Monday, November 10, 2008

Mtobwa, Nyaulawa wafariki


WADAU wawili wakongwe wa habari nchini wametutoka. Richard Nyaulawa (pichani kushoto), Mbunge wa Mbeya Vijijini na mmiliki wa kampuni ya Business Times inayochapisha magazeti ya Majira, Business Times, Dar Leo na mengine, amefariki dunia. Kwa mujibu wa habari za Majira, Nyaulawa amefia nyumbani kwake Kawe Beach, Dar es Salaam, Jumapili 09.11.2008. Siku hiyo hiyo, mwandishi mkongwe na mmiliki wa gazeti la HEKO, Ben Mtobwa, amefariki dunia kwa ugonjwa wa moyo 09.11.2008 katika hospitali ya Tanzania Hearts Institute, Dar es Salaam. Amewahi kuandika vitabu kadhaa, kikiwamo ZAWADI YA USHINDI kinachotumika katika mitaala ya sekondari. Baadhi ya wanafunzi waliosoma vitabu vyake walipata fursa ya kumtembelea na kumuhoji zaidi katika kujifunza juu ya fikra na mtazamo wake. Mwandishi mkongwe mwenzake, Ndimara Tegambwage anasema: "Mtobwa alikuwa mwalimu nje ya darsasa." Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa ndugu na rafiki zake, marehemu anatarajiwa kuzikwa Jumanne Novemba 11. Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi! Amina!

1 comment:

Anonymous said...

RIP Nyaulawa!

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'