Friday, October 26, 2007

Habari Corporation yafungua tovuti


Kampuni ya Habari Corporation, inayomilikiwa na Mbunge wa Igunga na Mhazini wa CCM, Rostam Azizi (pichani kushoto), imefungua tovuti ya magazeti yake. Magazeti hayo yaliyowahi kutamba kwa uchambuzi mahiri na makini katika miaka ya 90 na kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, yanapatikana hapa. Siku hizi inaitwa New Habari Corporation - yenye mmiliki mpya, sera mpya mikakati mipya na uongozi mpya.

10 comments:

Anonymous said...

Hivi karibuni katika gazeti la Tanzania Daima jumapili, kulikuwa na makala ya mwandishi wa Tanzania Daima ambae alikuwa amemaliza masomo yake yake huko Hull majuu akituaga wasomaji kwamba analihama gazeti kwahiyo tusingeziona makala zake tena!! Kwakweli nilifarijika sana kusoma kuwa bwana huyu anaondoka kwani he was in the wrong place, afadhali aende huko kwa Rostam wakawe makuwadi na mamluki wa huyu muiran!!'Komando' Manyerere yeye alishawahi kwenda huko. Hawa wote na waende lakini naamini kwa dhati kabisa siku ambayo Ansbert Ngurumo ataamua kununuliwa na huyu Rostam itakuwa siku ya majonzi na msiba kwa sisi wapenda uhuru na Nchi yetu.Ansbert umemaliza masomo yako njoo nyumbani ukabiliane na hawa mamluki wa Habari corporation; jengeni safu nzito ya kupinga utwala wa mafisadi ili nchi yetu ikombolewe.

Anonymous said...

Kama Na wewe utaenda huko Tutalia sana sana. maana siku Hizi Sio Habari tena maana yanamebaki na ushabiki wa kisiasa tu. Huwezi hata kusoma ukaona na kupata mtazama mpya maana yanashabikia sana CCM na hivyo Hakuna Jipya hata waje na tovuti 100 ni mara mia kusoma gazeti la Uhuru utaona na kujua nasoma gazeti la Chama lakini sio hayo siku hizi hakuna jipya humo.. Watakwenda wengi huko kwao na kuona sasa walishaanza kurejea kundini.
Josh Michael
University of Colorado

Anonymous said...

Ndugu yangu wewe soma mwenyewe magazeti yao. hakuna jipya tumechoka na bahari kama hizo. Mimi wakati nipo huko Tanznaia niliacha kabisa kununua magazeti yao tangu zamani maana hakuna cha kusoma labda usome ushabiki. tena nasikia hata wandisi wao huwa wanazuiwa kama wana Habari ya kuhusu CCM, Hata hilo Gazeti la Rai nimebaki kuwa Rai siyo nguvu ya hoja bali ni nguvu ya CCM.
Josh Michael
Marekani

Anonymous said...

Habari Corporation hawajakosea kusema kuwa magazeti yao yana sura mpya maana ni kweli YAHA SURA MPYA tunaona kuwa sura mpya na uandishi wa aina yake na kila kitu ni kipya KWAO so ni kweli kabisa yana sura mpya , Mara 100 ununue kazeti la kiu huko Tanzania kusoma utapata amani lakini sio hayo
Josh Michael

Anonymous said...

MSINUNUE HAYA MAGAZETI-YANAPOTOSHA HABARI. UNAKUMBUKA WALISEMA IRAQ KUNA SILAHA ZA MAANGAMIZI? HABARI HIZO ZILIANDIKWA NA WATU KAMA HAWA-SPIN DOCTORS!!

Anonymous said...

Spin doctor namba 1 ni mmiliki wa Habari corporation, au hamna hizo habari? Na Jenerali ameshawakimbia, hata Rai hatulitaki tena ngoja tukanunue Raia Mwema! Jamani naomba kuuliza blog ya Jamboforums vipi? Maana blog hiyo na hii are my favorites? Angalia Ngurumo wajanja wasije wakacrash server yako kama ya Jambo forums!

Anonymous said...

hakuna jipya.ni upumbavu tu,hatusomi hizo pumba zao

Anonymous said...

Bwana Anonymous uliyetangulia hapo juu, unasema HAMSONI hizopumba zao? Wewe na nani? Mimi naona wanaandika vizuri tu kwa sababu kama unatafuta kipya sijui umekiona Majira, HabariLeo au Mtanzania? Kama una chuki na Ulimwengu kwa sababu ya ushabiki wako wa JK na mfumo wake, unapoteza muda wako bure. Kwanza hawatakusaidia lolote, na watakufa na kuzikwa kwa aibu!!!!!

Anonymous said...

Nimeiona. Mimi nayasoma magazeti hayo bila ubaguzi kwani nisiposoma zitaweza kujua wanachokiandika. Lakini wale wanpezi Jenerali Ulimwengu msikonde mnaweza kumpata kupitia hapa www.raiamwema.co.tz

Anonymous said...

hayo magazeti mnayoyaponda, mnayasoma sana ndiyo maana mmeweza kujua yaliyomo.
Mwenye akili hawezi kusema eti hataki kusoma kitu fulani. Bila kusoma, mtajuaje ujinga na welevu? Tabia ya Watanzania hata tunapokuwa nje ya nchi, ni ile ile-kutotaka kusoma hapa yasiyotufurahisha. Kweli Mwafrika ukitaka kuficha pesa au dhahabu hadi asiipate mtu mwingine-ficha ndani ya maandishi-kitabu au gazeti.
Kwa kukataa kusoma baadhi ya mambo, tumeendelea kuwa wapumbavu na tunaoegemea upande mmoja.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'