Tunahitaji kujua kwa sababu hatujui; na hatuwezi kujua kama hatujui kwamba hatujui...Hatutajua chochote iwapo hatutahoji na kudadisi. Na kadiri tunavyojua, ndivyo tunavyogundua kwamba hatujui...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
- Ansbert Ngurumo
- Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'
10 comments:
Wewe ni mchochozi nimeisoma sana makala yako hii ya leo kwa ujumla umechemka hujui chochote kwani huwezi kusema hoja ya ya Mahakama ya kadhi ni ya waislamu na sio wakristo,watanzania ama mtu mwingine hadi hapa umechemka kwani ,waislamu sio watanzania na hapa hoja ya msingi ya suala la mahakama ya kadhi kuingizwa katika katiba huku katiba hiyo hiyo ikieleza wazi kuwa serikali haina dini ila watu wake ndio wana dini sasa iweje leo serikali ilijadili suala ya dini bungeni na hata kutaka kuliweka katika katiba yetu tukufu,je? wakristo itakuwa lini na wapangani je? unataka kusema hawataki Mahakama yao na mahakama zlizopo zitafanya kazi gani? nataka unielewe kuwa hakuna anayewazuia waislamu kuwa na mahakama yao ila sio iingizwe katika katiba ya nchi
Lakini nasikitika kusema kuwa wewe ni mjinga kwani umeingia kulijadili suala hili na kuweka uchochezi wako mwingi bila kusoma vizuri hata hiyo ilani ya uchaguzi ya CCM kama ulivyokaza kuisema kwani ilani haisemi wazi kuwa itaunda mahakama hiyo ila inasema italitafutia ufumbuzi suala la mahakama ya kadhi na ufumbuzi ni mwingi hata kuifuta pia ni ufumbuzi ulipaswa kuisoma sana ilani hiyo ya Mafisadi kabla ya kukurupuka kuandika maoni ya kijinga kama haya .
lakini hata katiba hiyo ya Tanzania bado inatamka wazi kuwa kila mtanzania ana uhuru wa kutoa maoni lakini wewe sio mtanzania kwani umebaki kuwa mchochezi na iwapo nchi itaingia katika vita wewe hauta husika kwa lolote
Makala zako nilikuwa mpenzi sana ila nimeona wewe ni sawa na fisadi mkubwa unatumika kuliingiza Taifa katika mvutano.
Mdau Jackson Kalinga mwanakijiji wa Lupalilo ,Makete Iringa
Jackson umechemka sana, maana umeshidwa kumwelewa Ngurumo katika hoja hii unayoijadili kwa mawazo ya kitoto, na kwa sababu umekariri tu hupendi kutafakari. Anachosema Ngurumo ni kuwatahadharisha wananchi wanaotanguliza hisia katika mambo ya akili kama haya, na kuanza kugombania tofauti zao za kiimani zinazochochewa na wanasiasa.
Soma vizuri makala hii utaona kwamba imetulia kuanzia sentensi y kwanza. Vile vile, unaonekana kukariri unachokisomakwenye ilani ya ccm, lakini hujali kwamba walioindi waliifafanua kwa mdomo majukwaani na sauti zao bado tunazo. Nikukumbushe tu kuwa hawakusema wataifuta, walisema wataaanzisha. Kama usingekariri, ungezngtua historia ya suala lenyewe la Makahakama ya kadhi ukajue kuwa kinachozungumwa, na ufumbuzi unasemwa hapa ni kuanzisha kusheria kama walivyofafanua kwa midogo yao zaidi ya mara 28 majukwaani. Sasa wewe umekazania maandishi bila kuzingatia contxt yake.
