Thursday, November 18, 2010

Chadema wamkataa Kikwete hadharani

Chadema wamesisitiza hoja yao ya kukataa matokeo ya urais kwa sababu za uchakachuaji. Mdau mmoja, Bartholomew Mkinga, ameamua kufafanua uamuzi wa Chadema kumkataa rais, na kuendelea na shughuli za Bunge. Anasema:

"CHADEMA haijatamka kuwa haimtambui Kikwete kama Rais wa Tanzania, bali hawayatambui matokeo ya uchaguzi yaliyompa Kikwete mamlaka ya kuwa rais. Kwa tafsiri rahisi, ni Kikwete hana tofauti na marais wan chi nyingine wanaotumia mbinu mbalimbali kuupata urais bila ridhaa ya wananchi wanaowaongoza; amewekwa madarakani na tume ya uchaguzi, si wapiga kura.

CHADEMA haiongelei matokeo ya kura za ubunge kwa vile sheria inaruhusu kuhoji matokeo ya ubunge kwenye vyombo vya kisheria. Kwa hiyo, CHADEMA inategemea kuhoji matokeo ya kura za ubunge katika majimbo kadhaa. Kwa upande wa urais ni tofauti kwa vile sheria hairuhusu kuhoji matokeo ya urais mara tume ya uchaguzi ikishayatangaza. Kwa hiyo, jitihada pekee inayoweza kutumika ni ya kisiasa.

CHADEMA hawatahudhuria matukio yote mawili kama njia mojawapo ya kuonesha kutokuridhika na kile kilichofanywa na tume ya uchaguzi ya kuhujumu demokrasia."

Katika tukio la hivi karibuni, Alhamisi wiki hii, wabunge wa Chadema wamesusa hotuba ya Kikwete Bungeni. Mara tu alipoinuka na kuanza kuhutubia, wabunge wote, wakiongozwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, wameondoka, wakimwacha Kikwete mdomo wazi. Kikwete amelazimika kuhutubia wabunge wa CCM, CUF, TLP na NCCR-Mageuzi.

2 comments:

Stella said...

Asante kwa tafsiri hii nzuri. Lakini inaelekea JK, Pinda, Tendwa na viongozi wa vyama vingine vya upinzani hawaelewi nia na dhamira ya CHADEMA.

Kejeli walizozitoa JK na Pinda kwa nyakati tofauti wakati wakilihutubia Bunge zinaashiria watu wasiofahamu kuwa wananchi wote ni raia wa Tanzania, wawe wananchama wa CCM, CHADEMA, CUF,TLP, NCCR, n.k. Hawa wote wanahitaji maendeleo yao na ya nchi yao Tanzania. Kwa JK kusema kuwa eti wabunge wa CHADEMA wataifuata serikali ya CCM kuiomba maendeleo ya wananchi wanaowawakilisha ni dalili ya kuumizwa na msimamo wa CHADEMA. Ni mbinu za kulinda nafsi kwa kujipa 'kanuni raha'.

Wabunge hawataenda kuomba kana kwamba si haki ya wananchi, bali watahitaji maendeleo ya wananchi katika majimbo yapatikane ili kuboresha maisha wa waTanzania wanaowawakilisha.

Anonymous said...

Vielen Dank für dieses Posting, war es sehr hilfreich und erzählte viel

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'