Sunday, October 28, 2007

Taarifa hizi zinatisha

Sasa tumeanza kuelewa kwa nini serikali inajikanyaga kuhusu tuhuma za ufisadi zilizoibuliwa na wapinzani. Taarifa mpya mpya zinaonyesha jinsi Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilivyotumika kuibia pesa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa 2005 ili mgombea urais wa CCM ashinde kwa kishindo. Binafsi naamini kwamba, kwa mazingira yaliyokuwapo, mgombea wa CCM angeshinda hata bila ya kununua kura. Soma mjadala hapa.

18 comments:

Anonymous said...

Mimi nilishawahi kusema kuwa JK na wazake wasema kuwa walitumia kiasi gani kwenye Uchaguzi maana unaona kuwa ufisadi ulianza mapema sana. Unakumbuka hata CCM walikwepa kulipa kodo kwenye Mafulana yao toka kwenye bandari ambapo pale Professor Ibrahimu Lipumba aliposema kuwa kuwa wamekwepa na wakatoa taarifa zao mara baada ya taarifa hizo. Ufisadi ilianza muda mrefu ndio maana hata yeye Jk anashindwa kabisa aseme nini hata wawajibishwe watu wote waliohusika kufanya ufisadi hivyo ni sawa kabisa kwa sasa kurudisha walichopanda. Walitoa pesa nyingi sana katika uchaguzi na hivyo wangetoka kiasi kilichotumiaka toka kampeni za CCM zianze kama Billion 6 hivi kwa wastani(kwa makisio maana unaona tu wewe mwenyewe hivyo lazime warudishe walichopanda.. Hapa hakuna kushangaa maana walianza mapema sana harakati zao. Ndio maana watu wote wajue na watambue uozo uliopo huko Tanzania.
Josh Michael
Colorado

Salim KK said...

Kama kawaida yao, kinan Rostam (CCM) wametembeza rushwa kwa vyombo vya habari mambo haya yasiandikwe. Lakini wanajisumbua kwani hawatatuzuia kuwasiliana. Tunazo njia zetu, wao watabaki na hizo za kizamani...Asante Dk. Slaa na mashuja wenzio. TUnakusikia na tunakuunga mkono.

Hii ni aibu kubwa kwa Kikwete; kumbe kishindo chake ni ha rushwa, na pesa yenyewe walituibia sisi na kutuhonga ili tumchague?

Kina Rostam mnapoteza muda wenu kudhibiti vyombo vya habari...Kamam mna dhamiri, ni vema mfunge virago vyenu mapema, wananchi wanaelekea kufanya kweli, muda si mrefu kuanzia sasa. Hatuwezi kuendelea kuumia kwa sababu ya urafiki wenu.

Anonymous said...

Kama Serikali nimechanguliwa kwa kutoa rushwa... HAIWEZI KUKEMEA RUSHWA THEN MIFUMO YOTE NDIO IMETOKANA NA RUSHWA HIVYO LEO KUSHINDWA KWA JK KUFANYA KWELI KWENYE RUSHWA NI USHAIDI MWINGINE WA KUWA AFANYE NINI MAANA NDIO WATU WALIFANIKISHA USHINDI WAO. LEO AMESHINDWA KABISA KUFANYA HIVYO. HIVYO KAMA ALIVYOSEMA KUWA FREEMAN KUWA TUMEPANDA BANGI HIVYO TUNAVUNA TULIYOYAPANDA. NDIO FAIDA HIZO.
JOSH MICHAEL
COLORADO

Anonymous said...

Haya sasa kama na wafadhili nao ni wapinzani CCM waseme basi maana wao wanapenda kusifiwa kama mithili ya Kasuku vile. Afadhali wao Wamesema maana wangesema Wapinzania wangeambiwa kuwa ni WIVU. Sasa Waache waseme wao. JK ameshindwa na kama yeye atabadilika kuna hatari ya wananchi ya kuchoka kusubiri hayo maendeleo ya CCM
Josh Michael
Colorado

Siriha said...