Mwisho, Ngurumo amesema, na mimi nakubaliana naye kwamba CCM inapaswa kujisafisha kwa Waislamu kwa rais kuzungumza nao sio kukimbilia majukwaa ya dini nyingine, jambo ambalo linawapatia waislamu sababu ya kulalamikia kuingiliwa na dini hizo. Kama wwe unadani unatetea Ukristo ndio ujinga wenyewe kwa sababu principle anayozunumzia Ngurumo ni kwamba kama leo CCM imewatumia Waislamu kwa maslahi ya kisiasa, kam tutaitetea hapa, kesgo itawatumia Wakristo na kuwatelekeza. Kwa hiyo, ukichunguza makala hii ni kwamba inawtaka wanaotoa ahadi wazichunguze kwanza kabla hawajazitoa, na wakishazitoa wasiwe waoga kuzitekeleza, au wakishindwa wajieleze kwa wahusika.
Unazungumzia uchochezi, na nimeona kwamba makaka hii imesadia sasa kuondoa uchochezi ulioanza kujitokeza, kwa kuwasaidia Waislamu watafakarii mbaa wao ni nani, si wakristo bali ni CCm na serikali, na wapambane nayo badla ya kupambana na wakristo. Unaweza kumlaumu Ngurumo kwa ushauri kama huu? Sanasana, wau wenye akili ndogo kama wewe msioweza kuelewa hoja nzuri kama hii ndio mnaishia kugombana na wasiohusika, na kuleta uchochezi dhidi ya dini nyngine mkidhani mnatetea imani kumbe ni hisia tu na kujua kidogo masuala yanayowatia presha. Jackson, kasome tena makala ya Ngurumo, upunguze presha nautumia akili kusihi vizuri na ndugu zako wa imani nyingine, huku ukisaidiana nao kuwabana mafisadi waache usanii.
Njia ya kuepeusha mgogoro katika jamii kutokana na suala hili ni kwa waislamu kuibana serikali (kama alivyosema Ngurumo) na kuacha kujihangaisha na wakristo. Unataka ushauri mzuri kuliko huu? Kama huelewi hili, amakweli umekariri.....
Ngurumo umechemka hicho alichoeleza Bw Jackson unatakiwa kukifanyia kazi ,vinginevyo utashusha heshima yako na gazeti unaloandikia la Tanzania Daima pamoja na Blog yako hii ambayo wengi wetu tulikuwa tukiipenda ila unakokwenda siko suala hapa ni kujirekebisha naamini kabisa hata utetezi uliofanywa na mchangiaji wa pili dhidi ya Jacksoni ni wako pia ila ukweli ndio huo Ngurumo umefulia
Ngurumo hana tofauti na Zeutamu inapaswa awajibishwe kwa maoni ya uchochezi
Neema Joseph ,Mwanza
Ngurumo achana na mambo ya imani za watu ,huo unaofanya ni ujinga mkubwa yawezekana kabisa umesoma ila hujaelimika
By Said Omary ,Tanga
Wewe Ngurumo si mwandishi makini ni sawa na kanjanja iga wenzako akina Michuzi,Mjengwa na wengine wanavyozitumia vyema blog na taalum zao wewe ni mchonganishi mkubwa tena sheteni ambaye hulitakii mema Taifa la Tanzania
Sada Juma, Dar
Kwa staili hiiya uandishi wa comments hizi inaonekana huyu bwana anonymous ni mtu mmoja aliyejipa majina mengi tu. Siamini kama Ngurumo anastahilimashambulizi haya unayomrushia....
Watanzania ni lazima tuelewe hili suala la Mahakama ya Kadhi linahitaji busara, subira na uelewa wa jambo lenyewe.
Ngurumo ametoa maoni yake kama ambavyo anaelewa juu ya suala hili na watu wote wenye busara tunategemea na wengine watoe maoni yao juu ya uelewa wao juu ya jambo hili kwa kutumia hekima walizojaliwa na Mwenyezi Mungu.
Sasa inapotokea mtu mzima na akili zake timamu (kama hana matitizo ya akili) akaanza kuandika matusi, kashfa na kutumia maneno yanayoashilia jazba sijui anataka aeleweke vipi?
