Tuesday, November 06, 2007

Mkaribisheni Peter Nyanje

Mkaribisheni Peter Nyanje, mhariri wa habari wa gazeti la Tanzania Daima katika ulimwengu wa blogu. Ameingia na kuahidi makubwa; na anatualika "tujadili hoja nzito." Tunaamini ataitumia blogu yake kuwaletea wasomaji kile wanachokikosa katika gazeti lake, yaani kile kilicho muhimu kinachobaki na kukosa nafasi katika habari za kawaida za kila siku. Blogu yake hii hapa. Mtembeleeni.

3 comments:

Kakobe said...

Nyanje hongera kwa hatua hiyo. Sisi wengine hatuna blogu bado, tunaendelea kuwasoma nyie wenye vipaji vya kuandika. Nilikuwa sijui kama wewe ndiwe mhariri wa habari wa Tanzania Daima... kumbe ni wewe? Afadhali umeonyesha tofauti kati yako na Manyerere kibaraka aliyeuma mkono unaomlisha! Tunaamini hutatuangusha wasomaji wako katika gazeti na blogu. Mwaga vitu, tutasoma tu usiwe na wasiwasi.

Anonymous said...

Hongera sana kwa kuwa mtu makini kwa Gazeti la tanzania daima maana ndio gazeti ambalo unaweza kusema kuwa huru zaidi.
Josh

benjamin said...

Kwa kweli mi si msemaji sana kaka,

lakini sima budi kukupa hongera,
Don give up, Because unaweza okoa maisha ya watanzania wenzako

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'