Wednesday, November 07, 2007

Kuna ukweli gani katika hili?

Ujumbe huu unazunguka katika barua pepe za watu. Ulipofika kwangu nikaamua niuweke hapa tuujadili wazi wazi. Unasema hivi:

"Je tutafika? ...tuhuma zote za ufisadi zinazoikabili BoT, je unawajua walioajiriwa kusimamia uchumi wa nchi yetu na kutuletea mafanikio? Pokea taarifa ya wateule hawa. Ndani ya mtungi wa BoT walioqualify kuajiriwa kwa sifa na vigezo vinavyotambulika na BoT ni pamoja na hawa wafuatao:-

1. Pamella Lowassa,
2. Filbert Frederick Sumaye,
3. Zalia Kawawa,
4. Harieth Lumbanga,
5. Salama Ally Mwinyi,
6. Rachael Muganda,
7. Sylvia Omari Mahita,
8. Justina James Mungai,
9. Kenneth John Nchimbi,
10. Blassia Blassius William Mkapa,
11. Violeth Phillemon Luhanjo,
12. Liku Irene Katte Kamba,
13. Thomas Mongella,
14. Jabir Abdallah Kigoda etc.

Hapa nani atamwajibisha Dalali alas Balali? Je KAPUKU MWENDE(a.k.a KAYUMBA) ATAAJIRIWA KWELI HAPO? Hawa ni wale wenye uhusiano wa moja kwa moja na wazito wa nchi, wapo wengine ambao ni ndugu wa karibu au kabila moja na waheshimiwa. Ni vigumu kuamini kuwa hii ni bahati mbaya (mere coincidence). Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika."

26 comments:

Anonymous said...

Ndio Maana tunasema kuwa ufisadi upo na una mizizi muda mrefu sasa kama hawa jamaaa huwa wana root mpaka kwenye BOT na familia zao sasa ndio TZ imekwisha.. Sasa wewe jaribu kuwaza maana yote ni majina ya watu ambao wazee wao ni watu wa CCM na Serikali yao.. Huu ni uhuni mkubwa sana sana ndugu yangu.. Sasa ndio kusema hata wao CCM na serikali yao wanashindwa kufanya kweli wana maslahi huko katika Hazina ya NChi Wewe chunguzza elimu zao ni Hatari tupu maana kuna watu wazuri wana uwezo wa kufanya kazi wanashindwa kuapata. Kazi hizo zinatangwa saa ngapi?? Wao wanajua.. Huu ni ufisadi mwingine ndugu yangu kujaza majina na watoto wao BOT ni uhuni mkubwa sana.
Josh Michael
University of Colorado

Anonymous said...

Watu wasischangae maana ndio watu ana ndio waliwapa madaraka. Ndugu yangu kama ndio namna hii ya watu ndio tunao kuna hatari sana ya kuficha bahari nyingi na tena kupiga taarifa za uchumi.. Mimi huwa nashangaa sana kuona watu ambao wanajiita wachumi wanapredict takwimu za kiuchumi. Nasoma Uchumi ni tofauti sana na jinsi CCM wanavyotafisiri mambo mengi sana katika uchumi. Nakwambia CCM wanapiga soga na porojo tupu. Kuna haja watu kujua namna ya watu ambao wanaongozwa nao. Huo ni uonevu mkubwa sana kwa watu makapuku na maskini wa Tanzania.
Josh Michael
Colorado

Anonymous said...

BOT!

Ngurumo, najua kabisa hawa wanaweza kuwa na sifa na ndiyo maana ukahoji kama kweli uwajibikaji utakuwapo hapa. Hii ndo issue, tabia mtu hazaliwi nayo ila hujifunza. Wengi wa hawa wazazi wao ni watu wanaotuhumiwa sasa hivi katika ufisadi mkubwa unaoligharimu taifa letu. Na wote tunajua kuwa mtu ukiacha shule na dini huanza kujifunza tabia nyumbani (familia)

Hapa sina maana kuwa hawa ni mafisadi nao, la. au kwamba si wawawajibikaji hapana, nachotaka kusema ni kuungana na wengi kuwa hawa hawana chochote zaidi ya kukaa hapo na kuuza sura tulizozizoea ambazo hazina jipya kwa maendeleo ya wengi.

