Monday, June 21, 2010

Siasa za JK na mwanaye

RAIS Jakaya Kikwete amemkabidhi mtoto wake Ridhiwani, fomu za kumuombea wadhamini 250 kwa mikoa 10 nchini ili kutimiza vigezo vya kuwa mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika nyumbani kwake mjini hapa ambapo zaidi ya vijana 40 watakaoongozwa na Ridhiwani walihudhuria. Mtoto huyo wa rais Kikwete, amechaguliwa kuwa kiongozi wa vijana katika kuhakikisha mgombea huyo anapata wadhamini wa kutosha kwa mujibu wa sheria na kanuni za CCM.

Kwa habari zaidi soma magazeti. Mzee wa Maswali Magumu amelijadili hili kwa kifupi.

2 comments:

Anonymous said...

Mbinu hii si mpya, tumeizoea; ilitumika tena mwaka 2005 na vijana 'walikamatwa' kweli kweli kwa ahadi ya kupatiwa ajira.

Baadhi ya wapambe mshuhuri wilayani ambao walimsaidia Ridhiwani kukamilisha kazi aliyokuwa amepewa na baba yake, waliambulia nafasi katika Umoja wa Vijana wa CCM - mfano mzuri ni kijana aliyehusika sana katika zoezi hili wilayani Bagamoyo.

Anonymous said...

CCM ya sasa ni chama cha wana familia..watu ambao wamefahamiana, wakawa family friends na wanaendelea kurithishana,,,najua ni wavivu wa kuona mbali na kuangalia madhara ya kila amuzi wanalofanya ila haya ndio yalivunja KANU..rejea siasa ya Moi na mtoto wa Kenyata...

watu wanaomjua Ridhwani wanakubali kwamba hastahili (Ki-uelewa, usafi, n.k) kupewa madaraka aliyonayo ila kwa vile kuna watu pia wananufaika kupitia yeye basi na hatutasema kitu...hadi leo hatujui ni vigezo vipi vimetumika hadi yeye kupewa madaraka ya juu kwenye umoja ambao ulitakiwa kua uti wa mgongo wa taifa

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'