Friday, October 12, 2007

Kikwete anasaidiwa na Ze Comedy?


Kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuhusu vigogo wanaotuhumiwa kwa ufisadi (akiwamo yeye) haina 'mashiko.' Ukichanganya kauli yake, ya Kingunge Ngombale-Mwiru, na ya Jaji Joseph Warioba, utaona kwamba hapa kuna kutapatapa kwingi. Nashangaa magazeti yameandika JK ajibu mapigo. Nimesoma kwa makini, lakini sikuona hata pigo moja alilojibu. Hata waliosema ametoa majibu mazito wamemkweza bila sababu. Sikuyaona. Kama waliomtangulia kutoa kauli, analenga lakini ameshindwa kuwachanganya wananchi. Lakini kwa kuwa yeye alipewa muda mrefu kusoma alama za nyakati, na kwa kuwa yeye ndiye mkuu wao, wananchi walitarajia kauli pevu zaidi kutoka kwake. Haijapatikana.
Nadhani wapinzani wamemjibu vema. Ametonesha vidonda. Na bado yataibuka mengine tu. Rais ameibua maswali magumu. Nami bado ninaye; namtafakari. Katika hili, siko peke yangu. Tazama mchambuzi mwingine alivyomfanyizia Kikwete. Sasa nasikia wasanii wa Ze Comedy wameanza kuigiza tuhuma za vigogo, huku wakiwatetea watuhumiwa na kumsakama Dk. Slaa. Niko mbali na nyumbani. Wanaojua walete habari kamili. Inawezekana CCM imeamua kuwekeza katika Ze Comedy kuwapumbaza Watanzania, kuwatetea mafisadi?

19 comments:

Siriasi said...

Si hao hao ndio walimchangia na kumweka madarakani? Hawezi kuwagusa kabisa, sana sana atawatetea na kuwalinda. JK ameshapoteza sifa za kuwa rais bora. Inasikitisha sana asilimia 80 alizopewa zimetumika vibaya, laiti watu wamngeruhusiwa kupiga kuratena leo, angekuwa kama Mwai Kibaki wa Kenya.

Siriha said...

Hawa ni vijana wetu wenye njaa ambao wanatumiwa bila kujua athali za kutumiwa kwao katika maisha yao na ya Taifa; sawaswa na vijana wanaobebeshwa madawa ya kulevya kwasababu ya njaa!! Jakaya ameshindwa kutawala nchi ndio maana yeye na wasaidizi wake sio tu wanashindwa kujibu hoja bali pia wanashindwa kujibu maswali ya msingi yanayoulizwa hata na watoto wa shule!!
Jakaya hawezi kupambana na ufisadi kwasababu ufisadi ndio uliomfikisha hapo alipo. He is not serious in his undertakings, kwa mfano nilitegemea kuwa baada ya Amina Chifupa kufariki angeongeza kasi ya kupambana na madawa ya kulevya, kuonesha kweli amelivalia njuga suala hilo. Badala yake kuko kimya kitu kinachoonyesha ukaribu wao na wauza unga.
Nadiriki hata kusema kuwa hata hizo safari za nje anazokwenda kila mara haendi kwa manufaa yetu bali anakwenda kuficha mali yeye na genge lake wanazotuibia. Hawa wanamtandao wanamdanganya Jakaya kuwa amevaa nguo kumbe yuko uchi wa nyama!!

Kakele said...

Wababaishaji hawa. wameishiwa, achana nao. Yaani sasa wanataka kututhibitishia kwamba CCM ni chama cha wansanii, serikali ni ya wasanii, na wanadhani wananchi nao ni wasanii. hapo ndipo walipokosea.

Kambele said...

Jakaya atapata matatizo katika utawala wake kwasababu ya jeuri yake ya kutokufuata ushauri wa watu waliomfikisha hapo alipo. Ingawaje anadiliki kuonyesha kwamba anamuenzi hayati mwalimu Nyerere lakini ni mnafifiki kwa sababu anafanya mambo kinyume na imani za Mwalimu; anawakumbatia watu ambao Mwalimu aliisha waita wachafu na ndio wanaongoza serikali na sasa amekigeuza chama cha CCM kutoka kwenye chama cha wakulima na wafanyakazi kuwa chama cha wafanyabiashara na wauzamadawa ya kulevya. Sio hivyo tu anadharau hata ushauri wa wazee wa CCM pale wanapomshauri kuhusu mambo ya utawala!! Ndio maana anaendekeza mambo ya uswahiba kuliko manufaa ya Taifa!! Huko anakotupeleka hakufai inabidi tumueleze hivyo kwa vitendo na muda si mrefu wananchi watamuonesha kuwa nchi hii si ya wanamtandao wasanii.