Naungana na wote wanaoamini kuwa kina 'kayumba' hata wasome na kufaulu vipi bado wataendelea kuhangaika kufanya 'biznesi' kwani haya ndo maisha wanaotuaminisha kutuletea maisha bora wanayotuwazia, kuwatengenezea maisha bora watoto wao.

Nafasi hata kama zingetangazwa nakuhahakikishia kwamba hakuna jipya ambalo lingetokea, wewe nenda na vyeti vyako hata kama vina sahihi ya 'chissano' bado hutopewa nafasi, uchumi unaojengwa ni kwa ajili ya 'watu', viatu tukae tunasubiri siku ambapo tutaweza kuona na kusema.

Kazi unayofanya Ngurumo ni zaidi ya kutuhabarisha, una darasa zuri sana kwa ajili ya wote wenye nia njema na taifa letu tajiri lililoshiliwa na wale ambao hawakutoa jasho katika kulijenga

Wapo w

Samson said...

Ndiyo ukweli wenyewe huo. Hiyo ndiyo Tanzania. Na hao ndio wanaojua jinsi uchumi unavyokua, maana ndio wanaoandaa ripoti za benki kuu inayotumiwa kuwahadaa watanzania. Au tuseme ndiyo maana tunaambiwa uchumi unakua lakini hatuuoni. Kumbe hawa ndio wanaoandaa taarifa hizo? Bais, tumekwisha!

Anonymous said...

WAna CCM kwao Uchumi ni kwenda kununua vitumbua na maandazi kila siku asubuhi na kunywa chai. yaani wanashindwa kabisa kutofautisha mambo muhimu na mambo ambao ya lazima kwa kila binadamu. Hivyo wewe sikiliza taarifa za hotuba ya Kikwete nayo kama Makamba vile. Ni SOGA KWENDA MBELE> Hiyo ni Hatari kwa Raisi kuwa naye mpiga soga kama wakina Makamba. Hivyo kuna lazima kwa kila mtu kujua uozo wa viongozi wao.
Joshua Michael
Colorado

Yusuf said...

Watanzania wenzangu, hiyo ndiyo Tanzania. Tusipoirekebisha hali hii tusishangae kwamba tunaelekea katika manmgamizi...

Anonymous said...

Wakurekebisha mambo ni wewe na mimi na wananchi wote lakini sasa kama vile sanaa ya kuigiza tu haifai kabisa ila inabidi kufanya kweli sio kubaki kuongea tu.
kaka yangu Ngurumo umesema kweli kuhusu mahakama ya kadhi mkuu, ya Tanzania, Tazama hutoba ya Rais kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Maaskifo wa Lutherani.
Josh Michael

Anonymous said...

Tazama Majibu ya Kikwete kwenye mahakama ya Kadhi, Uliyasema haya kwenye makala yako ya jana, hivyo hapa kuna mambo mengi ambayo JK inabidi ajiulize, yeye anasema hausiki. Hivyo kama kweli CCM wanaandaa Ilani bila ya kumshirikisha muhusika, hivyo ni hatari sana.. Hivyo kwake yeye kusema kuwa waliandaa ilani ni watu wengine sio yeye hapo ni kujitoa tu. Huwezi kuzunguka nchi nje nzima na kusema kuwa ILANI ya CCM ni Bora ya kujua watu walitunga au kushiriki.. Maana Wakati ule analikuwa anazunguka bila ya kujua ilani yenyewe.. HIi NI HATARI. Kusema tu wakati huu sio Kitu. JK alijua mapema. Kunadi sera wakati ule alisoma sana. Hivyo wewe ulisema ukweli kabisa. Naungana na wewe Ngurumo.Huwezi kuhubiri kitu ambacho hukijui kabisa.
Josh Michael
Colorado

mwandani said...

Kuna majina machache ya watu hapo hayahusiani kabisa na vingunge wenye majina hayo.

Nasema hivyo kwani ninawafahamu kwa ukaribu hao vingunge.

Ingekuwa vizuri barua hiyo ibainishe watu walioandikwa hapo wana uhusiano upi na vingunge.

Anonymous said...