Kama Balali asingetumiwa kuiba fedha toka benki kuu, leo hii hakuna kiongozi wa nchi ambaye angemtetea; angekwisha ondolewa zamani. Ametekeleza matakwa ya ccm ndio maana watawala wetu hawana moral authority ya kumuondoa. Hivi sasa imedhihirika kwamba Lowasa pia anahusishwa na kashfa ya mkataba wa Buzwagi!! Mimi binafsi sioni ajabu kwa waziri mkuu kuhusishwa na kashfa hii kwasababu imedhihilishwa kuwa alikuwa London siku moja kabla ya Karamagi kusaini mkataba na lazima walikutana. Haiwezekani kabisa kuwa alikuwa london na hawakuonana: ikumbukwe kwamba Rostam ndio kiungo muhimu kati ya mafisadi hawa. Anaweka mkakati wa kumuweka Lowassa awe Rais baada ya Jakaya na mbinu anayotekeleza sasa nikuwaondoa wakuu wa wilaya na mikoa ambao hawawataki na kuweka ndugu zao irrespective of their capabilities mfano ni mabadiliko yaliyofanywa kimizengwe kumuondoa mkuu wa mkoa wa Iringa!! Ukweli ni kwamba Lowasa ana hulka ya kujilimbikizia mali na hili hata marehemu mwalimu Nyerere alishasema ; kwahiyo huyu bwana yupo hapo kupora tu na kama Jakaya ataendekeza urafiki at the expense of national interests basi ajue mwisho wao unakaribia na watazikwa siku moja.

Anonymous said...

Kauli ya MAKAMBA HUKO Tanzania inadhibitisha jinsi gani CCM walivyochoka KIMAWAZO. Yaani Makamba anajua kuwa KUKOSEA Ni Haki yao tu.. Hapana MAKAMBA ACHA UZINDAKI HUO maana kama CCM ndio wanatumia MAWazo ha Watu kama wakina Makamba basi wapo sehemu mbaya sana katika ulimwengu huu. Naona Makamba hajui hata kazi ya Vyama vya Siasa. Then Makamba aache kujivunia Ushindi wa asilimia 80 sio Kitu. Mwaka jana tofauti sana na leo kwa kila kitu. Then kama Msimamo wa Makamba unakwenda kinyume na Hata Butibu. Sasa Busara ipo Wapi?? Makamba watu wamechoka kusikia Pumba hizo siku hizi. Wapinzani Watazidi kusema na kukosea mpaka mwisho wa mbingu hata Kama CCM wanataka au hawataki then vyama vya Siasa vipo hapo Kisheria sio sheria toka CCM bali ni Katiba. Acha Majungu Makamba.
Josh Michael
University of Colorado

Anonymous said...

HAKI YA KUKOSOA NI HAKI YA WATU WOTE THEN MAKAMBA AMECHOKA KIWAZO SASA

Anonymous said...

Makamba sio mtendaji size yake ni kwenda kupiga soga na majungu pamoja na Totti. Kazi ya utendaji sio sehemu yake

Anonymous said...

CCM wanasema wanajua madhabi ya wapinzani walipokuwa CCM. Basi WAO huwa wana Tabia ya Kuficha Madudu na madhabi wakati watu wako CCM. Hivyo kumbe CCM kuna watu wabaya wanafichana CCM. Ndio maana yake hivyo Makamba Kauli yake Haina Nguvu na sio kujibu ni kuropoka.

Anonymous said...

Jamani, mbona jamboforums.com haiko mtandaoni! Ilicrash leo saa 2! Au ndiyo kudhibiti huko! Mmh!

Kambele said...

Jamboforums ni ya CCM huwezi kutoa mawazo yako kwa uhuru kama huku kwetu!! usituchanganye kule kuna ma administrator mpaka waedit mawazo yako ndiyo yachapishwe. Tuacheni tujinafasi na blog yetu ya Ngurumo!! Jambo ni ya usalama wa Taifa!!!