Shamila said...

Jamani tulionywa mapema kwanza jamaa urais hawezi labda vichekesho na starehe. Hatukusikia, baadhi ya akina mama wenzetu wakabaki kusema ana mvuto. Haya sasa kuleni huo mvuto! (Samahani kwa lugha kali, lakini nitafikishaje ujumbe?)

Anonymous said...

Huo ndio undama wa wana Habari wetu wa Tanznaia , na yeye JK anasema kuwa anayo list ya wala rushwa?? je mpaka leo amefanya nini?? je wao ni wakina nani?? Haya maswali hayajibu kama kweli anapigana na rushwa au vipi?? maana unaweza kuona kuwa hana jipya sana katika hili hivyo huwezi kuwa na serikali inatuhumiwa na then wao bado wako Madarakani. Kiburi cha ushinda wa 80% ndio leo wanatapa nacho na kubeza mambo mengi ya kweli.. Na nyinyi waandishi mnaonfanya na kuona kama vile CCM bado wako kwenye kampeni mnampoteza huyu JK na kumfanya mtu asiye makini. lazima mfanye kweli na kuponya taifa hilo la Tanznaia.
Joshua Michael
Colorado marekani

Anonymous said...

JK na CCM waseme kwanza walitumia kiasi gani kwenye kampeni maana uona wakati mwingine kuwa ufisadi ulianza zamani sana na sasa mtu kama Karamaji ni Fisadi kama anabisha aseme mali yake na watu wote hasa CCM watangaze mali zao?? hata JK naye atangaze mali yake?? maana Mbona Mkapa alifanya hivyo yeye kwani ni nani au katiba ipi unayotumia??
Joshua Michael
Colorado
PS: Watu wote wanaosema kuwa wamesingiziwa wasema kwanza mali zao na wananchi ndio watasema kuwa wao wasafi

Ansbert Ngurumo said...

Ndugu Joshua Michael,
Asante kwa changamoto. Tunajaribu. Pale nguvu yetu inapoishia ndipo hapo. Lakini hatukati tamaa. Tunajitahidi kupiga hatua nyingine kubwa zaidi. Kinachotupa moyo sasa ni kwamba walau jamii imeanza kuamka. Yawezekana ni sababu ya kazi tunayofanya kuihabarisha jamii yetu, licha ya upungufu wa hapa na pale. Na nyie tuungeni mkono, tuendelee kuchapa kazi bila woga. Tanzania ni yetu sote.

Anonymous said...

Asante sana Kaka yangu Ansbert kwa kazi nzuri sana maana huwa wakati mwingine nasoma magazeti ya huko Tanzania napata kizunguzungu sana lakini sio gazeti makini la Tanzania Daima, But Naona kama vile Waandishi wengi wana ajenda gani na JK.. Lazima watu na sisi kama Vijana tuliye mbali na Tanznaia naona JK anakwenda Pabaya sana. Hivi ndio kushindwa huko kaka yangu.. CCM wanashindwa kumwambia ukweli?? Hali ni mbaya sana kwa sasa huko Tanzania. But wanaona ni Kawaida tu.. Hivyo Huwezi ukawa na Jambazi nyumbani kwako ukasema kuwa najua wewe ni jambazi lakini naamua kukusamehe tu?? Hali hii sio nzuri kabisa. Hivyo Mimi napata sana shida kujua msimamo wa JK but niliujua mapema sana kwa kwa Hata wagombea wa Urais wakati ule Hasa Professor Lipumba aliwahi kusema kuwa JK ni mtu wa naona gani?? watu waliona kuwa ni Ngebe za Kisiasa?? Hivyo kama kweli wana fanya kazi Tupo wote japo hatuko Nyumbani huko Tanznaia.
Asante sana Ndugu yangu
Joshua Michael
Colorado
Marekani

Siriha said...

