo ni facts tupu.

Umesema kitu kimoja ambacho mara zote nakisema mtu akiwa honest atamsifu Kikwete kama tu yeye ni direct beneficiary wa Kikwete otherwise ana matatizo ya ubongo.

Pili ni kuhusu Katiba ya nchi ambayo imempa madaraka makubwa sana rais (rais ni mungu mtu) which means mkiwa na chekacheka kama Kikwete mmekwisha na ndio yanayotokea nchini

Ngurumo wewe songa mbele kwaa sehemu yako kwani its your responsibilty na you never no ipo sio you will make a difference na wale wanooona una chuki binafi na Kikwete watakuelewa.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'