Tuesday, November 06, 2007

Kikwete mfa maji?


Usimshangae Rais Jakaya Kikwete. Huu ni mkakati wake. Wakati mawaziri wametoka mikoani majuzi kulaani kauli za wapinzani kwamba ni uzushi, yeye amesema wapinzani wasipuuzwe. Na baada ya kuona wananchi wanapuuza hoja za utetezi wa CCM na kukumbatia za wakosoaji kuhusu masuala ya madini, sasa rais anataka kuunda kamati ya madini itakayowashirikisha hata wakosoaji wake hao hao. Je, anataka kuwaziba mdomo wanaoikosoa serikali? Na tayari ameahidi kuwapa hela ya kutosha na ziara nje ya nchi kwa kazi hiyo. Ni hongo? Anataka kumaliza nguvu za upinzani kiujanja ujajanja? Au ndiko kutapatapa kwa mfa maji?

5 comments:

Kejo said...

hobger Ngurumo. Makala yako inasema ukweli mtupu. Huu ujanja ujanja wa Kikwete tumeshaujua. Anataka kutuchekea huku watu wake wanatubia. Hatukubali hadi hapo atapokuwa amewashugulikia.

Anonymous said...

Makala ya jana Tanzania Daima umesema ukweli kabisa juu ya CCM na mchezo wote wa Siasa za huko Tanzania. Sikiliza Hotuba ya Kikwete kama vile yupo kwenye kampeni vile.. Huo sio wakati wa kusema kuwa tutajenga barabara ua tutafanya hivi. Kukubaliwa Kikwete katika hili ni ushaidi tosha kuwa vyama vya upinzani umeonyesha kuimarika zaidi ya siasa hata hoja. Sasa hao mawaziri ambao walikuwa wanasema uongo waziwazi juu ya Upinzani. Umeonyesha mengi na kusema mengi na hivyo leo kufanya au kusema baada ya kelele za wananchi toka kambi ya upinzani. Jk anasoma alama tu lakini hakuna jipya huko katika serikali ya CCM hivyo kusema tu alikuwa anasema toka wakati hutoba yake ya kwanza bungeni sasa amefanya nini?? Toka mwaka wake wa kwanza. Hivyo hizo ni porojo za kisiasa tu. Kusema bila ya kutenda ni sawa na hakuna kitu. Jk ameshindwa anahitaji kusaidiwa sana toka upinzani na sio CCM. Kukubali kwake yote ni sawa na kusema kuwa sera zao zimeshindwa. Hivyo SIKILIZA HUTOBA ZAKE> NI SAWA KABISA NA MWAKA JUZI. Then kuna matatizo katika center ya serikali katika matumizi na ukubwa wake.
Josh Michael
Colorado

Anonymous said...

Ndugu yangu Tatizo kubwa ni kuwa sasa hivi kuna watu wanafanya usanii tu katika siasa huko. Hivyo Tatizo sio kamati Tatizo ni Sheria za madini na hivyo hata kama wataunda kamati but wameingia tayari mikataba hiyo.... kama wanataka hivyo ni sawa na kuvunja mikataba na itakuwa ni ukiukwaji mkubwa sana katika sheria za kimataifa. Leo tunasema hivyo lakini kutakuwa na tume hiyo but hakuna jipya katika hili. wewe jiulize kitu kimoja toka aseme kuwa anapitia mikataba lakini watu wake na serikali yake ndio kwanza imeingia mikataba mengine?? yeye alikuwa hajui. Then Hapa cha Kujiuliza kuwa CCM imekuwa Madakani kwa Miaka 45 sasa hivi. Hivyo umaskini wa watanzania ni Wao ndio chanzo.. Hivyo. sioni kipya
Joshua Michael

Mlalahoi said...

Na atakufa maji kwelikweli. JK mbabaishaji na muongo mkubwa.

dibal said...

jakaya ana macho yanaona vizuri kweli. Au ana macho mia mia ndani ya ccm. Je ana agenda gani sana, hebu atuambie sisi wananchi, kwani dunia haina siri, mabomu yatalipuliwa kama hawi makini. Niseme nisiseme.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'