Kweli sasa nakumbuka Ibrahim Nguyuru Lipumba alitutahadhalisha wakati wa kampeni kuwa yeye anamfahamu toka chuo kikuu kuwa JK sio mtu serious katika mambo yake lakini kama dada Shamila asemavyo watu wakasema ana mvuto!! Sasa watu wanakula mvuto wake!! Huyu bwana amekwama, hawezi kazi na ndio maana anakili kuwa hajui eti kwanini nchi yetu haiendelei! Ebo!! Nchi itaendeleaje wakati wewe na wapambe wako mnaikomba. Kodi mnakusanya lakini badala ya kuitumia kujenga madarasa mnatumia kulipa madai hewa ya Richmond na Radar; halafu unasema hujui chanzo cha umaskini wetu. Anza upya braza, chagua watu kazini kwa uwezo sio uanamtandao, usipofanya hivyo utakujakujilaumu kama Estrada wa Philipines!! Tanzania inabadika kwa kasi sana. Leo wanazomewa mawaziri wako itakapofikia na wewe unazomewa na si mbali usipojipanga upya, hata ukitumia FFU kuwazima ujue kibarua kitakuwakimeota nyasi.!!!

kamala J Lutatinisibwa said...

ndugu zangu CCM inajaribu kutumia propaganda ili siraha aonekane bomu, sasa wanamtuum eti aliacha upadre kwa kupenda wanawake. kuwatumia ze comedy hiyo ndiyo janjayao na vyombo vya habari. kinachofurahisha sasa wabongo wameanza kuamka na kusema hata kama magazeti yanampamba kikwete na wala lushwa. ila ukweli ni kwamba vyombo vingi vya habari viko mijini tu. hiv sasa niko mosi nikitokea njombe, nitajaribu kuangalia matumiziya vyombo vya habarina ict kwa vijana na watz kwa jumla, lakini kazi ipoya kuwaondoa watz gizani

Anonymous said...

KUBWA ZAIDI Ya Yote nu Kubwa wa Baraza lake na Mawaziri Hata FREEMAN MBOWE ALIWAHI KUSEMA HILI NA KUONYA KUWA UKUBWA WA BARAZA LAKE NI MZIGO WA WATANZANIA, NI KWELI KABISA MAANA HUKO MBELE TUTAKUJAKUWA NA BARAZA LA WATU HATA 100 NA SISI TUNAONA SAWA.. MIMI NAONA KUWA KUWA IFIKE MAHALI KATIBA ISEME WAZI WIZARA NGAPI THEN HIYO KATIBA IWE NA ACCOUNTABILITY KWA WATU SIYO KAMA HIVI.. KAMA BABA MZIMA HAJUI HATA MAJINA YA WANAWE BASI NI MATATIZO MAKUBWA SANA.. HIVYO KWA RAIS KUTOJUA MATATIZO YA WATU NA NCHI BASI NI TATIZO. NA PENGINE YEYE RAIS ANAJUA MATATIZO YAKE NA NI SERIKALI YAKE ANAAMUA KUFICHA UKWELI... JE WATU LAZIMA WATAKUMBUKA SANA KAMPENI ZA LIPUMBA ALIPOSEMA KUWA KUWA KIKWETE ATAKUWA NI MTU WA MAMISS JE MMEONA AU VIPI?? JE KAMA KAULI ZINAKUWA ZA KISANII KAMA HIVI JE SIO USANII.. AU VIPI?? KUSHINDWA KWA WATU NA WATU WALITOA USHINDI WA ASILIMIA 80 NA PIA NAKUMBUKA SANA FREEMAN ANLIPOSEMA KUWA WATANZANIA WAMESHINDWA NI KWELI TUMESHINDWA JE HUKO NYUMBANI VIPI MAFIGA MATATU NDIO MATUNDA YAKE HAYO.. HAYA NI MATATIZO KUWA NA VIONGOZI NA WATU WENYE UPEO MDOGO WA KUFIKIRI KAMA WANASHINDWA KUFIRIA KIDOGO TU ITAKUWA NGUMU SANA KUONDOA UMASKINI KWA WATANZANIA. POLENI KWA WALE WOTE WALITOA KURA KWA CCM NA HIYO NDIO MATUNDA YA MAFIGA MATATU.
JOSHUA MICHAEL
COLORADO MAREKANI

Anonymous said...

