Wednesday, July 07, 2010

URAIS Z'BAR: Dk. Shein akamiwa


BAADHI ya wanaCCM Zanzibar waliopo Dodoma wametishia kumburuza mahakamani Dk. Mohammed Gharib Shein na kuzuia uchaguzi iwapo chama kitampitisha kugombea urais. Wengine walio Zanzibar wanaendelea kusambaza vipeperushi vinavyokihamasisha Chama cha Wananchi (CUF) kijiandae kuingia madarakani ikiwa Dk. Shein atapitishwa kugombea urais. Wanadai Shein si chaguo la Wazanzibari, bali la vigogo wa Bara na Rais Amani Karume. Na baadhi yao wananukuu Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kuthibitisha kwamba Dk. Shein "amepoteza sifa" ya kugombea urais kwa kuwa amejiandikisha kupiga kura Bara. Ama kweli wamemkamia.

1 comment:

Anonymous said...

"BAADHI ya wanaCCM Zanzibar waliopo Dodoma wametishia kumburuza mahakamani Dk. Mohammed Gharib Shein..........."

Jina lililojitokeza hapa ni la watu wawili tofauti. Haya hutokea, usijali, ujumbe umetufikia.

Stella68

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'