Mtu yeyote mwenye busara hutumia nguvu za hoja na si vinginevyo, ukiona mtu anatumia matusi, kashfa, vitisho, na mambo mengine kama hayo ujue huyo Hoja yake/zake hazina nguvu kwa hiyo anadhani akitumia Hoja ya nguvu ndio ataeleweka.
Mtu yeyote akitumia busara zake vizuri anaweza kukataa jambo bila kutumia matusi, kashfa, vitisho, dharau na vitu vingine kama hivyo na akaeleweka anasema nini.
Mtu yeyote mwenye busara hujitahidi kuelewa jambo kwa kina kwanza kabla hajachangia kukubali au kukataa jambo hilo, na kama hana taarifa za kutosha huuliza kwa wenye taarifa za kina ili asije onekana limbukeni wa kupalamia mambo asiyoyajua undani wake.
Mtu yeyote mwenye busara huonyesha busara zake vizuri zaidi pale anapofikwa na changamoto kubwa lakini akawa mtulivu na makini zaidi katika kuitatua bila woga,upendeleo,kutoka nje ya mada wala kusababisha athari mbaya kwa wengine.
Mtu yeyote mwenye busara husikiliza hoja/maoni ya wengine kwa makini kabla ya kufanya uamuzi na pindi akifanya uamuzi huwa na msimamo juu ya uamuzi wake na yuko tayari kuwajibika kwa yatokanayo na uamuzi aliyoufanya.
Ni vizuri basi tuchangie maoni kwa busara na kusoma maoni ya wengine kwa makini ili kuelewa mchango wao katika hili jambo.
Mtu yeyote mwenye busara hushambulia Hoja ya mtu kwa kutoa Hoja ingine na siyo kumshambulia mtu mwenyewe kwa kumtukana, kumkashifu, kumtisha, kumdharau, n.k.
Kwa wale wasiojua kwa ufupi sana ni kwamba mahakama ya Kadhi kwa Waislamu ni IBADA!! Kuwazuia Waislamu kuwa na Mahakama ya Kadhi ni sawasawa na kuwazuia kufanya IBADA.
Mambo yanayopaswa kuamuliwa katika Mahakama ya Kadhi ni Mengi lakini kwa kuwa nchi hii ina dini nyingine ambazo Mahakama ya Kadhi si IBADA kwao ndiyo maana wakasema itashughulika na mambo kama ndoa (za Kiislamu), taraka (kwa ndoa za kiislamu), mirathi (kwa Waislamu) na mambo mengine yanayowahusu waislamu.
Makosa ya jinai kama wizi, uzinzi, ndoa za muislamu na Mkiristo, ndoa za Kikiristo hizo hazihusiki huko kwa sababu hazikufungwa kwa mujibu wa dini ya Kiislamu.
Kwa hiyo jambo lolote linalomhusu mkiristo halitabadilika litaendelea kuwa kama lilivyo hivi sasa.
Mahakama ya Kadhi ikiwa kwenye katiba haina maana nchi hii itakuwa ya Kiislamu, itakuwa kama ilivyo sasa kwamba NCHI YA TANZANIA HAINA DINI ILA WANANCHI WAKE WANA DINI.
Labda niwafahamishe kwa nini ni muhimu Mahakama ya Kadhi iwe kwenye katiba, ni kwa sababu ili maamuzi yake yawe na nguvu ya kisheria kwa hapa Tanzania ni lazima iwe kwenye katiba ya nchi, ingawa hiyo haibadilishi nchi kuwa ya kiislamu kama kuna wanaodhani itakuwa hivyo na wao wanaogopa/hawapendi nchi iwe ya kiislamu au itumie sheria za Kiislamu.
Hili nalo limetokana na sheria za Kiislamu kutofahamika/kupotoshwa kwa kutojua/makusudi na baadhi ya watu kwa chuki, ubinafsi, udini, kutozifahamu vizuri, n.k.