Ndugu Zangu FIKIRIENI JAMBO MOJA. UKIPATA RAIS MSANII THEN TAIFA LA KISANII YAANI( USANII SQUARE) UNATEGEMEA NINI HAPA KAMA SIYO KULEKEA KUZIMU AU JEHANAMU?? MAANA WAKATI MATATIZO YA TANZANIA KAMA VILE JEHENAMU MAAN KAMA WATU WANASHINDWA KULA MLO MITATU NI HATARI KABISA. KAMA WATU HAWANA HATA PESA ZA MATIBABU NI NINI KAMA KUELEKEA KUZIMU. CCM ITAKA KUSIFIWA KWA MAZURI BASI MABAYA NAYO NI YAO MAAN WAO NDIO WAASISI WA MATATIZO YA LEO NA TENA WANAZIDI KUYAKUMBATIA KWA KUSEMA KUWA WANATEKELEZA ILANI YAO.. IPI KAMA NENDA RUDI VILEVILE.
JOSHUA MICHAEL
COLORADO

Anonymous said...

SITAKI KUSIKIA CCM WANASEMA KUWA WATAFANYA HIVI, WATAFANYA VILE, TUTAFANYA VILE,WASEME WAMEWAFANYIA NINI WATU, SIYO KUJENGA SHULE, NI LAZIMA TU WATOTO WA HUKO TANZANIA HATA KAMA ANGEINGIA RAIS WA NAMNA GANI?? HATA KAM RAIS KICHAA SASA WAACHE UBABAISHAJI KATIKA ZAMA HIZI.. HATUTAKI KUSIKIA UBABAISHAJI HUO NA KUWAGEUZA WATANZANIA NI KICHWA CHA WANDAWAZIMU.. HIVYO CCM WAACHE MARA MOJA WASEME KWELI.. HIVYO WAO NDIO WAMEWAFIKISHA MAMA ZETU HAPO WALIPO HII NI AIBU KUBWA KWA CHAMA KUSEMA KILIKUWA MADARAKANI NA KUSHINDWA KULETE TIJA KWA WANANCHI WANABAKI KUPIGA DOMO.. HATUTAKI MADOMO YENU NA SOGA ZETU TUNATAKA MATENDO SASA NA KUONA OKAY..
JOSHUA MICHAEL
COLORADO

Anonymous said...

Mijadala mizito. Inapendeza kuona jinsi Watanzania wanavyofikiri kwa umakini na kwa kina namna hii.

Niseme tu kuwa JK ameshindwa. Serikali imemshinda. Nadhani alihisi kuwa mambo huwa yanajiendea yenyewe. Inasikitisha. Nchi inatumbukia shimoni. Ni nani wa kumlaumu kama si dereva? Na dereva huyo ni nani? Si ni yeye JK? Hivi kwa nini anataka kuwatupia wengine lawama wakati lawama zote anazo yeye?

Kumbuku kule Mbeya alisema kuwa anawafahamu wala rushwa wote. Aliongeza kusema kuwa anawapa muda wajirekebishe? Jamani, huu si utani huu, si dharau hii?

Sasa wanatapatapa. Heshima imewavuka. Siri ziko nje. Bw Kikwete usione watu wanapeana mkono na wewe na kukuchekea na kutaka kupiga picha nawe. Wameshakushusha heshima mpaka tone la mwisho. Wanakudharau, matarajio yao kwako yamesalitiwa.

JK afanye nini kurejesha heshima?
1. Avunjilie mbali baraza lake la mawaziri
2. Iundwe serikali ya mseto itakayowashirikisha wapinzani
3. Mikataba yote ya madini na mingine inayofanana na hiyo ivunjiliwe mbali
4. Mafisadi wote waliotajwa wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria ili wathibitishe wenyewe kuwa wao ni wasafi. Tayari wametuhumiwa, basi walete hoja kuthibitisha kuwa wao si wala rushwa na mafisadi.
5. JK naye alete orodha yake ya watu aliosema kuwa anawafahamu kama mafisadi, muda aliowapa umeshaexpire tangu mwaka jana.
6. Ikiwezekana, aachie ngazi na nchi ichague Rais mwingine. Ni uungwana pale unapoamua kuwajibika kwa ajili ya matatizo yaliyotokea ndani ya uongozi wako. Mbona Mzee Mwingi enzi hizo akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani aliwahi kujiuzulu kutokana na mauji yaliyotokea kule Shinyanga? Kwani ni yeye aliyewaua watu wale? Je, kitendo kile si kilimjengea heshima kubwa sana miongoni mwa Watanzania?

JK, bado unayo nafasi. Kama nilivyoainisha hapo juu.