Cecil said...

Makamba ni mbwatukaji, hana elimu wala busara. Watanzania wenye akili zao hawawezi kumsikiliza kwani ni mpuuzi tu!

Anonymous said...

Mafisadi wapo Ndani ya CCM Mtu aneyebisha amulize Makamba amewaficha watu wabaya CCM anasema kuwa watu wakiwa ndani ya CCM huwa wana kuwa wachafu na kufanya ufisadi lakini wakitoka huko ndio ufisadi wao unajulikana. hivyo makamba na CCM yako ni Mafisadi. Kumjua mtu mbaya na kumacha wewe pia umeshiriki vitendo vyao. Ndio maana Leo Makamba na CCM yake wanatetea ufisafi wao kwa sababu ya kuwa wapo CCM. Makamba una mwandishi kweli?? mbona kauli zako zimekaa na kujenga picha mbaya sana. Unasemaje kuhusu wapinzani?? Una mafisadi wangapi huko CCM leo?? Tuambie bwana mzee maana wakitoka utasema kuwa alijua ufisadi wao.
Josh Michael

Miruko said...

Mafisadi wanapata hela. Ndiyo. Lakini hawana amani moyoni. Ila kuna mambo yamenishangaza, baadhi ya watu ambao niliwaamini kwa taaluma zao za uandishi wa habari, wamebadilika gharla, wakatimkia upande wa mafisadi...Tuombe Mungu ili walau wachache wabaki.

Anonymous said...

Makala yako ya leo Tanzania Daima ni kweli Kabisa kuhusu CCM na JK na hata hivyo yeye JK kwa sasa hana ubavu tena wa kufanya kitu chochote kile ndani ya Chama hata Katika Serikiali yake. Hivyo Ndugu yangu toka Tuanze Kusikia Habari hizi Za kupitia leo Mikataba ni Leo??? Hapana ni siku nyingi then Kumbuka hata yeye JK aliwahi kusema kuwa Suala ya Mikataba ni Sheria sio kama hivyo watu wanavyosema?? Je hapa uoni kama yeye mwenyewe anjichanganya sana na kauli zake?? Maana kila siku naye anasema kama porojo za wakina Makamba. CCM wamelewa ushindi wa 80 ndio unaowalivya sasa hivi na hivyo kuna kila sababu ya kuona kuwa CCM wanapotea njia na Kama wanataka kweli mageuzi ni kuwa na mfumo Hodari nje ya CCM then ndio unaweza kuonyesha Njia mbadala lakini sio Sasa Hotuba yake ni sawa ni nyingine tu anasoma alama za nyakati na kupuliza kule wa Wapinzani wanaposema. Sasa yeye sio wakati wa Maneno kama hayo ni Vitendo.
Josh Michael
Colorado Marekani

Peter Nyanje said...

Mzee, haya mambo ni hatari sana. Wakati wengine tuna tafsiri fulani ya kujenga nchi, wenzetu wana tafsiri tofauti kabisa na yetu. jambo la hatari zaidi ni kuwa wao wanajiona kuwa wapo sahihi sana kuliko sisi... we wasikilize tu wanapokuwa majukwaani na kuwahimiza watu wafanye kazi kwa bidii, hivi kuna watu wavivu kwa kupenda katika dunia ya leo?
Anyaway, nimeanzisha blog yangu; http://nyanje.blogspot.com naomba nisaidie kuitangaza kwa waungwana wengine

Nyanje PW-Dar

kija said...

tuwe makini jamana, hawa wahindi wanaweza kutuingia kijanja, baadhi yao nchi za nje, wana ubaguzi sana, tuwe makini watanzania wenzetu, maana wanaweza kuvuruga watu akili hawa watu, lazima watutii.

allamwija said...

Hakika CCM ina kazi katika kuangalia jinsi ya kutekeleza sera na ilani yake ya uchaguzi

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'