Sunday, October 14, 2007

Huyu ni Mwalimu wangu


Mama huyu ni mmoja wa walimu wangu. Anaitwa Prof. Susan Miller. Cheo chake ni MBA Academic Director, katika Chuo Kikuu cha Hull. Mpiga picha alinikamata nikiwa nasisitiza jambo - ona mikono, utadhani nasali vile! Teh! teh! teh! Picha hii ilipigwa Alhamisi wiki hii mara baada ya mlo wa jioni ulioandaliwa na Hull University Business School kwa ajili ya wanafunzi wote wa MBA chuoni hapo. Uwongo mbaya, kazi anaiweza.

8 comments:

Siriha said...

Kama uchambuzi wako wa mambo ya huku nyumbani yanatokana na kazi ya huyu mama ni dhahili kwamba kazi yake anaiweza!! Nakutakia kila la kheri katika masomo yako. Ushauri wangu kwako ni kwamba usiwe na haraka kurudi huku malizia masomo yako yote kwanza huku nchi inatawaliwa na "MAFIA' naogopa kwa kalamu yako hawana nia njema na ujuzi wako. Rostam hana uwezo wa kukununua!! Kila la kheri na mwenyezi akulinde.

Ansbert Ngurumo said...

Siriha,

Mama huyu ni bingwa wa masuala ya uongozi na utawala. Si bingwa wa uandishi nan uchambuzi. Hata hivyo,nakiri kwamba elimu anayotugawia inasambaa katika nyanza nyingine. Hivyo, inawezekana uko sahihi.

Unataka nizamie? Hapana! Najua hawanipendi kwa sababu nawakosoa, nao wanataka kusifiwa. Lakini njia ya kuikwamua jamii yetu ni kuitumikia, si kuikimbia.

Wakiniua mimi watazaliwa wengine wenye mawazo na mbinu za kimapinduzi. Damu yangu itawalilia. Lakini piawakumbuke, nao ni binadamu kama sisi. Kama wao wana uwezo wa kuua wengine, wasisahau kwamba na sisi tuna uwezowa kuwaua wao.

Nchi ni yetu sote, na sote tuna connections, hata kama wao ndio wana madaraka leo. Yana mwisho. Ndiyo maana hatusiti kuwahimiza watimize wajibu katika wakati wao. Ipo siku hawatakuwa Ikulu; na siku hiyo yaja kwa kasi sana. Sijui kama wanalitambua hilo!

Hata hivyo, nashukuru kwa ushauri.

Anonymous said...

Nakupokeza sana kwa uandishi wako, your so Critical Thinker wa Tanzania kwa Sasa. Kazana sana tuko wote bwana..!!
Josh Michael
Marekani

Said Michael said...

Nimefurahi sana kumuona mwalimu wako, pili nakupongeza kwa ujasiri wako wa kuandika ukweli bila kuogopa mtu.

Unajua viongozi wetu wakiulizwa Tanzania hakuna mwandishi aliyeuliwa? Watajibu kwa kujiamini "NDIO", Lakini ukweli ni kwamba Tanzania vifo vya waadishi vipo, waandishi wanapotishwa na viongozi ni sawa na kuwauwa moyo wa kuandika ukweli.
HONGERA SANA KWANI MPO WAANDISHI WACHACHE SANA MSIOKUFA MOYO

Anonymous said...

On a different angle, pamoja na kipaji cha uandishi, hivi bado unatunga nyimbo...nimekuwa nikihusudu sana miziki yako mkuu...kama vipi tuwasiliane...
Willy

Ansbert Ngurumo said...

Ndugu Willy,
Sikuweza kukutambua kirahisi kwa kuwa hujaweka anuani wala jina lako kamili. Hivyo, unaposema tuwasiliane, nashindwa pa kuanzia. Labda wewe uwe wa kwanza kuwasiliana nami ama kupitia hapa au kwa kutumia anuani yangu na barua pepe ansbertn@yahoo.com

Ndiyo, bado natunga muziki, ingawa siku hizi nimepunguza kasi. Ukitaka kuzipata an kuzisikia za siku hizi watafute watu wanaitwa Huruma Rainbow Singers, wapo Dar es Salaam, ndio wana muziki wangu kwa sasa. Na mkanda mpya waliotoa (tuliotoa) unaitwa Mungu Kwanza, lakini haujazinduliwa wala kusambazwa. Kama unataka maelezi zaidi tuwasiliane nikupe jinsi ya kuwapata na kuupata muziki huo.

Na sasa nawaza namna ya kupanua wigo kuhusu muziki. Tukiwasiliana au ukiwaona hao HRS utajua mengi. Asante kwa salaam na pongezi. Ngurumo

Anonymous said...

Makala Yako ya jana umesema ukweli kabisa but ujue kuwa CCM ya Leo inategemea sana hekima za mtu mmoja kwa sababu hakuna connection kati na ndio maana kuna Matatizo ya leo. THEN LAZIMA TUJE KUWA NCHI HAWEZI KUONGOZWA KWA KUTUMIA HEKIMA ZA MTU MMOJA KAMA SASA HIVI. SITAKI KUAMINI KWA KIKWETE AU LOWASSA KATIKA KUONGOZA TANZANIA THEN LAZIMA TUJENGE MFUMO AMBAO NI ACCOUNTABILITY KWA WATU NA VIONGOZI WOTE SIO KAMA HIVI. UKITAKA KUJUA KUWA WATANZANIA TUNAONGOZWA KWA HEKIMA ZA MTU MMOJA NA SIO MFUMO TAZAMA MALALAMIKO KIBAO KWA RAIS KAMA VILE HAKUNA VIONGOZI WENGINE WA KUFANYA. LAZIMA TUFANYE HIVYO LA SIVYO MTU KAMA KIKWETE HAWEZI KUJUA KWA KUANZIA KAMA SASA HIVI. MAANA HAKUNA MAANA NA KUWA MSULULU WA VIONGOZI KAMA HIVI. THEN WATU WOTE AMBAO WANAONA KUWA MAMBO HAYAENDI VIZURI KWA SASA LAZIMA WAJIULIZE KWANINI??
JOSHUA MICHAEL
COLORADO
MAREKANI

Anonymous said...

Ansbert, nafurahi kusikia kuwa pamoja na majukumu mazito uliyonayo ya kuwakumbusha watawala wetu wajibu wao pia unapata muda wa kuangalia upande wa kipaji chako kingine cha muziki,

nitakuandikia email Mkuu ili nione nitaipataje iyo miziki,

Willy

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'