Sunday, July 04, 2010

Mdahalo wa wagombea urais Zanzibar

Taasisi huru ya habari nchini, Vox Media Centre Ltd, kwa kushirikiana na kituo cha Televisheni cha Star Tv, jana Jumapili, Julai 4, 2010ilifanya mdahalo kwa wagombea urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Hoteli ya Ocean View Hotel, saa 3.30 asubuhi hadi 7.00 mchana. Mdahalo huo, ambao ni wa kwanza katika historia ya siasa za Zanzibar, utarushwa na kituo cha Star Tv baadaye katika wakati utakaotangazwa baadaye mwanzoni mwa wiki hii. Wanahabari wengi za Zanzibar walishiriki, na kituo cha redio cha HITS FM kilirusha moja kwa moja matangazo ya mdahalo huo. Huu ni wa kwanza katika mlolongo wa midahalo ya kisiasa inayotarajiwa kufanyika mwaka huu kuelekea Oktoba 2010. Star Tv watarusha mdahalo huo Jumatano saa 4.30 - 5.30 usiku.

6 comments:

Anonymous said...

kaka sisi wa ugaibuni utatusaidiaje hasa video clips?

Mdau Hull

Anonymous said...

Tumefurahi kusikia hiki kilichofanyika, tungefurahi sana kupata kilichojiri kwa Video Clips(Short Video)Auidha kupitia kwenye blog yako (vlog) au you tube au kwa njia yoyote ile cha msingi nasisi tulio mbali na nyumbani tunahitaji kikla kazi munayoifanya ningependekeza kama hamjawa na website basi mujiimarishe website yenu iwe ya kisasa yenye uwezo wa kufyonza short video kama tunavyoona BBC iplayer.

Mdau London

Stella said...

Jambo zuri mno hasa kwa wakati huu kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 31. Ninaomba utuarifu mapema ama kupitia blog zako au kwa njia nyingine yo yote kuhusu midahalo mingine mnayokusudia kuendesha. Ninausubiri kwa hamu huo ambao Dr. Slaa ameutaka kati yake na wagombea urais wenzake. Ni vema mgombea wa CCM Jakaya Kikwete safari hii akashiriki; asiukimbie mdahalo kama alivyofanya mwaka 2005.
Kazi nzuri Mkurugenzi wa Vox Media, Ansbert Ngurumo.

Anonymous said...

Stella, Kikwete ameshakimbia! Tumsaidieje?

Anonymous said...

Mkurugenzi wa Vox Media, inasikitisha sana kuona Kikwete hataki kutetea utendaji wake wa kazi tuliyompa miaka mitano iliyopita. Sijui wanaotetea uamuzi wake wa kutoshiriki mdahalo wan maana gani wanaposema eti "Kikwete hahitaji kujitangaza kwani Watanzania wanamfahamu na wanaujua utendaji kazi wake". Wanaondelea kujidanganya kuwa "Kikwete hatashiriki mdahalo kwa sababu kwa kufanya hivyo anawatangaza wagombea u-rais wa vyama vya upinzani" wana mawazo mgando. Mimi ninafikiri wagombea wa vyama vya upinzani ndio wanaomsaidia Kikwete kijitetea na kutangaza aliyofanikiwa kuyafanya(endapo yapo yanayoweza kumtangaza).

Swali lako "tumsaidieje" ni gumu Mkurugenzi. Kama ni kusaidiwa alishasaidiwa sana na uchambuzi wa makala lukuki zilizokwishaandikwa katika magazeti. Kama hakuona zilikuwa na maana kwake, basi tumsaidie kwa kutompa tena nafasi ya kuendelea kukaa Ikulu.

Stella said...

Mkurugenzi Mtendaji, Vox Media, kwa hamu kubwa ninausubiri mdahalo. Hakika niliukosa sana ule wa wagombea urais kutoka Zanzibar kwa kutokuwepo nchini. Sitaki kuamini kuwa nitaondoka bila kuhudhuria, kuusikiliza, na kuushuhudia mdahalo wa wagombea kutoka Tanzania bara - wo wote watakaokuwepo.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'