Kaka yangu Ngurumo , Sasa waislamu watafanya nini baada ya kauli ya Rais.. Uliwaonya kuwa watapewa ahadi na Kama alivyofanya Kikwete Kukimbia hoja ni sawa na kukana Ilani yake Mwenyewe ya Uchaguzi.. Huko Ndio Kushindwa kwenyewe. Hataki kuonekana mbaya kabisa. Sasa kama walioanzisha ni wakina MREMA yeye iweje IWEKE kwenye ILANI> SIO KWELI KUWA ALIKUWA HAJUI> SIO KWELI>.. HUku ndio Kushindwa. Nafikiri kuwa kama wanapenda ushauri wakuulize hata wewe unaweza kuwasaidia kuliko sasa hivi.
Josh Michael
UNV of Colorado

kija said...

tuhuma zinatisha sana, na ni za ajabu kweli kweli, kwanza hao wote ni watoto wa vigogo, sasa mbona ni hatari sana, wa kwanza ni wa waziri mkuu, je watataua vipi, wakati ni mototo wa mkubwa, jamani na anajidai sana huyo mtoto pale bot, kuringia watu sana pale bot, kwani benki ni ya kwake huyo binti jamani, hata sina raha kufanay ane kazi pale bot.

Anonymous said...

kifaru said
Kwanza tuje na upande wa Kadhi na mahakam yake kwa hakika sjui nieleze vipi maana tukubali yusikubali Uislamu na Waislamu wameanza kupigwa vita miaka ya tangu Baba wataifa na kadamizo mbali mbali za siri na za dhahiri km waislamu wakihubiri watanza kupanga majina waislamu wenye siasa kali kwa sababu ya kusema kweli mashuleni watoto wanafelishwa maksudi na hawana pakulalamika na mabo mengi tu wanafanyiwa waislam hata nyadhifa za vyombo nyeti daima mkiristo atakuwa juu kabisa muislamu atakuwa nchini yake na hii ni kwa makusudi tunafanywa ili waingie chuki waislamu na yaanze mapambano lakini kiyu kikubwa cha kumshukuru Mola ni ule utulivu tulionao sie watu wa chini ambao ndio wengi,na ndio maana kukabaki salama na tunamuomba Muumba atuzidishie hi imani sote ukiwa muislam ukiwa mkiristo.Tuje bot wataendekea juchaguana wenyewe kwa wenyewe hao hta kama hana sifa za kuajiriwa maan ni mbinu mmoja wapo ya kuwacha wizi owozo wa serikali ubakie pale pale na sie walala hoi tunazidi kuumia lakini ni kosa letu watanzania kama ilivyo desturi yetu tunapenda san na kutawliwa na mawazo ya CCM kama tunataka mabdiliko ya kweli 2010 inakuja nyie sie ndio tulio na uamuzi kwenye visanduku vya kura na tulinde kura zetu bara na visiwani mikoani tuingize chama kimoja cha upinzani tuwe wajasiri na wazalendo tukipe chama kimoja cha upinzani tuwapime na wao tuone kama nchi hajabadilika.
Tuchaguwe viongozi sio watu waka nchi wal maana CMM ikibaki maisha tutabaki kuandika serikali imefanya hivi imefany vile tuwe wamoja tukipe cham tunachohisi kitasikiliza wananchi bila kujali tofauti zetu lazima na sie tusome makosa yetu ya kukingangania tu chama cha mapinduzi maana ya mapindizi ni kupinda pinda ndio maana nchi imetawaliwa na rushwa na kila ufisadi heko muandishi kamata uzi huo huo lakini uandike mabo bila ya upendeleo na usikubali, kutumia lugha za faul kama ati upinzani umedai.

Anonymous said...

Wewe Kifaru Said umesema kweli kabisa KUHUSU SUALA LA CCM maana ni aibu kubwa sana kusema tu bila la kutenda sasa wakati mwingine nasema kiuwa watanzania ndio walioshindwa maana waliwapa kura nyingi sana CCM na kuwapa kiburu za uzima na kujifanya wao ndio Mungu watu na ndio Faida ya kuchangua mafiga matatu hayo. JK ameshindwa na hata hivyo sula siyo Mikatba ya madini suala ni sheria ya madini na shughuli za madini ndiyo CCM walitengeneza sheria mbaya hivyo oyte hayo ni matunda ya CCM
Josh Michael
UNVErsity of Colorado

Reginald S. Miruko said...

nimepita hapa. Nasalimia, kaza buti . Sie tunajikongoja

bhai said...

