Sunday, February 20, 2011

Mmiliki wa Dowans yuko Bongo
Mmiliki wa Dowans, Brigedia Jenerali (Mstaafu) Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi, anayeishi Oman, ametua nchini na kuzungumza na vyombo vya habari katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski, Dar es Salaam. Akiwa na wakurugenzi wawili Stanley Munai na John Miles, alisema amelazimika kuja kwa sababu amesikia watu wanadai hawamjui mmiliki wa Dowans, na kwamba wanawadhania baadhi ya Watanzania kuwa ndio wamiliki wa Dowans. Akasema: "Mimi ndiye mmiliki wa Dowans."

Akasema si kawaida yake kuzungumza na vyombo vya habari, na kwamba hataki kupigwa picha yoyote, kwa sababu yeye ni mfanyabiashara asiyependa makuu na asiye na makeke. Akasema amewekeza katika nchi 12 duniani, na kwamba katika zote hizo anawakilishwa na rafiki zake; na kwamba hapa nchini aliletwa na Rostam Aziz mwaka 2005 kwa ajili ya mradi wa Fibre Optic.

Katika hili la sasa, alisema amekuja kujadiliana na Tanesco juu ya hatima bora ya kibiashara kwake na fursa ya umeme kwa Watanzania, katika mazingira ya sasa ya mkataba unaodaiwa kuwa na utata, na deni la bilioni 94 analoidai Tanesco baada ya Dowans kuwashinda Tanesco mahakamani. Alizungumza kwa Kiingereza, na nimeweza kunukuu baadhi ya kauli zake moja kwa moja alipokuwa akijibu baadhi ya maswali na hoja za waandishi. Hizi hapa:

1. “I am here to find a happy resolution, a business decision. I am ready to offer something nice to Tanesco if it works out.”

2. “I don’t want to be known. I am a low-profile businessman. I walk free here in Dar es Salaam, and no one knows I own Dowans.”

3. “Rostam Azizi is a friend of mine. He invited me to come and invest here, but he didn’t put in any cent in the project.”

4. “I have businesses in 12 countries allover the world. I can’t go and represent myself in every country. That’s why I gave Rostam power of attorney.”

5. “We have not been tarnished, but we have been mixed up with something else (Richmond)”

6. “I do not need to be cleared by anyone; my electricity here will clear me.”

7 comments:

Anonymous said...

“Rostam Azizi is a friend of mine. He invited me to come and invest here, but he didn’t put in any cent in the project.”


kwanini rostam anasema ye sio mmiliki km amepewa hayo mamlaka yote ina maana anafanya kazi bila malipo?
wasitudanganye bwana, hayo mabillioni yanayolipwa kuna % yake hapo na naamini sio yeye peke yake wapo na viongozi wengine.

the base said...

watanzania jamani tusiwe wapumbavu, awe amestaafu, ana maradhi, kijana, mzeee, mmiliki au sio mmiliki amekuja na amesema anaweza kukaa na tanesco na kuutua mzigo huu kwetu yaani kupunguza au kufuta deni ni jambo jema na la kumshukuru mungu tusitumiwe vibaya na wanasiasa.mungu ibariki tanzania.leornard mbasha.kaka mkubwa 0754453870.

Anonymous said...

Mbinu kama hizi za kusafishana kuelekea uchaguzi 2015 zitakuwa nyingi sana.

Anayesafishiwa njia ya Ikulu hapa ni Lowassa. Na kwa hiyo kumsafisha JK na Rostam.

Kamchezo haka ni katamu kwa wanaojua kufikiri kwa haraka; ila ni kachungu kwa wavivu wa kufikiri.

TUMELIWA!

Anonymous said...

Mchezo wa kuigiza huu. Haya waTZ pateni nondo hizo mkatunge filamu yenye title ZE DOWANS IN TZ.

mahijja said...

nashangaa hao wanahabari wachache walioenda, wamepata hiyo fursa kwa utaratibu gani... au kitu kidogo... na je kumeshindikana kabisa kupata picha? du hapo ndio naona waandishi wapate nyenzo advanced km CNN....
Kama Rostam amejiingiza ktk hiyo bizness akiwa km Mh mbunge na ametajwa , kwa maslahi ya taifa apumzike kando ili atuachie tufuatilie maslahi ya umma yeye ameshindwa.... kutetea maslahi ya umma...

Anonymous said...

rostam knows the a-z of dowans and he's using addawi as a scape goat. let's not be fooled by the emergence of this man. he doesn't own dowans rostam realised that the public is now aware of his wrong doings now he wants to play cool. WaTZ tuwe macho this is a scum

Anonymous said...

I look at Egypt; Tunisia etc and my despair eases somewhat. Don't ever think these thugs will give up without a fight and fact of the matter is, to bring back the rule of law in Tanzania, people will have to die. History tells us this is almost always the only way true liberation comes. The darkest hour precedes dawn. Fellow Tanzanians, don't give up hope. Liberation will come.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'