Kama hili lilivyotokea ni sawa kabisa na mchakato unaoendelea hivi sasa ambao kuna wanao upotosha kwa nia mbaya, chuki, udini, ubinafsi, n.k lakini ni vizuri tukakumbuka kwamba wote hapa duniani tunapita tu na kesho ahera tutahukumimiwa kwa kauli, nia ikifuatiwa na matendo yetu.
Vilevile hata binadamu wenzetu watatukumbuka kwa mambo hayohayo.
Nawaomba tuchangie kwa busara zaidi bila matusi, kashfa, vitisho, woga na mambo yasiyofaa kama hayo.
Maoni yangu ni kwamba Mahakama ya Kadhi ni nzuri kwetu sote na haina madhara yoyote kama ambavyo imekuwa ikipotoshwa na baadhi ya watu mbalimbali.
Ubsihi wa nini? Msomeni upya Ngurumo, mtamwelewa. Kumfananisha Ngurumo na Michuzi ni kumuonea na kutotambua mchango wake katika kutufikirisha na kututafakarisha kuhusu masuala yanayogusa maisha yetu. Kizazi hiki kikiishia kushabikia uandishi wa bandika-bandua na fagilia mafisadi hakiwezi kujikomboa kabisa. Machango wa Ngurumo hauwezi kupuuzwwa kirahisi, hata kama wanaoupuuza ni watoto wa wakubwa wale wale wasiotaka kuguswa, na kama alivyosema msomaji aliyetanguli hapo juu, dawa ni kujadili hoja kwa hoja sio kutukana mwandishi, hasa kama wanaofanya hviyo wanadhani wao ni 'bora' kuliko yeye. Ngurumo,. usikatishwe tamaa na vijiifisadi vidogo hivi, we endelea kutwanga tu na kuamsha fikira za wananchi waliolala katika ushabiki wa mafisadi.
Katika katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania inaeleza wazi kuwa kila moja wetu ana uhuru wa` kutoa maoni yake bila kuvunja sheria za nchi,hivyo sioni sababu wala kosa ambalo Ngurumo amelifanya katika uandishi wa maoni yake juu ya Mahakama hii ya Kadhi.
Ifahamike wazi hayo ndiyo maoni yake kama katiba inavyoelezea hivyo wewe mwenye maoni si vibaya nawe kutoa maoni yako kuliko kukosoa maoni ya mwingine bila ya kuwa na sababu za msingi.
Lazima wadau wa hizi blog kubadilika kwani kama mmiliki wa blog ameamua kutoa nafasi ya wewe kutoa maoni yako ni vyema nafasi hiyo ikatumika vizuri kuliko kuitumia kutoa maneo ya yanayokatisha tamaa japo si kusudi langu kukuzuia kkutoa kile ulichonacho ila kabla ya kutoa ni vyema ukapima kuwa kama wewe unasemwa na kutukanwa hivyo utajisikiaje?
Binadamu awaye yeyote lazima hufikiri kabla ya kutenda na huamua na kuachana na kile amacho nafsi yake huchukizwa .
Upo usemi usio rasmi sana kuwa maoni yako yaweza kuwa yangu na mtazamo wangu waweze kuwa wako ila kama ni ule wa kujenga na ambao ukitoa mbele za watu unaweza kupongezwa na kuzua maswali badla ya kuonekana hujui ulitendalo hivyo sina budi kukuomba kaka Ngurumo uwasamehe wote wenye maoni ya chumbani ambayo hulazimisha kuyatoa sebuleni ,wenye elimu wasioelimika na wenye busara wasizozifanyia kazi
WITO WANGU KWENU NYOTE TUSHIRIKIANO KWA PAMOJA KUJENGA NA KUDUMISHA BLOG ZETU TUSIZIGEUZE BLOG ZETU KAMA UWANJA WA MATUSI JAPO HUONEKANI ILA MUNGU ANAKUONA
Post a Comment