Sunday, October 19, 2008

Wananchi wamechoka

'Fujo' za wananchi dhidi ya viongozi wao na watawala zina chanzo na maelezo. HII HAPA ni sababu mojawapo. Soma pia makala ya Maggid Mjengwa akinikosoa na kuniambia Rais hapigwi mawe. Usikose pia majibu yangu kwake, mwendelezo wa mjadala katika makala isemayo: Hatuvunji nyumba, tunabomoa mlango. Na wewe toa maoni yako.

8 comments:

Fita Lutonja said...

Ansbert Ngurumo mambo yako safi lakini kumbuka kuwa Tanzania inaangamia polepole katika dimbwi la umasikini sasa nani ataikomboa?

Anonymous said...

Ngurumo anakumbuka hayo na ndiyo maana anaandika hivi, kutukumbusha na sisi na kututia moyo. Umeelewa?

Anonymous said...

kuna siku rais atapigwa amwe tena hapa jiini tutaambiwa na salva kwamba si mawe wananchi wanampenda rais wao na walikuwa wanamshangilia kwa kumrushia apples kama si mayai............!
siasa na sanaa!

Anonymous said...

kuna siku rais atapigwa mawe tena hapa jiini tutaambiwa na salva rweyemamu kwamba si mawe wananchi wanampenda rais wao na walikuwa wanamshangilia kwa kumrushia apples kama si mayai............!
siasa na sanaa!

Anonymous said...

Ansbert,
Naona kimya kidogo.
Nitakutumia kwa email makala niliyoiandika na kuchapwa na Raia Mwema kuonyesha mapungufu ya hoja yako kwa adhma ya kutia chachu mjadala huu.
Kazi Njema.
Maggid

Ansbert Ngurumo said...

Maggid nitumie makala hiyo niisome. Ansbert

Anonymous said...

Ansbert,
Nimerudia kusoma makala yako baada ya kumsoma Maggid. Nakiri sikubaliani na mapungufu wala kasoro kama yalivyoainishwa. Maggid, baada ya kauli ya msemaji wa chama tawala atakubaliana na wewe kuwa alikurupuka. Sikosi makala zako na nakubaliana na uchambuzi wa zote, labda ukiacha zile zinahusicha kifo cha Amina (MHSRIEP) na nguvu za giza!
Go Ansbert!

Anonymous said...

Huyu jamaa Ngurumo hana tofauti na wale jamaa tunaowajua TZ. Wanaopenda kupinga kila kitu na kufanya maandamano yasiyokuwa na maana kila siku.
Ambao sisi huwa tunawaita "siasa kali", ndo huyu jamaa Ansbert.
Kuandika kwa jazba na hasira kila siku na kusema unasema ukweli sio sahihi.
Makala zako nyingi nimesoma na zote huwa "ear-says".
Ninakubaliana na maneno unayokuwa ukisema kwa kiasi cha asilimia 50 na asilimia zilizobaki sikubaliani nawe. kwani habari zako nyingi huwa hazina ukweli halisi, bali maneno mengi ya mtaani ya watu wenye maisha mema, ambao huwa wanajifanya wanaifutilia seriklai kwa manufaa ya watu wote.
Hebu nieleze kilio cha mama wa kijijini Nalupe kule Mtwara , ukimweleza kuna EPA au mafisadi Dar ,itamsaidia nini au vipi leo hii hii. Maana ya kusema hivyo ni kwamba utajitahidi kumwambia hizo fedha zisingeiibiwa basi yeye angepata maji safi na mtoto wake kwenda shule nzuri. Hii ni baada ya kumuelezea sana , lakini kwa lugha fupi yeye hayo maelezo ameshayasikia sana katika miaka yake 40 na zaidi toka tumepata uhuru. Na hakuna hata la maana alilopata toka wakati huo.
Shule iliyojengwa na mkoloni, ndio aliosoma yeye hadi watoto wake hadi wajukuu. Mto alokuwa akichota maji yasiyo mazuri ndio aliokulia yeye na kukuza watoto wake nk.
Njia inayoenda shambani kwake ndo ile ile miak nenda miaka rudi. Nyumba yake ni ya nyasi na mbuzi wake wamepungua kutoka 20 hadi 4.
Hakuna lolote jipya, ila huo mji wa jirani ambao zamani ulikuwa kijiji cha biashara na mauzo yake ya Korosho sasa unaitwa wilaya mpya ya Ruangwa unakuwa kila siku kwa hela za Rushwa za hao mafisadi. Yeye kijijini Nalupe hana umeme wala maji safi ya kunywa wala chakula cha kutosha mwaka mzima.
Hivyo wewe kuisema serikali ni mtindo wako wewe wa kutaka "kupata share ya pie" kutoka kwa mafisadi hao hao ,ili usiwaandike na kuendelea kula nao pamoja .Ilihali kutuacha sisi wanakijijiwa Nalupe tukiumia na matatizo yetu miaka nenda na miaka rudi.

Nimesoma sana makala zako na mara zote huwa ni lawama , hakina suluhisho hata moja. Kwa mfano umemfuatilia nani katika hao mafisaidi kwa video au habari na kutuonyesha nyumba zake au miradi yake ambao inahusiana na wizi huo.
Na kuomba serikali ichukue nyumba hizo moja kwa moja, bila kupitia mahakamani, kwani wewe na mimi tunajua ni za kupitia fedha za kifisadi.
Inakuwa ngumu kwa sababu
tunajua fisadi ataenda mahakamani na baada ya muda mrefu wa sheria atashinda hiyo kesi na kurudishiwa mali zake. Sasa huo ufisadi unaousema uko wapi, kama mahakama inaweza mpa mali zake?, kupitia mkono wa sheria.
Mimi binafsi naamini kama wewe unavyoamini juu ya mafisadi kwamba hata Wewe mwenyewe umeishi kwa rushwa na ufisadi wa kiutapeli hapa na pale na unataka kutufisadi sisi kwa kutumia kalamu yako ili upate matawi ya juu na kutuacha sisi walala hoi bila bila.
Ansbert sikuamini hata wewe, mana nakuona ni mmoja wa hao hao.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'