makubwa wana kazi basi hao, sio kama scandal ya hosea, dah makubwa basi. Sasa ni nani anashughulikia, au mtafunika tu mambo haya. Kama yako kwa email, nini mnafanya. Muwaweke hao watu kwenye kikako maalumu. Na kuwashughulikia haraka sana. Wote hao, waitwe kwa wasomi na watu wanaoshughulikia mambo ya accounts.

kasi said...

jamani, mi taarifa hiyo hapo juu inanikera sana sana. Ni nini serikali inafanya, kuhusiana na hizo tuhuma lakini. mbona wamenyamaza tu. Wengine ndio hao hao, wanawasiliana na wakubwa serikalini, its about time, hayo majina yafanyiwe kazi mara moja, kabla mwaka haujaisha.

jaln said...

hivi huyo pamela anarudi kweli bot, mwakani. Jamani mtoeni, mnasema watu wanakula rushwa, na huyo pamela je?. Hivi tunarudi bot, kuendelea na mambo yaleyale, makubwa basi.

habibi said...

asanteni sana kwa haya majina, ya walanguzi wa nchi yetu, wafikishwe mahakamani haraka sana, kujibu tuhuma zao.

nino said...

makubwa, kuanzia jina la kwanza mpaka la mwisho. Wote waitwe mbele ya umma, kujibu mashtaka yao, ya ufisadi bila kujali. Wanablog amkeni jamani, kama yoyote bot ana taarifa zaidi, mwageni mbele ya umma. Tanzania ni ya wote, sio hao mafisaidi hapo juu na walanguzi, walete hizo pesa. KUweni makini, wakirudi bot hao, mtaendelea kuliwa macho macho.

jingo said...

wewe unayejiita MWANDANI wewe ni mmoja wa vigogo wala nchi nini?au upo hapo kwenye list,ndiyo maana unatetea kwa hoja dhaifu na legelege!

Butty said...

Tanzania yetu imeingiliwa na mcheezo mbaya kutoka na viongozi wetu kupenda kuridhisha watoto wao hata kama hawana sifa ili mradi wanajua kuna maslahi mazuri, Ndio maana BOT ni ya watoto wa wakubwa ambao wengine hawana sifa ya kuajiriwa hapo. Kwa kweli inauma sana kwa sisi tuliobahatika kupata elimu ya juu lakini tupotupo tu.Ningeomba serrikali yetu ione aibu maana sasa ni ngumzo ya nchi itoe tamko kuhusu suala hili.

Innocent said...

Kweli ni ngumu sijui kama tutafika.Je wana viwango vya kuajiriwa, dodosa utuambie mzee.

baloi said...

nakubaliana na watanzania wote mliotoa maoni hapo juu, hao waliotajwa kwa ufisadi wala msisite kuwasema mbele za watu jamani. Ni hatari sana sana, tena sana, na wahusika msikae kimya jamani waleteni mbele ya sheria haraka sana, msiogope wadhifa wao, kila mtu ana haki tanzania. Ombeni kazi pale bot, hao viongozi ni nyie mmewawela madarakani, wapiga kura ni wananchi.

kamo said...

kweli sina imani kabisa. wapo hapi hao jamani, kama na ndugu zao wanahusika wasemwe kabisa na tuhuma zao, safi sana aliyetundika hiyo list hapo juu. mwaka ndo unaisha ivyo, harakisheni jamani.

makoi said...

na kweli wamezidi sana, wafanyieni kazi ipasavyo, walanguzi hao, mnawaachia hivi hivi tu.

edward alex mkwelele said...

I HAVE NO BIG DUDE AT ANYWHERE IN THE SYSTEM, I HAVE AN MBA FRO UK BUT I COULD NOT FIND A JOB IN MY OWN COUNTRY TANZANIA, IT IS NOT JUST AN MBA BUT WITH 10+ EXPERIENCE IN BANKING, HALI NI MBAYA HADI UWE MTOTO WA KIGOGO NDIPO UPEWE KAZI TENA KWA KI-NOTE TU SI INTERVIEW, WEWE UKIWA KAJAMBA NANI SAHAU KAZI KUPATA HATA KAMA UNA PhD HALI NI MBAYA YANATAKIWA MABADILIKO YA HARAKA KAMA ENZI ZA MWALIMU KILA MTU ALIKUWA ANAPATA KAZI BILA UBAGUZI SASA NI HATARI KWA NINI WATU WANA MIOYO HII.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'