Monday, March 17, 2008

Bado Sisi

Wakenya wamepiga hatua ambayo lazima tuionee wivu. Huko nyuma niliwahi kuandika kwamba kama tunatakakufanya mageuzi tujifunze Kenya. Lakini tunahitaji 'injini ya mageuzi'. Kenya walikuwa na injini yao, Raila Odinga. Sisi tunaye mtu wa aina hiyo? Ni nani? Ndiyo! Tunahitaji 'Mbegu ya Haradali'...

5 comments:

bulesi said...

Ni muhimu kumjua Raila "AGWAMBO" ni nanikabla hatujaanza kutafakali kama tuna mtu wa aina hiyo hapa kwetu. Raila ni mtu mwenye msingi kiuchumi kutokana na familia yake kwahiyo ni mchumia tumboni, ni mtu msomi mwenye vision ya nini anatakk kwa nchi yake, ni mtu jasiri na mzalendo, ni mwanasiasa mkomavu asiye na visasi na yuko tayari kucompromise kwa faida ya nchi yake.Watu wetu wana visasi, wabinafsi na masikini, bado hajazaliwa "RAILA" wetu hawa waliopo ni wachumia tumboni tu!!

Anonymous said...

Nadhani bwana Bulesi hapo juu ana maana kuwa Raila sio mchumia tumboni bali mtu mwenye nafasi nzuri kiuchumi kwahiyo hawezi kuingizwa kwenye EPA au Richmond watu wetu walivyoingizwa!!Huyu bwana anauchungu na Kenya hawezi kuuza nchi yake kama wanamtandao wanavyofanya kila mmoja na "kamhogo kake".

Anonymous said...

Raila Odinga wetu sisi watanzania ni Freeman Mbowe Mwenyekiti wa CHADEMA.
tumpe support ya kutosha anaweza!
si mchumia tumbo,ni msomi na ni mtu mwenye upeo/uelewa mkubwa wa mambo!

Anonymous said...

na nyinyi hamna lolote mageuzi gani hayo,kenya siasa yao ya kikabila sisi watanzania hatuna ukabila,au ndio ina amasisha ukabila nini.mimi na sema tutajifunza mazuri lakini siyo ya kukatana mapanga.kwasababu najua watanzania hatujafikia katika ujinga walionao hao unao wasifia.MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA YAKO NA YANAENDELEA KUSAMBA NCHINI."WATANZANIA ACHENI KUOTA NDOTO ZA KUPATA MAENDELEO KWA SIKU CHACHE".KWA MDOMO HATA NCHI ZILIYOENDELEA HAZITUPATI.

Anonymous said...

duh,Ansbert mnakazi kubwa kama hawa ndio watanzania ambao mna nia ya dhati kuwakomboa!basi inahitaji kitanzi kuwapunguza wachache hao wenye mwelekeo usiothabiti ili kupata wengi wanaotaka mafanikio ya nchi.nyarubamba

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'