Unajua, nilikupa kura yangu. Nilikupa si kwa sababu nilivutiwa na tabasamu lako, la hasha. Nilijiambia, ngoja nimempe kura yangu, nina imani naye, atasaidia kubadilisha maisha yangu na ya Watanzania wenzangu. Lakini, lazima niseme wazi kuwa nasikitika matarajio yangu hayakutumia. Ninafanya kazi kwa saa zisizopungua 14 kwa siku. Lakini sioni mafanikio. Naona tu watoto wa mafisadi wanavyozidi kuneemeka pasipo kufanya kazi hata chembe. Bw JK, hutakaa upate tena kura yangu. CCM haitakaa ipate tena kura yangu. Hilo ninakuhakikishia. Mtabaki kupata ushindi baada ya kuiba kura, si kwa sababu tuna imani nanyi tena.

Kwa heri.

Anonymous said...

wewe umesema kweli kweli na sasa ndio majuto makubwa sasa hivi hana wala cha kusema na tena baya zaidi ni kheri hata Mkapa Kuliko JK maan kila siku anazidi kwenda mlama na ahadi zake umesema kweli kabisa.
Joshua Michael
Colorado

Anonymous said...

SHIDA MOJA KUBWA YA WATANZANIA WANA UGONJWA WA KUSAHAU HATA WAGUMU SANA KUONA MBALI NA TENA HATA IKIFIKA WAKATI WA KAMPENI WAO NDIO WATU WA KWANZA KWENDA MBELE NA KUTETEA CCM NA UFISADI WAO. JE KAMA WATU WANATAKA MADADILIKO YA KWELI SIYO KUSEMA TU NI KUFANYA KWELI.. NAJUA UGUMU WA WATU HUKO NYUMBANI TANZANIA. LAZIMA KUWAPA LIKIZO CCM MAANA WAMESHINDWA KAZI NA HIVYO NI KUWAPA LIKIZO NA KUJARIBU NJIA NYINGINE NA KUTAFUTA NJIA MBADALA YA KUPONYA TANZANIA KATIKA CANCER YA UFISADI NA WATU WOTE WANOMPINGA DR. SLAA WASEME MALI ZAO NA WATU TUTASEMA KUWA NI WAKWELI LAKINI NDIO KUMTISHIA NYAU ETI KWA SABABU YA WAO NI VIONGOZI. ZAMA HIZO NI KIMLA SIO SASA.
JOSHUA MICHAEL
COLORADO

Anonymous said...

ni kweli wasanii wa ze comedy walimuigiza slaa kama padri na kuwa alikula pesa za walemavu nafikiri sasa hata gazeti la rai nalo limebadili mwelekeo wa uandishi,watanunuliwa wengi tu tutaona

Anonymous said...

KWA WATU MAKINI SANA NA HATA WAJE NA KUSEMA KWA KUTUMIA PUA, MACHO HATA WAWALETE MTU KAMA MR BEAN UKWELI UNABAKI PALEPALE. HUWEZI KUCHANGANYA MAMBO MAKUBWA NA UPUUZI WA WAO ZE COMEDY. KAMA NYINYI WATANZANIA MMELEWA NA UTANI NA UPOTOSHAJI HUO NI SAWA KABISA NA CCM KUWALETE BENDI YA TOTI NA KUPIGA NYIMBO BAADALA YA KUSIKILIZA HOJA. NILISHAWAHI KUSEMA KUWA WATANZANIA NI WEPESI SANA KUCHUKULIA MAMBO (MEPESI SASA KAMA WATU NI WEPESI NA SERIKALI YAO ITAKUWA NYEPESI, KAMA HIVYO HATA WANASIASA NAO WANAKUWA WEPESI, SIO HIVYO HATA MIFUMO YETU YA UTAWALA ITAKUWA MEPESI, SIO HAPO HATA BUNGE NALO NITAKUWA NI LEPESI KAMA UNAVYOONA KIPINDI CHA MIEZI3 ILIYOPITA NA KUMSIMAMISHA ZITTO. HIVYO NI KAMA CHAIN NA VISCOUS CYCLE YA UWEPESI SASA WANASHANGAA NINI. WATU LAZIMA KUKATAA MAMBO DHAIFU NDIO UFUMBUZI WAKE. NA KAMA HAYO YOTE YAKIKUINGIA BASI UNAKUWA MTUMWA NA SASA NDIO MAJUTO YAKE.
JOSHUA MICHAEL
COLORADO

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'