Friday, April 18, 2008

Spichi 'Tamu' ya Raila Odinga


Nimeisoma hotuba ya Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, baada ya kula kiapo. Ni kauli nzito yenye ujumbe murua kwa Wakenya. Na inamtia katika wakati mgumu iwapo hatatimiza alichoahidi. Nikiitazama kwa kina, ni kama vile ndiyo alikuwa amejiandaa kutoa siku ya kuapishwa kuwa rais, lakini ameibadili kidogo ikawa ya waziri mkuu. Nimeilinganisha na hotuba ya Rais Mwai Kibaki ya siku hiyo hiyo, katika tukio hilo hilo. Tofauti iko wazi. Kila la heri Wakenya! Pichani juu ni vigogo wa Kenya: (Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka, Rais Mwai Kibaki, Waziri Mkuu Raila Odinga na Naibu Waziri Mkuu, Musalia Mudavadi).

3 comments:

Sam said...

Kalonzo Musyoka ndiye ameharibu picha hii. Msaliti mkubwa yule!

Anonymous said...

Mbowe atakuwa Raila wa 2010

Anonymous said...

Tunasubiri kazi, sio kuvaa suti na kuchekelea tu!

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'