Wednesday, November 03, 2010



Dk Slaa amesema kuwa matokeo ya kura za urais na ubunge yanayoendelea kutangazwana Tume ya Taifa ya Uchaguzi yamepikwa na Idara ya Usalama wa Taifa. Aliwaambia waandishi wa habari, makao makuu ya chama chake, kuwa Chadema kimefuatilia na kugundua kuwa takwimu za matokeo zinazotangazwa na Tume hazifanani na zile zilizo majimboni na kwenye kata, kutokana na idadi ya kura kutoka vituo vya kupigia kura. Alitoa mifano kadhaa, ukiwamo wa Geita ambako Chadema kilipata kura zaidi ya 22,000 za urais, lakini Tume ilitangaza kwamba kilipata kura 3,000.

Kwa sababu hiyo, Dk Slaa aliitaka Tume kusitisha mara moja utangazaji wa matokeo ya urais na kuandaa upya uchaguzi wa rais. Alimtaka pia Mkurugenzi wa Idara ya Usalama ajiuzulu kwa sababu amekipendelea chama kimoja badala ya kujali maslahi ya taifa.

5 comments:

Anonymous said...

Nadhani tusipeleke siasa mbali namna hiyo... anachocharibu kukifanya DR Slaa ni yaleyale ya Zanzibar 2000.. hayana tija. Utawajaza ujinga wahuni, wataingia mtaani wafanye fujo, mara risasi zitaanza kurushwa na miji haitakalika.. Acha kuchochea vita Dr Slaa.

Hadi hapo ulichokifanya kinatosha, otheriwse mengine ni uroho wa madaraka na kutaka kuvunja amani. Kua mstaarabu. Wewe ni mtu tajiri, ikianza vita watoto wako utawafungia ndani ya gate,, watakaoumia ni watoto wa kina sisi.. Kuna kesho pia, usikate tamaa. Mengine muachie mungu

Anonymous said...

Wewe mtoa mawazo wa kwanza, nadhani unachoongea hukielewi. Dr. Slaa hayasemi hayo kwa nia ya kuwafanya wananchi wafanye fujo na kuvuruga amani. Bali ni kujaribu kuonyesha ni kwa kiasi gani CCM kwa kushirikiana na Idara za serikali zinavyoshindwa kuweka utaifa mbele na kulinda maslahi ya watanzania wote. Hujiulizi athari za kukubali matokeo haya bila ya kuuliza madhumuni yao ni nini? Kumbuka watanzania ni watu waelewa na tunahitaji huduma bora za Afya, Elimu nzuri na yenye kutufanya tuendelee mbele katika sekta zingine za maisha, miundombinu mizuri, kujenga uchumi mzuri na shirikishi bila ya kuwabagua wengine. Hayo ndio madhumuni ya watanzania. Sasa, malengo hayo yatatimia kwa kukaa kimya na kuwaacha mafisadi wetu wakuu waendelee kuchakachua kura? Kuwaacha viongozi na baadhi ya idara za serikali ziwasaidie kuwepo madarakani kwa faida zao binafsi? Please, kionee huruma kizazi kijacho na jamii yote ya watanzania. Ububu, ni kitu kibaya, mtazamo ya kwamba ukidai haki basi wewe ni mpenda madaraka, mroho na mwenye nia ya kujitajirisha. Tuache ubinafsi wa kifikra, tunapohisi tunadhulumiwa na hawa watu tuseme na tupeane moyo. Ikitokea shida ya afya wote tuaathirika, miundombinu mibovu ni sisi sote na pia elimu bora ni yetu wote. Tumuunge mkono Dr.Slaa katika madai haya mazito. idara zetu ziache kuchangany'a siasa na profession zao, wapo kulinda maslahi ya nchi na uzalendo utawale. Kama Kikwete ni dhaifu, jamani, idara hizo zifanye fair, ang'olewe kama hayo ndio matakwa ya wananchi. jamani nyie ndio mtakao kuwa chanzo cha fujo na machafuko kama hamtajali maslahi ya walio wengi. Ahasante.

Anonymous said...

Naomba nikujibu wewe mtoa maada wa pili, uliyejaribu kujibu hoja yangu..

Wakati wa kampeni, Dr Slaa mwenyewe alinukuliwa akisema nusu ya ma-afisa wa usalama wa taifa wamareport kwake na hivyo kama alikua anasema ukweli, basi haiwezekani akaibiwa kura hata moja.

Tusichochee mapigano kwa visingizio vya ufisadi na maisha duni ya watanzania. Hiyo sio njia endelevu. Nitakupa mfano rahisi.

Mwl Nyerere aliomba uhuru wa watanzania kwa njia ya kiungwana na kistaarabu. hakuwatukana wakoloni, na wala hakuwalazimisha wananchi kuuunga mkono juhudi zake, bali aliwaambia kwa nini alikua na uwezo wa kuiongoza tanzania na watu wake kwa ujumla.

Dr Slaa ameshindwa kuwaambia kimahesabu wananchi ni kwa nini bado tuko nyuma kimaendeleo, badala yake amekua akiwachonganisha baadhi ya watu na wananchi. Sio siasa ya mtu mwenye hekima hiyo. Na sio njia sahihi ya kuomba uhuru wa masikini wengi wa tanzania.

Msemo wa kwamba haki inadaiwa/tafutwa ni mzuri kwa watu kama Dr slaa mwenye uwezo kifedha, wa kuwakimbiza nje ya nchi watoto wake pale vita itapoanza..

Mwanamziki 2pac shakur aliwahi kusema msemo mzuri sana na wenye hekima, kwamba; "I'm not saying i will change the world but, I guarantee you, i'll spark the minds that will change the world.

Ni vyema Dr Slaa akapandikiza mbegu bora zitakazozaa kina nyerere wapya badala ya kupandikiza mbegu zitakazozaa kina jonas savimbi au kina maalim Seif wapya.. hii ni dunia ya leo, tunaenda kwa mahesabu. Sio kuongea tu kitu ambacho unajua watakao umia ni hohe hahe.. Mwl nyerere hakutaka siasa yetu ifikie hapo, ila alipenda sana mageuzi. tumuenzi..

napenda sana mageuzi ila sikumpigia kura dr Slaa kwa sababu sikusikia sera yake ya maana zaidi ya kutaja taja majina ya watu na kuwadhalilisha wananchi wengine kwa ajili ya kukiongezea ruzuku chadema. Niliona bora niharibu kura yangu. tafakari

Anonymous said...

....Hata jeshi liliamua kuwa upande wa CCM sembuse USALAMA wa TAIFA!?

Anonymous said...

....Hata jeshi liliamua kuwa upande wa CCM sembuse USALAMA wa TAIFA!?

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'