Tunahitaji kujua kwa sababu hatujui; na hatuwezi kujua kama hatujui kwamba hatujui...Hatutajua chochote iwapo hatutahoji na kudadisi. Na kadiri tunavyojua, ndivyo tunavyogundua kwamba hatujui...
Tuesday, February 22, 2011
Adawi apigwa picha
BAADA ya sokomoko la juzi la Brig. Jenerali Sulaiman Mohammed Yahya Al-Adawi kukataa kupigwa picha, leo "zimefanyika njama kinamna" dhidi yake, akapigwa picha bila kujua alipokuwa anatembelea mitambo yake ya Dowans Ubungo, Dar es Salaam. Ndiye huyu hapa! Na baada tu ya ziara yake hiyo, akaelekea uwanja wa ndege kupanda pipa kurudi makwao Oman. Hata hivyo, kabla ya tukio hilo la Ubungo, Adawi alimtembelea Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal, Ikulu, na akiwa ofisini kwa makamu wa rais, alikataa katakata kupigwa picha yoyote kama alivyowagomea waandishi juzi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
- Ansbert Ngurumo
- Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'
4 comments:
maskini watanzania, sa waandishi wetu walioenda kulala vichakani ili wapate picha za huyo jamaa zitasaidia nini baada ya hapo japo mwenyewe kwel nataka nimwone anafananaje coz hata jina limekaa kitanzania isije ikawa ni mtz aliukana utaifa wake ili aweze kuvuna bila was was!
yaani w wameshindwa kumtia hatiani mpaka kapanda mhuumu mkubwa wa uchumi wetu ghabachori....lol
The most important part of his statement ni pale aliposema kuwa Rostam Aziz ni rafiki yake. hii inamaanisha kuwa hata mkataba walioingia ni wa kirafiki. na mkataba unaohusisha watanzania, so watanzania pia tumeingizwa kwenye urafiki wao, and now they want us to pay the price. Hivi ni wapi kwenye suala la kikazi ukaingiza urafiki mambo yakaenda sawa jamani? This is a big joke!!!!!!!!!! Na kinachonishangaza ni kwa nini hakukamatwa!
wanaopaswa kukamatwa ni viongozi wa serikali si mmiliki huyo wa Dowans
Post a Comment