Tuesday, April 01, 2008

Mugabe kama Kibaki?


UCHAGUZI Mkuu wa Zimbabwe unaelekea kwenye mkondo ule ule wa Kenya. Tume ya Uchaguzi inatoa matangazo kwa jinsi inayotia wasiwasi. Lakini dalili zinaonyesha upinzani umechukua viti vingi zaidi au umeshinda. Baadhi ya taarifa zinasema hadi sasa, upinzani umepata viti vingi zaidi (74); chama tawala ZANU-PF cha Rais Robert Mugabe kina viti 64. Mawaziri watatu wa Rais Mugabe wameangushwa. Kura za urais bado ni siri ya tume, lakini upepo unaonyesha mambo ni magumu kwa Mugabe, na tetesi ni kwamba tume inajaribu kumfanyie kile ambacho ile ya Kenya ilimfanyia Mwai Kibaki, ikamtangaza mshindi akiwa na kura chache zenye utata. Taarifa nyingine zinasema tayari Mugabe ameshajulishwa kwamba ameshindwa, na watu wake wanajadiliana namna ya kukabidhi madaraka kwa mshindi. Maana tayari upinzani umeshaanza majadiliano na majeshi ya Zimbabwe. Tusubiri!

3 comments:

Anonymous said...

Sikio la kufa...

Anonymous said...

Mambo bado, mzee mzima kashindwa lakini keshaitisha kikao cha kuandaa 'mapinduzi' kwa kutumia marudia ya kura!

Anonymous said...

Mugabe aibu tupu. Kama Karume vile!

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'